Sijui kama unajua au hujui kuwa sensa imefeli

Simba Mkali

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
620
239
Sina hata haja ya kutoa maelezo mengi, leo Ijumaa ndiyo mwisho wa Sensa na kwa jinsi ambavyo nimeshuhudia zoezi lenyewe lilivyopelekwa pelekwa kwa vyovyote vile limefeli, tungoje idadi ya uongo ya uongo. lakini nadhani kuna fundisho tutakuwa tumelipata.

Viongozi wa serikali wanatakiwa kujenga mpango makini wa kudumu katika kufanikisha zoezi hilo kilahisi next time.
 
Sina hata haja ya kutoa maelezo mengi, leo Ijumaa ndiyo mwisho wa Sensa na kwa jinsi ambavyo nimeshuhudia zoezi lenyewe lilivyopelekwa pelekwa kwa vyovyote vile limefeli, tungoje idadi ya uongo ya uongo. lakini nadhani kuna fundisho tutakuwa tumelipata. Viongozi wa serikali wanatakiwa kujenga mpango makini wa kudumu katika kufanikisha zoezi hilo kilahisi next time.

Mapango makini si uuelezee au unabwabwaja tu. Kusema limefeli kabisa siyo sawa ila nijuavyo takwimu za idadi ya watu zitakazotolewa siyo sahihi kwa sababu:

1. Maandalizi yameingiliwa na ujanja ujanja na rushwa kwa watendaji wa zoezi ngazi za mkoa na wilaya
2. Watu wa sensa wamepita majumbani mwa watu saa za kazi na kusababisha taarifa za majumbani kutolewa na wasichana wa kazi including nyumbani kwangu.
 
Sensa hii aisee magumashi kibao, mtaani kwetu jamaa wamekuja j2 tu hawajatokea tena, nikachukua hatua za kwenda kwa Mjumbe nikareport ili nihasabiwe nikaambiwa nitapigiwa simu.

Office za serikali za mtaa nao wananiambia nisiwe na wasi nitulie nyumbani wanakuaja. Sasa sijui niende makao makuu wakanihesabu?
 
Mimi nimehesabiwa kwa simu maana walipofika nyumbani nilikuwa kazini wakapata namba yangu ya simu wakanipigia. Sijui kama huu utaratibu unaruhusiwa na hauwezi kuleta kasoro.
 
Sina hata haja ya kutoa maelezo mengi, leo Ijumaa ndiyo mwisho wa Sensa na kwa jinsi ambavyo nimeshuhudia zoezi lenyewe lilivyopelekwa pelekwa kwa vyovyote vile limefeli, tungoje idadi ya uongo ya uongo. lakini nadhani kuna fundisho tutakuwa tumelipata. Viongozi wa serikali wanatakiwa kujenga mpango makini wa kudumu katika kufanikisha zoezi hilo kilahisi next time.

mmmmhhhh na wasiwasi na uwepo wako hapa dunia leo ni alhamisi au ijumaa.. fafanua hilo ndio tukuelewe...
 
mmmmhhhh na wasiwasi na uwepo wako hapa dunia leo ni alhamisi au ijumaa.. fafanua hilo ndio tukuelewe...
Usiwe na wasiwasi, mkuu miye ni binaadamu naweza kuchanganya mambo, leo Alhamisi kesho Ijumaa. nashukuru kwa kunikumbusha.
 
Mapango makini si uuelezee au unabwabwaja tu. Kusema limefeli kabisa siyo sawa ila nijuavyo takwimu za idadi ya watu zitakazotolewa siyo sahihi kwa sababu:
1. Maandalizi yameingiliwa na ujanja ujanja na rushwa kwa watendaji wa zoezi ngazi za mkoa na wilaya
2. Watu wa sensa wamepita majumbani mwa watu saa za kazi na kusababisha taarifa za majumbani kutolewa na wasichana wa kazi including nyumbani kwangu.
Unajua maana yakubwabwaja? kama wewe ni mgeni, wana JF tumeongea mengi sana kuhusu serikali ilichotakiwa kufanya, pia kila sehemu wenye akili wametoa ushauri wa maana. sikuona sababu ya kurdia hapa. asante kwa kunielewa.
 
Mi ni kama sikuhesabiwa tu, mtu mwenyewe aliyekuwa akituhesabu licha ya kutokuwa na kitambulisho,yunifom pia taarifa zetu alikuwa akizirekodi kwenye kinotbuku kama fundi mwashi akihesabu idadi ya mbao toka kwenye fuso
 
SENSA MWISHO JUMAMOSI... Mnakuwa kama huwa Hamsikilizi TV na Radio.. Sensa ni Siku 7, acheni kukurupuka

Karani amepangiwa Eneo lenye kaya Zaidi ya 150 halafu mabalozi hawatoi Ushirikiano unadhani atazimaliza kwa siku mbili au Tatu?? Kaya zenyewe zina watu zaidi ya Nane na Anatakiwa kuuliza Maswali 37 au 62 Atamaliza Leo.

Vumilieni Wanakuja si kuja kulalamika JF wakati mda hata wa Sensa kuisha hamuujui

UKIONA UNA KAZI SANA MWACHIE HAYA MFANYAKAZI AU MTU MZIMA HAPO HOME

* Majina ya Wanakaya waliolala jumamosi kuamkia jumapili mkiwamo na Nyie

*Uhusiano na wanakaya hao[mke,mme,ndugu,rafiki au watoto]

* Umri wa wanakaya
*Viwango vya Elimu

*Kama wana-vyeti vya kuzaliwa au Lah

*Idadi ya Mifugo[kuku,ng'ombe,Kondoo na mbuzi]

*Kama wewe na wanakaya wengine ni Wanachama wa Mifugo ya Jamii au Lah

*Kama kuna Mlemavu yoyote[wa kuöna,kusikia,albino,kutembea]
 
jamani siku saba za sensa zinaisha tarehe 2 kwahiyo tujipe moyo tutahesabiwa manake mim na familia yangu hatujahesabiwa nikahisi labda kwakua kwang ni mbal sana na majirani nikaenda kwa mjumbe wa nyumba kumi akasema watakuja tu nisubiri hivyo naendelea kusubiri.
 
Back
Top Bottom