Sikia hii ya mama Mkwe...UNGEFANYAJE HAPA?

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,027
Hii nimeisikia leo Radio flani tanga:

Kuna njemba moja alioa msichana mmoja mzuri tu, huyu dada mama yake alikuwa RPC(Mkubwa wa Polisi), ndoa yao ilifana sana. Baada ya miezi michache matatizo yakaanza katika ile ndoa. Yule binti akawa analalamika kwa mme wake kwamba kabadilika na mara nyingi huwa anarudi usiku sana, matunzo sio mazuri, muda mwingine hata fedha haachi.

yule dada baadaya kuona hamna mabadiliko kwa mme wake akaamua kumshtaki yule jamaa kwa mama yake yule Polisi.(Mama Mkwe wa huyu jamaa). Kwa sababu mama mkwe anaheshima sana sehemu yoyote, basi busara ilitumika na yule jamaa akaitwa na Mama wa yule dada, jamaa akakalishwa chini na akaulizwa inakuaje siku hizi unarudi usiku sana na complain nyingine, jamaa akajitetea kwa kudai kazi tu nyingi kutafuta hela n.k, na akadai atajirekebisha, yakaisha.

Sasa siku moja kutokana na utaratibu wa jeshi la Polisi kugundua wazamiaji, wakaamua kufanya utaratibu wa kukagua gesti za mtaani usiku(huyu mama akiwa ndio mkubwa wa msako), sasa guest walipoenda wakaamuru mapokezi kuorodhesha wageni wao walikuwa vyumbani, na badae kwa utaratibu wa kawaida wakaamua kupitia chumba hadi chumba kuuliza uraia wa wageni mule hotelini/guest.

Sasa mlango wa kwanza kufungua jamaa uso kwa uso na mama mkwe, na alikuwa na kimwana ndani ya room, jamaa kutahamaki, mama mkwe...!!

Kama wewe ungefanyaje hapo ilhali siku chache za nyuma umekalishwa chini na huyu mama.??
 
Hii ni hatari kwelikweli! Unajua mama mkwe anaweza kumwek jamaa ndani kwa hasira kabla ya kufikiria namna ya kumwadhibu!
 
...hahahahahahaha...Kosa..1..kukutwa nyumba ya wageni wakati si mgeni..
Kosa...2..uzembe na uzururaji.(kumbuka ana kwake)
kosa...3..kutembea nje ya ndoa..
kosa...4..kumhatarishia mtoto wake..maambukizi ya v.v.u...
hakukosi kweli hapo...eti mkuu...then anachanganya na adhabu zake...
 
Najifanya simjui kabisa. walahatujawah onana najua hawezi kunitia ndani kwakuwa hatokuwa na uhakika na mm. pili hawezi kumwambia mwanae kama kanifuma gest. ila kiukweli baada ya hilo soo nitakuwa narudi home saa10 jioni maana hatwari
 
Najifanya chizi natoka speed,naenda hosp naongea vzr na doctor ananiandikia nina malaria ya kichwani.kesho nikikutana na mamamkwe najifanya sikumbuki.eehh ila nikipona hapo sirudii tena.
 
Unazimia, afu ukizinduka unajifanya uko kwenye coma huelewi kitu wala huongei.
 
hahahaha! Mamushka hiyo yako nimeipenda! Daaah, utabaki kwenye koma mpaka lini?..lol..
 
...hahahahahahaha...Kosa..1..kukutwa nyumba ya wageni wakati si mgeni.. Kosa...2..uzembe na uzururaji.(kumbuka ana kwake) kosa...3..kutembea nje ya ndoa.. kosa...4..kumhatarishia mtoto wake..maambukizi ya v.v.u...hakukosi kweli hapo...eti mkuu...then anachanganya na adhabu zake...
kosa 1 nomaa.,hahahaa
 
Kwa Tanga hilo si tatizo na haswa ukiwa dini fulani,na akiona ni tatizo kwa kawaida ya mama wa ki Tanga inabidi atafute jibu la kwanini hutosheki nyumbani mpaka unakwenda kula nje.
Shida case ya hivyo ukumbane nayo Iringa au Tabora!
 
Mama mkwe hakukwenda kufumania yupo kazini kukagua uraia; nitajitambulisha haraka kama kaka yake Arafat nimekuja leo kutoka kijiji kuna pacha wangu anaitwa Arafat yupo hapa ameowa binti anayeitwa Fatuma mama yake nasikia ni RPC hapa nimekuja kuwatembelea niliambiwa kuwa wana matatizo mke wake alimshtaki kwangu sasa nimeigia usiku huu nataka kesho niende kuwasuluhisha na nitarudi kijiji kesho mapema na huyu niliye naye hapa ni mke wangu tumekuja pamoja kwa ajili ya hayo matatizo ya mdogo wangu, maana pia mke wangu ni mtu mzuri sana katika Nasaa za ndo kwasababu ni Mlokole wa kwa Kakobe kule kijijini kwetu amekuja kwa ajili ya kuwaombe hawa wanaondoa, je mna maswali mengine kama hamna tunaomba tulale sisi tumechoka sana na usafiri wa shida na hili giza la Ngereza.
 
Umewahi kutunga novel we? Maana stori yako imeniacha mbavuless!! Ha! ha! ha! haaaa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom