Siipendi tabia hii

Rosweeter

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
1,171
4,432
Tabia ya wasichana kuomba omba vocha

"Honey, simu yangu haina credit,
naomba uniongezee..........."

Ningekuwa kidume ningewajibu "Pambaf....... kamuombe baba yako"

Wewe ni tabia gani inakukerai?
 
Tabia ya wasichana kuomba omba vocha

"Honey, simu yangu haina credit,
naomba uniongezee..........."

Ningekuwa kidume ningewajibu "Pambaf....... kamuombe baba yako"

Wewe ni tabia gani inakukerai?

kutoka kwa wanawake au wanaume?
 
Tabia ya mistrust... kila saa maswali ya uko wapi? uko na nani? unafanya nini?.... kwangu siipendi
 
Mi napenda toa na nina moyo wa kusaidia. Asiponiomba vocha naona kama nalack kitu fulani hivi.
 
Mi sipendi tabia ya mtu kila mara "naomba simu yako nimpigie mtu fulani nina shida naye" kila mara? wakati naye ana simu. afadhali aniombe hela akanunue vocha. Vilevile sipendi mtu anibip kwa shida yake mwenyewe!!!
 
Mi sipendi tabia ya mtu kila mara "naomba simu yako nimpigie mtu fulani nina shida naye" kila mara? wakati naye ana simu. afadhali aniombe hela akanunue vocha. Vilevile sipendi mtu anibip halafu ukimpigia kumbe yeye ndiye mwenye shida!!
 
Tabia ya mistrust... kila saa maswali ya uko wapi? uko na nani? unafanya nini?.... kwangu siipendi

Haswaa kwa wanaume, ukimwambia niko kwa shoga yangu anakwambia nipe niongee nae, ukimwambia niko nyumbani peke yangu anakwambia washa tv, zima washa tena, weka tbc, haya hamishia clouds........ mambo gani haya
 
Mi sipendi tabia ya mtu kila mara "naomba simu yako nimpigie mtu fulani nina shida naye" kila mara? wakati naye ana simu. afadhali aniombe hela akanunue vocha. Vilevile sipendi mtu anibip kwa shida yake mwenyewe!!!

Tena bora hata awe na shida, lakini anakubeep alafu analeta hadithi zisizo za maana mwisho anakwambia "ok bro nilitaka kukusalimia tu"
 
Mi napenda toa na nina moyo wa kusaidia. Asiponiomba vocha naona kama nalack kitu fulani hivi.

Kama ni kweli una moyo wa kutoa usingengoja akuombe, ina maana ungetii kiu yako ya kutoa na yeye asingepata nafasi ya kukwambia naomba, sema unapenda kuchunwa
 
Mbona mimi haniombi namtumia tu ninapojisikia, ila ikiisha na uliza aliongea nani.nukta
 
tabia ya baadhi ya wasichana na wanawake kutoka na waume za watu

Vipi juu ya wanaume wanaotoka na wake za watu, tena ukizingatia takwimu zinatuambia wanawake ni wengi kuliko wanaume, imekaa vipi hiyo...?
 
Haswaa kwa wanaume, ukimwambia niko kwa shoga yangu anakwambia nipe niongee nae, ukimwambia niko nyumbani peke yangu anakwambia washa tv, zima washa tena, weka tbc, haya hamishia clouds........ mambo gani haya

hata baadhi ya wadada wanayo sana... na sipendi wanaovuta sigara kwenye public areas kama kwenye mikusanyiko ya watu wengi ama kwenye daladala ilhali kwa wengine ni keeeeeero!!
 
Back
Top Bottom