Siita alaaniwe na genge la mafisadi wa ccm wanaojumu rasimu ya tume ya katiba

Apr 29, 2013
31
12
CCM KUHUJUMU KURA ZA HAPANA KATIKA BMK WAALANIWE NA WATZ WOTE NA WATETEZI WA HAKI KWA DHAMBI HIYO YA KIHISTORIA.

Watz wenzangu, kura ya siri huwa ni siri, na kura hupigwa mara moja tu kupata maamuzi yanayotakiwa.

kura ya siri kamwe haitowi nafasi ya kujua nani amepiga kura ya mlengo flani wa ushindani.

Kura halali huwa haipaswi kuwekewa msukumo wowote dhidi ya mpiga kura unaomrubini mpiga kura wakati anapiga kura.

Ikiwa hivyo, kura hiyo ni batilu, na haina uhalali kwenye maamuzi maamuzi yanayotakiwa kufanyka.

MAAJABU YA SIITA NA CCM KATIKA MBK

Mwenyekiti wa BMK na ccm wenzake wamekiuka miiko ya upigaji kura, na kuhalarisha dhuruma ya dhidi ya wapiga kura wa BMK waliopiga kura ya "Hapana" na wale wsliopiga kura ya siri kwa kile alichokiita kufanya maridhiano nao ili wabadirishe msimamo wao ili wakubali kupiga kura ya ndiyo kupitisha Rasimu ya bunge lililotekwa na makada wa ccm.

kufanya hivyo kunakiuka uhuru wa mpiga kura, uamuzi sahihi wa mpiga kura, na uhalali wa kura itakayopigwa awamu ya pili.

Swali kwa samweli Siita kiongozi wa Mafisadi wa ccm ndani ya Bunge maalumu la Katiba!!

1. Siita atafahamu ni nani kapiga kura ya "hapana" au "ndiyo"?? maana zilipigwa kwa siri.

2. mfumo wa upigaji kura haukueleza toka mwanzo na hikuwekwa bayana kuwa kura za "hapana" tu ndizo zitaundiwa kamati ya maridhiano na siyo kura za "ndiyo"

je, siita ametoa wapi legal na moral responsibility kuunda kamati ya maridhiano ambayo from the beggining haitawahi kutajwa wala haitambuliki ktk sheria ya mabadiliko ya Katiba??

Huu ni wizi, first order ya ufisadi wa haki za Watz ambao haujawahi kufanyika kote duniani bali WaTz ndio wanaushuhudia kupitia ccm na kiongozi wao wa ufisadi ktk Bunge Maalumu la Katiba.

Niwaombe Watz wenzangu suala hili tulipikemee kuanzia vinywa vyetu, mtaani, makanisani, msikitini, na kwingineko kunakofaa kuwafikishia ujumbe Watz wakatae ushetani unaofanyika ndani ya Bunge la Katiba lililohujumiwa na ccm wakaamuwa kunyonga Rasimu bora ya Warioba na kuichakachua na kuondoa misingi bora ya sheria mama (Katiba) na kuweka sheria inayopetipeti ufisadi wa ccm na washirika wao.

Watz tulaani kwa nguvu zote kitendo/wizi/ukandamizaji wa Watz unaofanywa na Bunge la ccm kurazimisha kuwanyima Watz haki yao ya katiba bora.

Tusikubali kwa sauti moja Bunge la Ccm wanachokifanya kuturudisha nyuma kwenye karaha ya katiba mbovu kupita zote duniani.

Ujumbe huu uwafikie Watz popote walipo ili wizi wa ccm na washirika wao ushindwe mpaka hapo Watz tutakapojipanga kupitia Ukawa kupata katiba Bora.

UKAWA Tumaini Letu!!!
 
Pasco kawaambieni toka jana kuwa mpira dk90 sijui kama mlimuelewa alichokimaanisha!!! Tatizo watu wengi mnatanguliza mihemko kama kuku aliyeona pumba. Kama ni kujipanga basi ccm wanajua kujipanga na kutumia njia zote iwe halali, haramu, umafia na uchawi mradi wapate wanachokitaka.

Msiwe mnakimbilia kushangilia kabla mpira haujaisha.
 
Tusifananishe mambo muhimu kwa Taifa na mpira bhanaa!! Watu wameshatishiwa maisha yao na taarifa za habari zimetangaza hivyo. Haihitaji masaa chungu nzima kuhesabu kura 600!

Pasco kawaambieni toka jana kuwa mpira dk90 sijui kama mlimuelewa alichokimaanisha!!! Tatizo watu wengi mnatanguliza mihemko kama kuku aliyeona pumba. Kama ni kujipanga basi ccm wanajua kujipanga na kutumia njia zote iwe halali, haramu, umafia na uchawi mradi wapate wanachokitaka.

Msiwe mnakimbilia kushangilia kabla mpira haujaisha.
 
Back
Top Bottom