Sijui nimsaidiaje huyu dada

MATESLAA

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
1,246
74
Ndugu zangu naomba usauri wenu ,,, nini ni mwanafunzi wa chuo.nilikuwa na nchumba wangu wa kidato cha 6,,alikuwa akinidharau sana,matusi sana,na alikuwa hakiniwekea masharti wakati wa kula tunda,,sasa amemaliza kidato cha 6 na amepata 0 aninilazimisha turudiane wakati ni na chombo cha chuo nafanyeje wana jm
 
Achana naye,sasa hivi ameona hana mwelekeo ndo maana anakupenda,atakuchuna tu bure,mweke kapuni.
 
Ndugu zangu naomba usauri wenu ,,, nini ni mwanafunzi wa chuo.nilikuwa na nchumba wangu wa kidato cha 6,,alikuwa akinidharau sana,matusi sana,na alikuwa hakiniwekea masharti wakati wa kula tunda,,sasa amemaliza kidato cha 6 na amepata 0 aninilazimisha turudiane wakati ni na chombo cha chuo nafanyeje wana jm

Pole mdogo wangu, kwa 'yanayokusibu'

Ushauri ni kuwa we fuata moyo wako, na siyo wake, kwani ukiamua kuridhisha kila moyo unaelekea kwako, unaweza kuchizika...

Ushauri wa pili ni kuwa hicho ni kiwimbi kidogo sana kati ya 'mawimbi ya kawaida' ya mapenzi... Usijifanye bingwa wa mapenzi kwa kuyapa promo sana kichwani mwako, yatakuangamiza... Hakikisha kuwa huyapi zaidi ya 5% ya muda wako, na mwingine fanya mambo yako ya muhimu, hasa kusoma.

Ushauri wa tatu ni kuwa huyo ulikuwa nae akakuzingua, sasa una mwingine nae anaweza kukuzengue mbeleni n.k... Ili uheshimike kwa watu, na hasa kwa mwanamke wako, ni vyema ukawa na maisha mazuri. pamoja na umuhimu wa ki-sociology wa wewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi, lakini jua tu sasa level ya mapenzi uliyo nayo sasa ni sawa na mcheza football anayechezea Toto Africa... kwa nini usikomae kutafuta maisha mazuri, ili baadae ukawa na level ya akina Van Persie kwa mfano? (naamini wewe sio mshabiki wa Chelsea...lol)
 
angekuwa hajapata div 0, akakuomba mrudiane nayo usingemfikiria

kufeli kwake sio sababu ya kutosamehewa au kutopendwa
 
Kama bado unampenda, jaribu kumsamehe na urudiane nae. Binadamu tunaghafilika.
 
mrudie halafu akikutenda rudi tena humu jamvini tuje tukushauri upya, si unadai akili yako ni ya kuazima!
 
Mkuu si umesema tayari una chombo cha chuo? Sasa unaomba ushauri ili uwe nao wawili au ni vipi mi sijaelewa, huyo wa chuo humpendi uko nae kwa sababu ulitoswa na wa div 0 au?

Tulia na maamuzi yako kiongozi, huyo wa chuo ni dhahiri unaridhika nae (maana hujatuambia makosa yake) sasa kwa nini unajaza server ya ubongo wako kwa kurudisha makumbukumbu ya mtu aliekuwa anakutesa moyo wako?

Endelea na maisha yako mapya bwana, japo inaonesha bado una mapenzi na huyo mtalaka wako
 
njuka at work. ww unatembea na wanafunzi afu unadai alikuwa anakupa masharti kwani ulistahili kutembea nao?
kweli we bado njuka soma zingatia masomo naona hili jukwaa sasa hata watoto wanatoa mada zao
discuss haya mambo na roomate wako au wasela wenzio sio kumgwaga upupu hapa JF
 
mbona jibu unalo mwenyewe kijana, kwanini unataka kusumbua akili zetu?
 
Back
Top Bottom