Sifa kumi za mwanamke asiyekupenda

chriss brown

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
292
63
Kwanza ifahamike mapema ninapozungumza dalili za asiyekupenda kwa dhati, sina maana nachonganisha watu katika ndoa zao, ila kuwatanabahisha kaka zangu kugutuka katika maisha yao ya kila siku, kumekuwa na ulahai wa hali ya juu katika ndoa nyingi hapa kwetu Zanzibar na hii yote inachangiwa na ugumu wa maisha kwa ujumla.

Nitajaribu kuziweka bayana dalili za Mwanamke asiye kupenda kwa dhati lakini hii haimaaanishi kuwa ufarakano katika mapenzi yenu bali ukae na kufikiri na kuyapima kwa kina haya ninayoyaandika humu isiwe kuporotoka na kuanza mtafaruku kwa kuwa Abdullmalik kasema.

1 : Hataki kuambatana na wewe katika matembezi na kama ikiwa lazima anakuwa mtu wa masharti mara akuambie tangulia nakuja au kutembea nawe kwa mbali.

2: Anapata kigugumiza kukutambulisha kwa rafiki zake na jamaa zake.Ukimwambia tuachane,atakuambia sawa,ukimpata mke mwenzangu nionyeshe,na mimi ntakuonyesha shemeji yako.Damn women.

3: Haonyeshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleo, kwake ni kufuja na kwenda mbele na huwa mfujaji mkubwa wa pesa na anapokosa kununa kabisa.

4: Anaahirisha kukutana na wewe mara kwa mara, tena bila kukueleza sababu za msingi, au kukutungia uongo wa dhahiri.

5: Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanamme amtakaye sifa zake zinakuwa hazilingani na wewe, kwa mfano atakwambia napenda mwanamme mwenye mwili mkubwa , sifa ambazo wewe huna.

6: Hacheki kwa furaha, hata kama ukimchekesha haonyeshi furaha ya moyoni, ukimwambie twende tukatembee forodhani atakujibu ''Aaah, nimechoka mie nipo nyumbani'

7: Huwa hana wivu kabisa, hudiriki hata kukushawishi uwende Disco peke yako.

8: Hasamehe na kusahau, kosa la mwaka juzi analijengea hoja.

9: Humsisimui katika mambo ya faragha.

10: Mwepesi wa kutoa kauli ya TALAKA, ''kama vipi bora kila mtu akae kivyake vyake'' tena hataki kuambiwa ukweli na anapotokea akaambiwa hujitetea kwa kumtaja mwanaume mwingine '' Mbona Al-Udii (si jina halisi) anamfanyia hili , hamfanyii hivi mkewe'':A S embarassed:
 
Mwingine ukitokea tu ananuna hahahhaaa.....au ukimpigia simu anakwambia 'ntakumpigia sasahivi',ndo imetoka hiyoo..kisha baadae mpka unampigia wewe kisha anakwambia 'nilisahau bahati mbaya jamani'.. Balaaa!
 
mtu kama huyo achana naye kabisa! huwezi kukaa na mwanamke anayemsifia mwanamme mwingine kila saa! wewe ukimsifia mwingine tu kosa kubwa! na kama upo naye akili yake imehamaje kwako hadi kuanza kumuongelea mtu mwingine
 
Dah, I hate that with my whole life!

Sure inakera sana....Mwingine unamkaribisha kwenu mkitoka tu anaanza kuwabeza wazazi wako au nyumbani kwenu..live yaani..Mwingine mkiwa pamoja full kumuongelea ex-boifriend na vituko vyake halafu yeye utakuta ndo anatawala maongezi...hahhaahaaa..
 
Hii kwel inaboa jaman mh me afanye yoote lkn asinibeze kwetu lol tena wazaz wangu! anataka tuachane vibaya.
 
aisee! Kuna dada niliwahi kuwa naye,ukimpigia simu anakwambia niko bize ntakutafuta baadae kidogo. Mtalala mpaka kesho,ukimpia anaanza kukulaumu eti mbona hukunitafuta? Nilikula kona fasta.!!
 
kwanza ifahamike mapema ninapozungumza dalili za asiyekupenda kwa dhati, sina maana nachonganisha watu katika ndoa zao, ila kuwatanabahisha kaka zangu kugutuka katika maisha yao ya kila siku, kumekuwa na ulahai wa hali ya juu katika ndoa nyingi hapa kwetu zanzibar na hii yote inachangiwa na ugumu wa maisha kwa ujumla.

Nitajaribu kuziweka bayana dalili za mwanamke asiye kupenda kwa dhati lakini hii haimaaanishi kuwa ufarakano katika mapenzi yenu bali ukae na kufikiri na kuyapima kwa kina haya ninayoyaandika humu isiwe kuporotoka na kuanza mtafaruku kwa kuwa abdullmalik kasema.

1 : Hataki kuambatana na wewe katika matembezi na kama ikiwa lazima anakuwa mtu wa masharti mara akuambie tangulia nakuja au kutembea nawe kwa mbali.

2: Anapata kigugumiza kukutambulisha kwa rafiki zake na jamaa zake.ukimwambia tuachane,atakuambia sawa,ukimpata mke mwenzangu nionyeshe,na mimi ntakuonyesha shemeji yako.damn women.

3: Haonyeshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleo, kwake ni kufuja na kwenda mbele na huwa mfujaji mkubwa wa pesa na anapokosa kununa kabisa.

4: Anaahirisha kukutana na wewe mara kwa mara, tena bila kukueleza sababu za msingi, au kukutungia uongo wa dhahiri.

5: Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanamme amtakaye sifa zake zinakuwa hazilingani na wewe, kwa mfano atakwambia napenda mwanamme mwenye mwili mkubwa , sifa ambazo wewe huna.

6: Hacheki kwa furaha, hata kama ukimchekesha haonyeshi furaha ya moyoni, ukimwambie twende tukatembee forodhani atakujibu ''aaah, nimechoka mie nipo nyumbani'

7: Huwa hana wivu kabisa, hudiriki hata kukushawishi uwende disco peke yako.

8: Hasamehe na kusahau, kosa la mwaka juzi analijengea hoja.

9: Humsisimui katika mambo ya faragha.

10: Mwepesi wa kutoa kauli ya talaka, ''kama vipi bora kila mtu akae kivyake vyake'' tena hataki kuambiwa ukweli na anapotokea akaambiwa hujitetea kwa kumtaja mwanaume mwingine '' mbona al-udii (si jina halisi) anamfanyia hili , hamfanyii hivi mkewe'':a s embarassed:

you are right mkuu, nilishapata demu wa hivyo sifa zote hizo ulizozitaja alikuwa nazo, nikampiga chini akapata jamaa mwingine akakuta ngoma ngumu sasa anatamani kurudi, ananibip kwa kujichekesha na kuomba mshiko, na amepigika ile mbaya na wazazi na ndugu zake hawasapoti kwa 100% halafu she is still a student anapata tabu mpaka anakuwa omba omba tena kibinadamu namtoa lakini anajutia na anaifizia nafasi ya kurudi tena lakini nampotezea na sina mpango nae tena
 
duh, kazi kweli kweli

@manyanza, unakula mwanafunzi? Hope ni wa chuo ujue mie ni afisa elimu nikisikia ivo waniumiza loho.
 
Bwana weee,hahahah
awa viumbe
ptuuu
Mwingine ukitokea tu ananuna hahahhaaa.....au ukimpigia simu anakwambia 'ntakumpigia sasahivi',ndo imetoka hiyoo..kisha baadae mpka unampigia wewe kisha anakwambia 'nilisahau bahati mbaya jamani'.. Balaaa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom