Sikiliza kipindi - sheria mtandao ( cyberlaw )

Status
Not open for further replies.

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Kipindi – Maisha na Teknohama - Sheria Mtandao – 1

Karibu kusikiliza Kipindi cha Maisha na teknohama leo tulizungumzia Sheria Mtandao ( CYBERLAWS ) hii ni sehemu ya kwanza ya kipindi hichi , Sehemu ya Pili Ni jumapili ijayo .

Click

Hotfile.com: One click file hosting: SHERIA NA MATUMIZI YA TEKNOHAMA-01_08_2010.MP3

Click Regular Download Subiri sekunde 60 kisha Download

…………………………………………….

Click

RapidShare: 1-CLICK Web hosting - Easy Filehosting

Click Free User Subiri Sekunde 60 Kisha Download .
 
Hizo link ulizoweka hauvunji sheria? Sijazifungua, bado natafakari.
 
Sheria za wapi ?
Umesahau ulichowahi kuandika?

Hivi umeshaona tovuti yoyote inayouza au kusambaza programu bandia imeweka link ya tovuti halali ya mtengenezaji wa programu halali wa programu hiyo au msambazaji ? umeshawahi kujiuliza kwa nini mara nyingi tovuti hizi au forum hizi huwa zinaweza links kwenda kwenye tovuti au forums ambazo zina vitu hivyo hivyo batili au bandia .

Kwa sababu katika zile tovuti halali za programu husika au wasambazaji waliodhibitishwa wameweka masharti kuhusu matumizi ya tovuti au forum zao pindi mtu mwingine unapoamua link nao kwanza uhakikishe tovuti hiyo haihusiki na hujuma au chochote ambacho si halali au kwa namna moja au nyingine mambo ya tovuti yako au forum yaendane na tovuti husika .

Mwaka juzi ulikuwa ni mwaka wa mfumuko wa tovuti nyingi na blogu nyingi kwa Tanzania miaka hiyo ndio ambayo blogu ya zeutamu ilianzishwa pamoja na zingine nzuri ambazo zina maadili na zingine zisizokuwa na maadili kwa nchi yetu zote zilianzishwa wakati ambapo nchi ilikuwa haina sheria za kuweza kudhibiti viwango vya blogu , forum na tovuti hizo kwa watumiaji wa ndani ya nchi .

Mfano kuna tovuti moja ilikuwa inaitwa dinalici hii ilianzishwa na mdada mmoja angalia forum yake kwa kutembelea JUKWAA LA WANAWAKE WA BONGO , zamani kidogo blogu ya zeutamu pamoja na zingine ambazo hazina maadili ya kitanzania waliweka links zao na baadhi ya makala za blogu ya dinalici , baada ya dina kushituka akaweka tangazo kwenye blogu yake kwamba tovuti au blogu yenye mahadhi ya ngono isilink chochote na blogu au forum yake kama akigundua hivyo atashitaki katika vyombo vya sheria .

Walipoona tangazo hilo basi hizo link zikaondolewa mara moja , lakini kwa siku za karibuni kumetokea watu mbali mbali kuanzisha blogu , au tovuti Fulani au forum za majina yanayofanana na blogu zingine au forum zingine na kulink mara nyingi blogu hizi zinakuwa hazina nia njema kama yule mwanzilishi wa mwanzo kabisa wa blogu au forum husika .

Tatizo nimegungua tovuti zinazokubali kufanyiwa links za aina hiyo unakuta katika sheria za matumizi ya forum hizo au tovuti hizo hawajasema lolote kuhusu mtu mwingine au kikundi anapoamua kulink nao kwa njia yoyote kama ni kosa na kama wakifanya hivyo wanaweza kushitakiwa , kwahiyo watu wanalink wanavyotaka .

Kwa sababu imeonyesha kwamba serikali inashugulikia sana tovuti au blogu zinazoandika masuala binafsi basi watu hawa wanachofanya ni kutafuta mada zinazohusu masuala binafsi na kulink na blogu zao ili watu waanze kujadili kupitia blogu zao lakini kwa kutokea mtandao mwingine ila kwao wako huru zaidi kutukana na kutumia lugha zingine chafu na za kudhalilisha .
Kama umefuatilia masuala ya habari kwa siku za karibuni utaweza kuona mambo yanayoendelea katika mitandao hii haswa inayotumiwa zaidi na idadi kubwa ya watanzania , kwanza ilianzia kwa ile habari ya mwendeshaji wa tovuti ya zeutamu kukamatwa .

Habari hii iliripotiwa kwa mara ya kwanza na tovuti ya chemponda ambaye amewahi kufanya kazi na gazeti la daily news kwa muda wa miaka 10 hivi kabla ya kwenda marekani , katika blogu yake hakuandika habari hiyo aliipata kwa nani mwanzo , ila huyu ni mwandishi nguli alikuwa anajua kabisa anachofanya ni nini .

Watu wakachukuwa habari hiyo wakatumiana na kuweka link kwake , watu walipotembelea blogu yake baada ya masaa 10 akatoa habari hiyo na kusema alipatiwa kwa njia ya email tu hawezi kudhibitisha kisha akaweka link ya kwenda katika forum ya JF kwa makusudi kabisa ,ukisoma sheria za JF haziongelei chochote kuhusu linking .

Huyu aliona kafanya kosa kwahiyo ikabidi arushe mpira kwa wengine kama nilivyosema huyo ni mwandishi nguli haiwezekani aweke post ile kwake bila sababu za msingi , au yeye ndio alituka hadithi hiyo kwa maslahi yake au alikuwa anataka kuitangaza JF kwa makusudi kwa mkataba maalumu alikuwa anamtangaza nani ?

Siku za karibuni pia kuna wengine wakaanzisha Blogu yao kwa kutumia jina jf pamoja na kujua jina hilo limesajiliwa wao wamefanya hivyo na kuweka link ya jf kwao kama vile zinahusiana kwa namna moja au nyingine ingawa jf imeshatoa tamko dogo walitakiwa kutoa tamko kubwa na zito pamoja na kubadilisha baadhi ya sheria za kulink forum yao na wengine wa nje .

Kulink ni kosa kama hiyo link inapotosha watu au kundi Fulani la watu kama unalink basi weka habari sahihi bila kupindisha habari au sehemu yoyote ya maelezo ya habari husika .

Ni wakati sasa wadau wa forum na tovuti hizi pamoja blogu kwa Tanzania kuanza kufikiria mara nyingi kubadilisha baadhi ya sheria za forums , tovuti na blogu zao ziendane na wakati huu ili kuepuka usumbufu kama nilivyojionyesha kwa wakati wa sasa .

Pia ni vizuri waendeshaji wa forum na tovuti au blogu hizi kama zinahusu masuala ya jamii basi wawe wanakutana mara kwa mara kujuana na kubadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu forums hizi kujenga mshikamano na uaminifu kati ya pande zote sio kama sasa ambapo wamiliki hawa wanaogopana au mmoja akienda kwenye forum ya mwenzake ni kutukanwa na kudhalilishwa

Kwa bahati nzuri mimi nimewahi kukutana karibu na waendeshaji wote wa blogu hizi , forums na tovuti hizi nitaweza kutoa ushirikiano mwingi kutokana na uzoefu wangu katika mambo haya ya mahusiano .

Lazima tushirikiane kutokomeza tabia hizi na kujenga jamii imara
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom