Sijahesabiwa Bado na Deadline Inakaribia

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
hivi kwa nini huyu JK ni failure kwa kila kitu? hivi inakuwaje mimi mpaka dakika hii sijahesabiwa? au Chadema hatuhesabiwi?
 
hivi kwa nini huyu jk ni failure kwa kila kitu? Hivi inakuwaje mimi mpaka dakika hii sijahesabiwa? Au chadema hatuhesabiwi?
na tahimin imeshatolewaa tayari!tumefanikiwa kwa 80% hivyo ambao bado hautwahitajii sana,maana makadilio yetu ilikuwa ni 60%.tumevuka lengo!!!!
 
Mimi sina chama lakini sijahesabiwa. Jana walipita kwa jirani yangu walipomalizana nae wakamuuliza vipi huyu jirani yako yupo?

jirani akawajibu yupo. baadae wakaanza kuulizana vipi tumuhesabu na huyo? mmoja wao akasema ahhh tumechoka bwana, na akaongezea, mtaa huu waliobaki tuwaache kesho twende mtaa mwingine siku zinaisha.

Kwa hiyo mimi na familia yangu hatutahesabiwa. kwa hiyo ni wengi tu ambao hawatahesabiwa na kwa ujumla takwimu zitakazopatikana hazitakuwa sahihi.
 
Pole sana, but we are in the same boat. Mimi na familia yangu pia hatujahesabiwa. Jana nilienda kwa mwenyekiti wa mtaa kutoa taarifa sikumkuta ila niliacha ujumbe but mpaka ninaondoka nyumbani leo saa mbili asubuhi hakuna aliyekuja.

Kinachonishangaza ni kuwa baadhi ya majirani wamehesabiwa, sielewi kama sensa ya mwaka huu italeta real picture ya idadi ya watanzania ukizingatia kuna maeneo tunasikia makarani waliishiwa vitendea kazi toka jumamatatu tarehe 27/08/12
 
Kama hujahesabiwa nenda ofisi za serikali ya mtaa utahesabiwa huko na huo ndiyo utaratibu uliotolewa kwa wale ambao hawatafikiwa.
 
Mimi nimehesabiwa nasubiri hayo maendeleo wanayoyasema kwenye kauli mbiu zao eti sensa kwa maendeleo ya taifa
 
Kama hujahesabiwa nenda ofisi za serikali ya mtaa utahesabiwa huko na huo ndiyo utaratibu uliotolewa kwa wale ambao hawatafikiwa.

TULIAMBIWA TUWASUBIRI WATAKUJA NA MJUMBE NA WATAKUWA NA VITAMBULISHO
SASA SISI TUKAFANYE NN SERIKALI ZA MITAA??? DOUBLE STANDARDS
BADO NAWASUBIRI :rant:
 
Kama hujahesabiwa nenda ofisi za serikali ya mtaa utahesabiwa huko na huo ndiyo utaratibu uliotolewa kwa wale ambao hawatafikiwa.


Hapo kwenye red - yaani utaratibu rasmi ni kufuatwa kwenye KAYA yako na kuhesabiwa or tuseme mahali ulipolala tarehe 25 usku kuamkia 26.

Watu wamepewa mafunzo juu ya kuhesabu watu, wamelipwa, wamepewa vitambulisho ...........halafu washindwe kufanya zoezi kamili.

MIMI NITOKE KWANGU - KWA JASHO LANGU..............KWA MGUU AU USAFIRI WANGU.............. KWA MUDA WANGU......HADI SERIKALI ZA MITAA ............NIMTAFUTE MWENYEKITI NA KAMA KATOKA NIMSUBIRI ILI TU

NIHESABIWE!!!!!!!!!!!!!!!!!!! VERY FUNNY INDEED ............... ??????????????????????????? :eek2::eek2:
 
mi najiuliza yule mama mkurugenzi wa sensa zile asilimia za mafanikio ya sensa sijui zaidi ya 90 kazitoa wapi? Kaazi kweli kweli.
 
Acheni kulalamika kama wale majamaa, chukueni hatua. Imekwishatolewa tamko kwamba kama hujahesabiwa nenda kwa mwenyekiti wako wa serikali ya mtaa. Sasa ninyi mmechukua hatua gani kabla hamjaja humu JF?
 
Mie bado nawasubiri kwangu wasipokuja basi siwezi kupoteza muda kumtafuta huyo cjui ndio mkiti kwani hawa makarani wa sensa wanalipwa posho kubwa tu.

Jirani yangu wameshapita!!!!!ajabu
 
Acheni kulalamika kama wale majamaa, chukueni hatua. Imekwishatolewa tamko kwamba kama hujahesabiwa nenda kwa mwenyekiti wako wa serikali ya mtaa. Sasa ninyi mmechukua hatua gani kabla hamjaja humu JF?

mkuu sio sahihi kabisa kwasababu kama ni hivyo basi kusingekuwa na haja ya kutumia mapesa yote yale ya kuwalipa makarani na isitoshe nilishapoteza muda kuwasubiri, bado niendelee kupoteza muda tena kuwatafuta? Liwalo na Liwe!
 
Acheni kulalamika kama wale majamaa, chukueni hatua. Imekwishatolewa tamko kwamba kama hujahesabiwa nenda kwa mwenyekiti wako wa serikali ya mtaa. Sasa ninyi mmechukua hatua gani kabla hamjaja humu JF?
Sielewi mtazamo wako ni upi hasa sambamba na haki yako ya msingi: kuna mantiki gani makarani kulipwa pesa za walipa kodi kwa ajiri ya kupita nyumba kwa nyumba kuhesabu watu alafu kwangu wasipite tena kwa makusudi kama si uzembe alafu leo uniambie niende kwa M/kiti wa serikali za mitaa kupanga foleni!!!!!.

Ambao hatujaesabiwa ni wengi mno, mi naishi kwenye apartment yenye jumla ya familia 12 cha ajabu hakuna hata mmoja aliyehesabiwa.

Katika pitapita zangu nilikutana na makarani wa sensa mitaani nikawaomba wanihesabu wakagoma wakadai kuhesabiwa kwangu ni mpaka niwe mtaani kwangu ninakoishi, nilishindwa kuwaelewa kwani mi nilifikiri kila mtu anahesabiwa popote pale anapokua amepatikana kwa muda muhafaka kumbe siyo na wao wana maana nyingine.

Mimi niko Dar es salaam sikuhesabiwa japo nilitamani Je yule wa Namtumbo, Vyadigwa, Lupembe na Butakya?????.
 
Back
Top Bottom