Sijui nina ugonjwa gani..??

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,634
4,519
Kawaida nikiona mwanamke yuko singo wala hanishughulishi.Lakini nikiona au kusikia tu kuwa ana mtu wake basi mimi mapenzi hunishika kupita maelezo ,yaani hapa hata sijielewielwi sijui nimtongoze yupi ..??Najua kabisa Madame B yuko na mwanasheria ruttashobolwa beibe nasty yuko na Judgement,wake zake Asprin nao nawatamani na sijui nimtongoze yupi charminglady wala sikuwa na habari naye kipindi anamkataa hommie wangu wakati ndio sasa lakini toka atangaze uchumba na C6 basi roho inanienda mbio juu yake Arabela wala nilikuwa simfikirii,lakini toka nigundue kuwa yuko na zubedayo_mchuzi basi mimi hoi..ni nini hiki jamani wandugu..??
 
Last edited by a moderator:
Halafu kila siku huwa najiuliza Preta ana mtu wake au yuko singo...nashindwa kujua na sijielewi kama naye namtamani au nampenda,ila nikishajua nitadhihirisha..
 
Last edited by a moderator:
Kama una hamu ya kufia jela, jaribu kumtongoza mke wa mwanasheria.
Na hatutokutoa milele.


We nianze tu,halafu kila siku najiuliza na sikumbuki,au wewe ni yule niliyelala naye pale Himo wakati navizia kuvuka kwenda Tarakea kupeleka mahindi ya magendo...
 
HAPANA,
Yule ni Pacha wangu.


Ish ni hivyo kumbe au utakuwa ni yule aliyeniibia mtaji wangu Kahama wakati nilipoenda kununua dhahabu maana walikuwa wanafanana kweli..? Leo navunja ukimya mpaka nikujue wewe ni yupi..
 
Hee!!
Utaweza?
Mziki mnene huu,CD 990,
wa kuucheza ni Ruttashobolwa peke yake.



Wanawake mna shida kweli yaani ndio alivyokudanganya kuwa anaweza kuucheza yeye tu..??Lakini kabla sijaamua kuanza kukutongoza nataka kujua tulikutana wapi alkini..~?Au wewe ni yule wa Ilula nilipokwenda kukusanya nyanya ukaning`ang` ania turudi wote Dar
 
Back
Top Bottom