Sifa 10 za Mafisadi ambazo wasingependa ujue

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Sifa 10 za Mafisadi ambazo hawapendi uzijue!

Baada ya kufuatilia mikakati ya mafisadi na matendo yao ndani ya miaka hii 15 na hasa katika kufuatilia kwa kina mambo yao mbalimbali hatimaye nimefikia hitimisho kwamba mafisadi wanazo sifa kumi ambazo zinawatofautisha na watu wengine. Mafisadi wote wanazo sifa hizi au huongozwa nazo. Ni sifa ambazo wasingependa watu wajue:

10: Mafisadi ni kama wachawi; hawajitaji.

09: Mafisadi hawana mwiko; kwao vyote vinaruhusiwa.

08: Mafisadi hawana dini; imani yao ni juu yao wenyewe na maslahi yao.

07: Mafisadi hawana uungwana. Hawana sababu ya kuwa nao.

08: Mafisadi hawana heshima; isipokuwa kwa mafisadi wenzao.

06: Mafisadi hawaogopi yeyote; wote wako chini yao.

05: Mafisadi siyo bahili; hulipa gharama yoyote kuendeleza ufisadi wao

04: Mafisadi hujaribu lolote; lisipowezekana hutafuta njia nyingine (angalia #5)

03: Mafisadi hawana vyama vya siasa; utawakuta popote

02: Mafisadi hawajulikani kwa kuwaangalia kwa nje; wanaonekana waadilifu!

01: Mafisadi ni wenzetu na jamaa zetu; wakati mwingine ni SISI WENYEWE!
 
Ungeanza na ku define ufisadi ni nini? Maana usije kuta kuna maana nyingi za neno fisadi...
 
.....Ufisadi ni Fikra Potofu zinazopelekea Matendo Potofu.

Kuutokomeza Ufisadi, inahitaji mabadiliko ya Fikra.
 
09: Mafisadi hawana mwiko; kwao vyote vinaruhusiwa.

Kula huku kula gani
Mwala hata visivyolika.

Kula huku kula gani,
Mwala huku mnacheua....

Napenda sana shairi hili...
 
.

08: Mafisadi hawana dini; imani yao ni juu yao wenyewe na maslahi yao.
mbona mmoja wao msemaji mkuu wa familia yake ni ASKOFU?unless,you tell me otherwise kwamba:
-dini ya yule askofu SIO DINI
-au uniambie yeye si FISADI
 
mbona mmoja wao msemaji mkuu wa familia yake ni ASKOFU?unless,you tell me otherwise kwamba:
-dini ya yule askofu SIO DINI
-au uniambie yeye si FISADI

Mhhh...!

Haya sasa, lile jambo limezua jambo, ngoja tumsikilize mwenyewe!

Geoff, Heshima mbele young Broda:)!

Lakini mi nilivyomwelewa MKJJ, ni kwamba amechukua situation GENERALLY, na si kwa kumpoint mmojammoja.

Lakini pia, dini ni matendo..."Dini miliyo njema ni kuwasaidia masikini, kutembelea wafungwa, na kuwapa wahitaji...". kwahiyo mtu kama hafanyi hayo ni kama vile hana dini.
 
....kwamba mkjj is not PRECISE!:D?
 
mbona mmoja wao msemaji mkuu wa familia yake ni ASKOFU?unless,you tell me otherwise kwamba:
-dini ya yule askofu SIO DINI
-au uniambie yeye si FISADI

wanaweza kuvaa roman collar na kusimama kwenye mimbari na wanaweza kushika tasbihi mkononi na balakeshea.. lakini hicho ndicho tunachokiona; moyoni mwao wanaamini haki yao wao kufanikiwa na kutumia njia yoyote wao kufanikiwa; hawana dini isipokuwa wao wenyewe!
 
got it!......
na hawa ''maaskofu'' WASEMAJI WA FAMILIA?.....?!
 
Mimi ni mwanachama mpya ninayejulikana kwa jina la Madoshi Kuzenza wa Geita. Nitakuwa pamoja nanyi katika kupokea na kutoa maoni katika mambo mbalimbali ya msingi. I hope you enjoyed your Xmas. Cheers.
 
Siku hizi dini inatumika tu kama mwavuli wa kufanya ufisadi. Fikiria ufisadi wa mama rwakatare.....anantumia dini ili kuhifadhi fedha za mafisadi na pia yeye mwenyewe anatumia dini kufanya ufisadi.

Mbaya zaidi ameingiza na uchawi ili kuuimarisha ufisadi wake kwa mgongo wa kanisa. Mwangalie kakobe, amekwiba dhahabu za walala hoi akisema ni anasa lakini walipo zitoa kanisani kwake kama sadaka yeye kaziuza na kuijiimarisha kifedha za kuendeleza mradi wake (kanisa).

Hakika mafisadi hawana dini ila wanatumia makanisa na misikiti kuimarisha ufisadi wao. Mwangalie Mzee yahya.....anantumia dini ya uislamu kufanya ufisadi wake, mbaya zaidi amejikita zaidi kuhubiri uchawi na hata kutishia wale wanaopinga ufisadi kwamba watakufa.
 
