Sikiliza Mjomba...

Asante MM,
Leo unaweza kuonekana mwenye kichwa kidogo, lakini ukweli unatabakia siku yaja na Tanzania itakukumbuka!
God bless you.

sauti zetu zitanyamaza na siku moja hata vidole hivi vitakoma; na ndipo yote tuliyoyasema yatabakia kama ushahidi wa jinsi tulivyolipenda taifa letu na watu wake.
 
Well done mwanakijiji.It touched the very bottom of my heart.
Its my solemn prayer that "mjomba" will heed the words.
 
sauti zetu zitanyamaza na siku moja hata vidole hivi vitakoma; na ndipo yote tuliyoyasema yatabakia kama ushahidi wa jinsi tulivyolipenda taifa letu na watu wake.


Safi sana,

Ndo maana siku moja nilikushauri kuwa unaweza kujifanya kinyonga ili ubadili mikakati. Huu ujumbe utafika na naamini unakubalika hata kwa vichaa wa vijiweni kwa sababu unatumia lugha yao. Kwa hiyo ombi langu ni lile, jaribu kuweka nondo zako kwenye audio ili wale (na ndio tulio wengi) wasiopenda kuumiza macho yao wakapate ujumbe pia.
Bravo bro,
The roaming DC
 
So sad! Sikio la kufa...huyu mjomba kama hakuzaliwa na mama yetu! Hata kama amekuwa kiziwi ukubwani tuseme tu hata kwa ishara! MM - good stuff!

"Our Lives begins to end the day we keep silent about things that matter"
- Dr. Martin L. King, Jr.
 
Hongera sana Mwanakiji kwani ni ujumbe murua kabisa ingawa mjomba wako ni Kiziwi.

Hata kama ni kiziwi kuna siku atasikia tu kama sote tukipaza sauti zetu.,huwa naamini hakuna sikio gumu linaloshindwa kusikia sauti ya vinywa vingi vikizungumza kwa pamoja.
 
Mjomba anatuangusha kweli.,kama hawezi kusoma hata picha pia hatazami?.,mbona wala haihitaji PhD kujua jinsi hali ilivyo mbaya?...
 
aah nimeumia sana, nimefadhaika sana, utenzi umenigusa moyoni, chozi limedondoka kwa msisimko, nimekwazika, nimepata kwikwi, imenichukua dakika kumi kuweza kurejea katika hali yangu ya kawaida, ijapokua ni maudhui tuliyoyazoea kuwa Raslimali zetu zafujwa na watawala , wanapiga makofi.
ASANTE KWA UJUMBE
 
Hauwezi kushirikiana na msanii yeyote wa hapa kwetu bongo ukatoka hata kwenye audio cd?. Naamini vipo vituo vya radio hapa nchini vinavyoweza kuthubutu kuupiga. Sasa hivi kuna taarab moja inachezwa ITV inampamba kwelikweli JK wakitumia hadi picha za Mwalimu.
 
Utenzi umekaa mahali pake. Mjomba hataki kusikia haya yote. Akirudi kijijini kuomba kura asipewe tena.
Ni lazima atarudi kijijini kuomba kura, asivyo na haya ata katika maeneo aliyouza ataonekana akipitapita na kuwashawishi watu wamkubali, japo hana huruma na ndugu zake.
 
It's said, VOX POPULI VOX DEI, hivi hata Tz huu msemo na imani vinaishi kweli? Mbona vilio na kelele zote hizi hayo 'masikio ya kufa' ya watawala hayazisikii?
 
Kweli imeni touch sana inauma kuona mali asili zetu zinakwisha huku mjomba kaziba masikio imenikumbusha wakati tunapigania ukombozi Afrika kusini tunaimba nyimbo za kulaani makaburu it is very sad

Jaribu kuongea na radio studio hata wapo radio wanaweza kuupiga na wananchi wengi wausikie nimeumia sana nikikumbuka enzi zile tunaimba nyimbo za ukombozi NCHI YANGU TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE umejaliwa mito bahari misitu na madini lakini sasa yanakwisha big up MMKJ
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom