Sijamwelewa wife jamani. ..

Calnde unapaswa kuwa makini sana na maneno unayoongeaa hakuna mama anaefurahia kusikia mtoto wake kuitwa majina ya ajabu,sioni sababu ya kwenda kupima DNA eti kwa sbbu ya reactin ya wife mtoto ni wako kwa hiyo we tafuta means za kumaliza hilo tatizo.
 
Ushawahi kuingia delivery room/leba ukajionea watoto wanavyokuja duniani? Kama umewahi basi nitakushangaa lakini kama hujawahi hebu jaribu kuingia mtakapo-plan kuleta mtoto mwingine,then utapata majibu ya maswali yako yoooote.
Nadhani mkeo akikumbuka maumivu aliyoyapata leba room wakati akimleta mtoto wenu duniani akiunganisha na kauli yako ya kutiliashaka uhalali wa mtoto kwako wakati akijua wewe ndiye uliyepandikiza mbegu, INAUMA SAANA. Wewe zidi kumwomba msamaha mkeo na usirudie tena kauli uliyoitoa.
 
mkuu wakati tunaoana ye alikuwa amemaliza Masters na alikuwa amekusanya senti na kujenga bonge la hausi Njiro Arusha.. . .
Mie nilikuwa na nyumba maeneo ya kijitonyama lakini haikuwa kubwa kama yake. Tukakubaliana kuiuza ili tununue usafiri pamoja na miradi flani ya maendeleo. Mie kwa sasa sina nyumba, ila nilinunua kiwanja Moshono Arusha pamoja na Kingine Kidogo maeneo ya Wazo. .

Tunaishi kwenye nyumba ya wife, japo hajawahi kuninyanyasa wala kuringa. Ananipenda, tunapendana, tunaaminiana, ila hili la juzi limebadilisha kabisa mtizamo wangu kwake!
kaka we umeliwa kuanzia sasa chokochoko zote kwa mkeo uache kama bado unapenda muishi pamoja,yaani huyo kweli master yake kaitumia vizuri,kitendo cha wewe kukubaliana nae kuuza nyumba ukae kwake pole sana bro inabidi uwe mpole hata kama kakauchezea faulo maana mi yashanikuta kama yako nae alikua binti wa hukohuko arusha,nakumbuka mwishomwisho wa mapenzi mama alinifukuza kama mbwa nyumbani na nguo zilitupwa nje uwanjani na majirani wanaona,nnachoshukuru mtoto sina shaka nae kabsaaa maana nilipiga kopi ya nguvu,sema baaada ya kuzaa mama alikuja na revolution ndio tukaachana,sasa ushauri wangu huyo kashakuzidi ujanja,ukianza kuingiza mambo ya kupima d.n.a na nini umekwisha mama atajua tuu,mtoto tayari mkubwa huyo hata ufanyeje atamwambia,na gia zao ndo hizo kwanza lazima unyimwe unyumba ili uzidi kukasirika na yeye akuwashie moto na ikiwezekana kukutimua kabisa,inawezekana upole wake ni imani tu alikua anakuwekea sababu hujawahi leta ukorofi sasa ukilianzisha hilo kashapata sababu,yaani nakuonea huruma kitanzi kinakunyemelea,mi nilipata uchizi kabisa mpaka nikaombewa na kufanyiwa counselling ya nguvu ndo nikapiga moyo konde na mungu amenisaidia mpaka hapa nilipo.
 