Kwa maana nyingine ni kwamba, hawa jamaa kulingana na tabia yao kuwa tofauti na mwonekano; tunaweza kusema wamevaa ngozi ya kondoo kumbe ni mbwa mwitu! Nafikiri hii itawakilisha vyema kundi hilo lisilohitajika katika jamii ya watanzania kwa vile kazi yake ni kuwinda na kukilalua kila kilichokusanywa kama kodi kutoka kwa watanzania ambao wengi wao ni maskini wa kutupwa.
 
Mimi ni mwanachama mpya ninayejulikana kwa jina la Madoshi Kuzenza wa Geita. Nitakuwa pamoja nanyi katika kupokea na kutoa maoni katika mambo mbalimbali ya msingi. I hope you enjoyed your Xmas. Cheers.

Mkuu karibu jamvini, vipi Geita bado barabara ni vumbi au kuna mabadiriko?
 
Siku hizi dini inatumika tu kama mwavuli wa kufanya ufisadi. Fikiria ufisadi wa mama rwakatare.....

-anantumia dini ili kuhifadhi fedha za mafisadi

-anatumia dini kufanya ufisadi.

-ameingiza na uchawi ili kuuimarisha ufisadi wake kwa mgongo wa kanisa. .
tunaomba JUSTIFICATIONS za ufisadi wa huyo mama,PLEASE!......

-Mwangalie kakobe, amekwiba dhahabu za walala hoi akisema ni anasa lakini walipo zitoa kanisani kwake kama sadaka yeye kaziuza na kuijiimarisha kifedha za kuendeleza mradi wake (kanisa)..
huyu mzee MNAMUONEA BURE!hana hizo fedha nyingi za kujiimarisha.napafahamu hadi anapoishi,hadi gari anayotembelea!huyu mzee sio mbinafsi wala sio tajiri kama MWINGILA

- Mzee yahya.....anantumia dini ya uislamu kufanya ufisadi wake,

-Mzee yahya amejikita zaidi kuhubiri uchawi na hata kutishia wale wanaopinga ufisadi kwamba watakufa.

HUYU MZEE ANAZEEKA VIBAYA!actually njaa ni mbaya sana.inawalazimisha watu kujipendekeza
 
Sifa 10 za Mafisadi ambazo hawapendi uzijue!

Baada ya kufuatilia mikakati ya mafisadi na matendo yao ndani ya miaka hii 15 na hasa katika kufuatilia kwa kina mambo yao mbalimbali hatimaye nimefikia hitimisho kwamba mafisadi wanazo sifa kumi ambazo zinawatofautisha na watu wengine. Mafisadi wote wanazo sifa hizi au huongozwa nazo. Ni sifa ambazo wasingependa watu wajue:

10: Mafisadi ni kama wachawi; hawajitaji. - e.g. KAGODA establishment

09: Mafisadi hawana mwiko; kwao vyote vinaruhusiwa. E.g Hakunaga utawala wa sheria. hakuna aliemsafi CCM, Bunge kazi yake ni kushauri tu na pia hata rais akimteua mkewe kuwa PM nani anahoji? Wamejitengenezea mfumo

08: Mafisadi hawana dini; imani yao ni juu yao wenyewe na maslahi yao. Na kama wanayo hawapendi ichanganywe na siasa. Wanataka kutenganisha eti dini kazi yao ni kuandaa maisha yajayo. Ulimwengu mpya

07: Mafisadi hawana uungwana. Hawana sababu ya kuwa nao. Wakiwa waungwana watakosa mtaji. Eti uzungumzie UBORA WA ELIMU, BORA MAJENGO bwana.

08: Mafisadi hawana heshima; isipokuwa kwa mafisadi wenzao. Utamsaidia nini, labda liwe group la watu kwa ajili ya interest zao!

06: Mafisadi hawaogopi yeyote; wote wako chini yao. Maana wamewekana ili kulindana.

05: Mafisadi siyo bahili; hulipa gharama yoyote kuendeleza ufisadi wao. E.g. Msaada wa 400millions kutangaza biashara.

04: Mafisadi hujaribu lolote; lisipowezekana hutafuta njia nyingine (angalia #5). Chimbuko la vita ya wenyewe kwa wenyewe.

03: Mafisadi hawana vyama vya siasa; utawakuta popote. Popote penye maslahi au panapotishiwa maslahi, athari zake angalia #4.

02: Mafisadi hawajulikani kwa kuwaangalia kwa nje; wanaonekana waadilifu! Utamtambuaje? Matendo? tafakari. Hapa ndipo pagumu na kwame hawatoi nafasi hii. Angalia #7.

01: Mafisadi ni wenzetu na jamaa zetu; wakati mwingine ni SISI WENYEWE! Sio lazima ufisadi mali za umma hata za nyumbani na ofisi yako. Unafahamu wajibu wako?

MMKJJ nimejaribu kuweka nilivyokuwelewa. Asante
 
Back
Top Bottom