Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 59,188
- 79,401
Mara nyingi hainiingii akilini pale huyu Mh wetu anapowaalika watu kwa mazungumzo na majadiliano ya mwafaka wenye Mstakabali wa Kitaifa halafu pale wahusika (yaani wawakilishi wa wenye kilio) wanapogeuka huyu Mh hufanya yasiyotarajiwa! Tumeona mchakato wa katiba ulipoanza huyu Bwana aliwaita viongozi wa CHADEMA kujadiliana nao baada ya kususia mchakato Bungeni kwa kutoka nje! Na pale wahusika walipotoa pua yao nje ya lango Kuu la Ikulu, huyu Bw. akasaini mabadiliko yale ya katiba yaendelee mpaka na mpaka leo hamna anayejua linaloendelea hata kama kuna kuchukua maoni hamna mtu anayejua wapi yanachukuliwa na hao wachukua maoni watakuja lini! na hii ikiwa haki yetu Kikatiba kama wananchi wa nchi hii!
Hapa juzi baada ya wauguzi na madaktari wetu kulalama bila wafanikio, waliamua kugoma mara 2 bila ya mafanikio wakipewa ahadi na longolongo nyingi waliamua kugoma tena! Huyu Mh kawa kawaida yake aliwaalika wawakilishi wa MAT na mbali na viongozi hawa kuitikia mwito wake kwenda Ikulu na kujadiliana naye, walienda mbali zaidi na kukubali kusimamisha mgomo kwa nia safi! Huyu Bwana siku mbili baadaye alikutana na Wazee wa Dar na utumbo aliomwaga pale hausemeki na kwa kiufupi ni kuruka kimanga madai muhimu ya madaktari na wauguzi wetu katika shughuli zao za kila siku kwa kuyaweka kiporo bila kutoa dira ni vipi atayashughulikia! Kama vile kutafuta mchawi, Mh huyu wa fitna zilizozidi maelezo alienda mbali zaidi kuwaparamia wanaharakati walioandamana kushinikiza serikali yake ishughulikie swala la madaktari na wauguzi kwa kuwaita waliokosa ubinadamu kwa kushinika serikali yake ichukue hatua zipasavyo na kuunga mkono madaktari na wauguzi katika mgomo wao wa kuendelea kuua!
Bwana huyu maarufu kwa uzabazabina alienda mbali na kuwa mkalimani na mtetezi mkuu wa haki za Kibinadamu kwa kuanza kutafsiri haki ya kuishi kama haki ya kwanza ya msingi inayotambulika kwa nchi zoote wanachama wa Umoja wa Mataifa! Katika hali ya kawaida katika kufikiri na kutenda kizembe Bw huyu alienda mbali na kuwasafisha viongozi wawili waliokataliwa na umati wa wafanyakazi walio chini ya wizara wanazoziongoza yaani Waziri na naibu Waziri na pia kutoa dalili ya uwezekano mkubwa wa hata yule Katibu Mkuu aliyesimamishwa kwa tuhuma kibao kurudishwa kazini! Haya yoote yanafanyika kweupe bila kutuambia ni kivipi serikali yake imesimamia haki hii ya wananchi wake kuishi kwa amani na utulivu huku tukijua kwa kipindi choote cha utawala wake kuna maalbino wanaendelea kuishi kwa kuhofia maisha yao na watuhumiwa wapo wametajwa lakini hakuna kilichofanyika kuhusu utendaji wa haki kwa wote! Pili Kizabazabina huyu mpaka leo hajatoa tamko lolote juu ya ukandamizaji na matumizi ya nguvu zilizopitiliza kwa wananchi pale askari wake huko Songea pale walipoamua kutumia bunduki na kusambaratisha maandamano ya amani ya kuishinikiza polisi isimamie ulinzi wa roho za Raia wema waliokuwa wakiuawa kwa sababu za kishirikina! Roho za marehemu wanne zilipotea huko...! Mbali ya hayo suala la utawala bora limeendelea kubaki la kufikirika kwa Mh huyu wa Wazee wa Dar!
katika hali ya kawaida Mh huyu anakosa uhalali wa kuongelea haki ya kuishi kama anashindwa hata kutoa pole kwa waliopoteza uhai uko Songea kwa kupitia kwa wauaji wake walio chini ya uongozi wake! Ila Bw. huyu asiye na soni hakuona hilo ila lile la Madaktari na Wauguzi wetu waliojaribu kutumia kila mbinu ya ustaarabu kudai haki yao ya kuweza kujikimu na kufanya kazi katika mazingira stahili kwa kazi zao hatarishi! Hivi kweli huyu Mh anategemea makubaliano na MAT yaendelee kwa jinsi alivyojirahisisha na kudhihirisha ahadi zake hewa ambazo wakati woote huzitoa na kuzigeuka ndani ya masaa 24 baada ya kuzitoa! Hivi yeye kama kiongozi mkuu wa nchi anategemea nani kuwa msuluhishi kama makubaliano yakivunjika? BTW hii jeuri anaitoa wapi ya kudharau matakwa ya wengi? Tutegemee makubwa haswa pale hulka ya ustahimilivu wa Watanzania itakaposhindwa!