Sifa za wagombea moro press club

Inkognito

Member
Feb 13, 2011
86
108
Ndugu wanajamii, napenda kuwabandikia sifa za wagombea nafasi mbalimbali ndani ya Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Morogoro kama ifuatavyo:

NAFASI YA UENYEKITI
1. AZIZI MSUYA

SIFA ZAKE:
  • Ni mwajiliwa wa Bussiness Times Limited
  • Anaweza Kuhama muda wowote kwenda mkoa mwingine iwapo atahamishwa na mwajiriwa wake
  • Ushiriki wake kwenye mambo ya habari ni mdogo,ni mpokeaji tu wa taarifa
  • Si mtu wa kujichanganya na wadau tofauti tofauti
  • Hajawahi kushika nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama cha waandishi wa Habari Morogoro
  • Hakubaliki miongoni mwa waandishi walio wengi
2. IDDA MUSHI
SIFA ZAKE

  • Ni mwakilishi wa IPP Media (Mwandishi wa ITV na Radio One)
  • Ni Makamu Mwenyekiti anayemaliza muda wake
  • Ni mshiriki mzuri katika mambo ya habari
  • Ni mtu wa kujichanganya na wadau mbalimbali
  • Ni mtendaji mzuri,ana sifa nzuri ya kuongoza,amekuwa akikaimu nafasi ya uenyekiti tangu mwezi November 2010 mpaka sasa baada ya mwenyekiti wake kuugua kwa muda mrefu
  • Ni mwanachama wa muda mrefu wa chama cha waandishi wa Habari Morogoro
  • Ni mfuatiliaji mzuri wa kanuni,taratibu,sheria na maadili ya tasnia ya uandishi wa habari
  • Amewahi kukumbana na Changamoto kadhaa katika kazi yake ikiwemo kushtakiwa na mafisadi na kuwashinda mahakamani
  • Anakubalika na wadau wengi hasa waandishi wa habari na utangazaji

MAKAMU MWENYEKITI

1. DEVOTA MINJA
SIFA ZAKE
  • Ni mwanachama wa muda mrefu wa chama cha Waandishi wa habari
  • Ni mzoefu wa mambo ya habari
  • Anafuata na kuzingatia kanuni,taratibu na sheria za taaluma yake ya uandishi wa habari
  • Ni mtu wa kujichanganya na wadau mbalimbali
  • Anakubalika miongoni mwa waandishi wa habari
2. RAMADHANI LIBENANGA
SIFA ZAKE
  • Ni mwajiliwa wa Majira
  • Ni mlopokaji, Si mtunzaji wa siri
  • Hana msimamo katika maamuzi
  • Si mtendaji wa kazi
  • Anajali zaidi pesa kuliko kazi
  • Ni mwanachama wa muda mrefu wa chama cha waandishi wa habari
  • Ni mzoefu wa mambo ya habari
  • Ni swahiba wa karibu wa Aziz Abood (Mbunge wa ccm-moro mjini) na matajiri wengine wa Morogoro
  • Ni mtu wa propagamda na vurugaji wa mambo
NAFASI YA UKATIBU
1.ABEDI DOGOLI
SIFA ZAKE
  • Ni mwajiliwa wa siku nyingi wa Abood Media Group
  • Anatumiwa na Aziz Abood kwa ajili ya kulinda maslahi ya Aziz Abood
  • Anafanya kampeni za Rushwa
  • Ni mtu wa kudhoofisha kanuni,taratibu na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari
  • Amewahi kuwa meneja wa kampeni wa Aziz Abood japo kwa siri
  • Si mtu wa kujichanganya na wadau mbalimbali
  • Alisimamia zoezi la kununua magazeti yote yaliyoandika kuhusu kifo cha mwandishi wa habari marehemu KUANDIKA aliyefariki baada ya kupata ajali akiwa ndani ya basi la Abbod
  • Hakubaliki miongoni mwa waandishi wa habari
  • Ana tuhuma za kupewa shilingi milioni mbili kutoka kwa Aziz Abood ili ahakikishe anashinda nafasi ya Ukatibu
2. JOSEPH MALEMBEKA
SIFA ZAKE

  • Ni mwakilishi wa Vyombo mbalimbali vya habari
  • Ni mshiriki mzuri katika mambo ya habari
  • Ni mtu wa kujichanganya na wadau mbalimbali
  • Ni mtendaji mzuri,
  • Ni mwanachama wa muda mrefu wa chama cha waandishi wa Habari Morogoro
  • Ni mfuatiliaji mzuri wa kanuni,taratibu,sheria na maadili ya tasnia ya uandishi wa habari
  • Amewahi kukumbana na Changamoto kadhaa katika kazi yake
  • Anakubalika na wadau wengi hasa waandishi wa habari na utangazaji
Naomba kuwasilisha wadau
 
Back
Top Bottom