Ni jioni, tumepumzika, na mpenzi wangu, mke wangu,katoto ketu ka miaka nane katundu kweli. Basi kanaleta utundu wake, nakafokea, kanazidi, nikakasirika na kukaambia 'we mbona mtudu hivyo, utadhani sio mwanangu?'

duuh, nikawa nimeharibu, wacha mama yake awake, unadhani wa nani. huniamini ee? akaendeleza maneno kibao ya malalamiko, toka juzi amekasirika. Nimemwomba samahani, kakubali, lakini bado kakasirika kwa msemo wangu.

wadau napata mashaka,simwelewi, mbona kakasirika?
kapime dna mapema mkuu
 
unajua mtoto anapokuwa mtundu ni kazi sana kumlea na kama hiyo haitoshi watu mbali mbali wanaoshuhudia huo utundu huwa wanatoa comments ambazo sio nzuri tena mbele ya mtoto, hizi zinaweza kuumiza roho ya mama yake tena sana akajiona kama failure ktk malezi nk lakini kwa mwanamke mpole asiyependa ugomvi kama unavyomuelezea mkeo hapa sio rahisi akajibu mashambulizi, huwa mahasira yote anayaweka rohoni tuu

sasa comment kama ya kwako tena mbele ya mtoto inaweza ikaamsha mahasira yoote na kwa vile wewe mumewe ni mtu ambaye anaweza kugombana nae basi yoote anakumwagia tuu atoe duku duku lake...lakini sio kwa kukusudia bali hutokea tu involuntary
 
Kaka kama haujui kusoma basi natumaini hata picha unaona, mchukue mtoto bila kumwambia mkeo kampime DNA, nakuhakikishia huyo si mwanao na kama akiwa wako basi kuna mwenzio alikusaidia kuweka ubongo na utundu!
 
Inawezekana mtoto ni wako kabisa. Genetically, unaweza kuwa ulikuwa na genes za utundu lakini phenotically (physically) za upole zikawa zimejionyesha zaidi, ukadhani wewe ni mpole sana. Mtoto kuwa mtundu si haja. Angalia je sura yako ipo. Kinachokupa wasiwasi ni jinsi mama alivyokujibu labda kwa muda huu ni expectant na amekuibia akijua wewe zuzu. lakini ukisisitiza ukapime DNA lakini fanya maamuzi kabla ya results za DNA kwambe zikitoka negative what is the way forward, usije ukajikuta unadeepen crisis na ikakuathiri sana kisaikolojia. Hata kama amezaliwa na mwingine unaweza ukandelea kumwdopt pia.
 
Kwa kauli yako hiyo uliyoitoa kwa mke yeyote yule lazima angekasirika hata kama mtoto ni wa kwako.Nakushauri endelea kuamini ya kwamba mtoto ni wa kwako ili kudumisha na kuimalisha hiyo ndoa yenu.Otherwise kama kuna previous cases zinazo kufanya usimwamini mwenzako hapo unaweza kufikiria mambo ya DNA.Lakini kwa jinsi ulivyo present issue yako kwa uzoefu wangu naamini hako katoto katundu kama ulivyo kaita ni damu yako na wewe ndiyo ulichafua hali ya hewa!hayo ni mawazo yangu tu mkubwa.
 
Hahahahaha duh ukiona n'tu anajihami basi ujue kuna kitu around basi wewe chunguza n'jomba utabaini ukweli kachukue kapime DNA utabaini pengine kweli sio wako.

bravoooo,
Na ukikuta siyo wako, muulize, alaah!!
 
Kaka kama haujui kusoma basi natumaini hata picha unaona, mchukue mtoto bila kumwambia mkeo kampime DNA, nakuhakikishia huyo si mwanao na kama akiwa wako basi kuna mwenzio alikusaidia kuweka ubongo na utundu!

Kwi,kwi ,kwiii hiiihii hiii hiiiiiiiii.
Labda karithi toka kwa babu yako yule kwa mjombake na bibi,...
 
Basi ujue katika familia yenu kuna series ya visa vya ajabuajabu unavyomfanyia huyu mama ,kiasi kwamba ameona huo ni mwendelezo tu wa kashfa zako!

Lakini katika hali ya kawaida mwanamke hawezi kukasirika kwa maneno rahisi tu kama hayo!

Rudi nyuma angalia mienendo yenu ya maisha ya kila siku utaona mahala pabovu!
 
pole sana kaka ..hao ndio mama zetu...tunatakiwa tuishi nao kwa ungalifu na maarifa makubwa....jipange mkuu kabla ya ku-take next move...hata kama unataka kuelewa uhalali wako kama biological father wa mtoto its ok...ila ujue nini kitafuata baada ya majibu either yako safi i.e. ni mtoto wako au sio safi. BABA KUPIMA DNA KAMA KUPIMA NGOMA TUU...MAJIBU LAZMA UWE UMEJIAANDA KUYAPOKEA....

Swali kwa wadau ...kwani dna inahitaji kumpeleka mtoto?...au hata unywele wa mtoto unatosha kabisha kutoa majibu ya dna...pia kuna sheria hapa kwetu zinazuia matumizi ya kipimo hicho bila kuwa na recommendations from either ni mahakama au police...ingekuwa ni rahisi kivile nadhani kila mzazi angepima dna za watoto wake....NI MAONI TU WADAU
 
Sasa utani tu watu ndo mnachukulia big deal basi mnakuwa na sababu zenu around
 
Ni jioni, tumepumzika, na mpenzi wangu, mke wangu,katoto ketu ka miaka nane katundu kweli. Basi kanaleta utundu wake, nakafokea, kanazidi, nikakasirika na kukaambia 'we mbona mtudu hivyo, utadhani sio mwanangu?'

duuh, nikawa nimeharibu, wacha mama yake awake, unadhani wa nani. huniamini ee? akaendeleza maneno kibao ya malalamiko, toka juzi amekasirika. Nimemwomba samahani, kakubali, lakini bado kakasirika kwa msemo wangu.

wadau napata mashaka,simwelewi, mbona kakasirika?

ningekushauri uangalie ulipo na unapoelekea, sahau yaliopita na think positive, masuali muhimu ya kujiuliza kwa sasa ,ni je:-

a) ndoa ina mapenzi ?
b)mke wako anakujali?

kama majibu ni yes ,basi achana na kwenda kupima dna ,kwani unavyoonekana unampenda mke wako na jibu la dna linaweza likaja likakuchanganya akili kama utalikuta tofauti na ulivyotarajia.


My take: mke wako anakupenda sana hivyo hio kauli ilimvunja moyo kiasi fulani na akakasirika ili kuwakilisha hisia zake kwako. (hakuna chochote zaidi)

unlikely alternative: hata kama mtoto sio wako, madhali kwa sasa umekiri kwamba ana mapenzi na wewe ,hivyo hata kama alikosea ina maana ametubu na nadhani anastahiki kusamehewa kwani binadamu sote ni wenye kukosa.

ushauri: rejesha mapenzi kwa mke wako na usiruhusu dhana mbaya zikatawala akili yako.

ni ushauri wangu tu kama haufai,weka kwenye taka.

Quiet.
 
mkuu kweli nukigundua nieendelee, hapo sitaweza, atakufa mtu ati! Fikiria mtoto yupo darasa la pili, namlipia pesa nyingi mpaka nachanganyikiwa, alafu nieendelee nae! itakuwa kazi nzito. . .
Mungu saidia tuu awe wangu

Mkuu,

Haina maana ya kujiuliza swali hili. Labda uanze kwa kujiuliza mwenyewe, je wewe ni mtoto wa huyo unayemwita baba? Sorry, sounds stupid but at the end ukweli ni kwamba utaleta matatizo zaidi kwa kujaribu kumpima huyo mtoto kuliko solution. Kitu muhimu ni kwamba mtoto kazaliwa nyumbani kwako, na ukiamini kabisa kwamba ni wako...hilo ndilo muhimu. Ukimpima, ukakuta siyo wako utafanya nini? Unaweza kumpiga mkeo hadi akafa, lakini bado ukweli uko palepale, sio wako! Unaweza ukamwacha mke huku unampenda: bado ukweli ni ule ule "somebody fuckked ur wife". Unaweza ukamuua yule mtoto, then what? si utaishia jela tu! Hata mitume walilea watoto wasio wa kwa, sembuse wewe? Kama kanafanana fanana we kavumilie tu maana mtoto ni mtoto tu, ili mradi ni mwafrika mwenzio.
Halafu, suppose unapima , halafu daktari anakwambia huna uwezo wa kumpa mwanamke mimba utafanyaje? Why create all this fuss for a damn proof? We mradi unaweza kuejaculate , hilo ndo muhimu....stop asking, take care of your loving wife ( afterall amekuletea katoto proud is on you, not her) !
 
Mie sijawahi kabisa kuwaza mambo yakupima. Na ni lazima nikiri nampenda na kumwamini sana! Hilo la kufanana tena unaniongezea shaka, maana toka amezaliwa kila mtu anasema amefanana na mama yake. Hata siku moja sijawahi kumsikia mtuu akisema amefanana na baba yake. . .

Kaka hii sasa ni nini?
Kwani lazima mtoto afanane na baba? Biology inasema kuna pheno type na geno type. Mtoto anaweza akafanana na wewe lakini akili ya upande wa mama. Nina kaka yangu amefyatua photocpy ya watoto wake, lakini wote ni vichwa vizito darasani wakati yeye yuko bright! Ukifuatilia, kwa mkewe aliyesoma zaid amefika std 7, tena ya kuburuzwa! Hivyo kama hufanani naye sura,checki akili na matendo yake. Ukikosa cha kufananisha hapo, sasa ndo uanze kuwa na wasiwas.
SORRY : umesema mkeo mtu wa Arusha? Mie sio mkabila, ila kama ni MMERU watch out, the game is over! utatupiwa kila kitu nje na ndugu zake......mimi nakaa Njiro baba, kama wewe ni jamii ya Masanilo (alcoholic) niambie kijiwe chako nikutafute kwa ushauri zaidi!!
 
Ushawahi kuingia delivery room/leba ukajionea watoto wanavyokuja duniani? Kama umewahi basi nitakushangaa lakini kama hujawahi hebu jaribu kuingia mtakapo-plan kuleta mtoto mwingine,then utapata majibu ya maswali yako yoooote.
Mungu alimwambia Adam "kwa jasho lako utakula" na akamwambia Hawa 'kwa uchungu utazaa".
 
mkuu kweli nukigundua nieendelee, hapo sitaweza, atakufa mtu ati! Fikiria mtoto yupo darasa la pili, namlipia pesa nyingi mpaka nachanganyikiwa, alafu nieendelee nae! itakuwa kazi nzito. . .
Mungu saidia tuu awe wangu
Mkuu mtoto darasa la pili na hakuna mdogo wake,mmmhhh kulikoni Mkuu? ni utashi au matatizo,maana..........
 
Hebu niambieni wanapimia wapi na vitu gani vinahitajika ili nipate najibu mazuri, ila akijua atantimua home aisee! Mungu wangu . . . .
Calnde una uhakika mkeo haingii JF,maana akiiona hii thread kisha akaunganisha moja na moja patachimbika mzee!
 
Calnde una uhakika mkeo haingii JF,maana akiiona hii thread kisha akaunganisha moja na moja patachimbika mzee!

Sina hakika mkuu ingawa sio mpenzi wa Internet hata emails zake nyingi huwa namsaidia japo nimewahi kungusia juu ya hii site. Anyway tumezungumza nae na akaniambia hamna lolote ni hasira tuu zilimpata za kuona kwamba simwamini wakati yeye kwa miaka yato ameniamini na kuwa mwaminifu japo wakubwa wamekuwa wakimtaka kwa gharama kubwa. Hata hivyo mtoto nimezidi kumchunguza na mashaka yameongezeka japo nimemwonyesha wife i don care. Ntaenda kupima kwa siri tuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom