Sielewi nimepatwa na nini mwenzenu...

Kaka kama ulikuwa hujaenda naye mbali huyo mchumba wako wa awali i mean hujamuahidi kitu kama ulivyosema ulitaka kum surprise basi chukua roho inataka. Lakini unaonekana kuwa na tamaa hapo sina cha kukushauri maana kesho utakuja tena kusema nimeona mwingine yuko moto kweli kweli. Cheza na roho yako kama unajua huyo ndo mwisho wa maneno na hutakuwa na tamaa basi jimwage tu.
 
Wewe ni weak kwa mapenzi na hata ukionjeswa na mwingine utaona naye ana akili zadi ya huyu aliyekuchanganya, tumia akili zako za kuzaliwa ujue utafanya nini? umelewa utamu wa demu mpya
 
Mkuu,,,angekuwa ni huyo mpenzi wako amepata bwana akataka kukuacha bila sababu WEWE UNGEJISIKIAJE, Kumbuka unachotaka kukifanya ni uuwaji,,, na malipo yake ni hapa hapa duniani,,,, wewe umeshampotezea mtoto wa watu muda sasa unataka kumwacha bila sababu ya msingi,,,angekuwa ni dada yako au ndugu yako amefanyiwa kama unavyotaka kufanya utajisikiaje,,,, kumbuka hapo umeenda Arusha ukampata huyo bado hujaenda Mwanza, Dodoma wapo wengi tu na inaelekea utawapenda na huyo wa Arusha utamwaona si kitu kwako

Mkuu acha hicho kitu unachotaka kukifanya kitakugarimu maisha yako yote,, na ni vema tukawaheshimu hawa dada zetu
 
maana mtu kwenye mkutano tu umeshajua yuko HOT!!

yaelekea ww ni walewale sketi isipite mbele yake wataka kuona imepindiwa uzi wa rangi gani halafu unajiita mtu wa msimamo ! kwanza nikuulize una msimao upi wakuangalia sketi gani imekupitia au.....

1.Mara yamwisho kwenda angaza ilikuwa ni lini?? ...15.01.2010 na sikwenda angaza nilipima ngoma Agakhan hospital nilikuwa niko fit tu mkuu.

2. Si kweli kuwa mimi ni wale wale sijui ni akina nani hao wale wale.
3. Kumpenda mtu huitaji mabavu au kuchukua miaka..muhimu ni hisia tu.
4. Mi siangalii sketi mkuu ni jambo linaloweza kukutokea hata wewe kama mwanaume rijali.
 
Mkuu,,,angekuwa ni huyo mpenzi wako amepata bwana akataka kukuacha bila sababu WEWE UNGEJISIKIAJE, Kumbuka unachotaka kukifanya ni uuwaji,,, na malipo yake ni hapa hapa duniani,,,, wewe umeshampotezea mtoto wa watu muda sasa unataka kumwacha bila sababu ya msingi,,,angekuwa ni dada yako au ndugu yako amefanyiwa kama unavyotaka kufanya utajisikiaje,,,, kumbuka hapo umeenda Arusha ukampata huyo bado hujaenda Mwanza, Dodoma wapo wengi tu na inaelekea utawapenda na huyo wa Arusha utamwaona si kitu kwako

Mkuu acha hicho kitu unachotaka kukifanya kitakugarimu maisha yako yote,, na ni vema tukawaheshimu hawa dada zetu
...nashukuru mkuu. Lakini mi naheshimu kile mtu atakachoamua, kwani kama yeye angepata bwana akaenda ni jambo limetokea siwezi kubadili matokeo kwani maisha yanatakiwa kuendelea. any way thanks nitachanga karata ninavyojua ila sina lengo la kumuumiza mtu!
 
mkuu majibu yoote kakupa masaki hao nami nakubaliana naye unajua mimi nimeoa mei 1, 2010 ni kweli unapofanya maamuzi mazito ya kuoa majaribu huwa yanakuja just kutest ur strength but mind you anayekuja ghafla pia huondoka ghafla

please muingage mchumba wako fasta

pleae be advised accordingly
 
Duh! pole sana.
nadhani hapo ni tamaa tu. tulia itaisha na utaendelea na mchumba wako wa kwanza.
 
SAJENTIIIIIII................Unataka kufanya kosa kubwa sana katika maisha yako na utalijutia milele! Take my words! Mchumbie mchumba wako haraka iwezekanavyo na usisubiri mambo ya July 24. Hayo ni majaribu tu, na huyo binti mpya ana kasi sana na ndicho kinachotia shaka. Pia wakati wa kufanya maamuzi mazito kama kuoa au kuolewa, watu hukumbwa na vishawishi vingi ambavyo wala huwa hawakuvitegemea na wala hata hujui vimetoka wapi.

Kama una sikio la kusikia na unisikie sasa.....BETTER THE DEVIL YOU KNOW THAN AN ANGEL YOU DON'T KNOW!


Mkuu Masaki, Nakushukuru sana..Hapo kwenye red nahisi umeniamsha usingizini...Ubarikiwe bana!
 
...umepatwa na pepo!
Kitendo tu cha kukutana na msichana na kumsahau mchumba wako mtarajiwa ni kosa la jinai! (ungekuwa huku UAE tungekupiga na mawe)
Yaani unataka kusema kila unpomwona msichana mrembo unalala naye kwanza ujue wa baridi ama moto..
1. Unahitaji sala ya toba na umpokee bwana Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako.
2. Then uende kwa huyo mchumba wako mtarajiwa na umweleze kwamba akuache kwa sababu u r not worth to be with her.
3. U should be ashamed of this
4. Mwanaume rijali ni yule anayeweza kuzuia hisia zake mpaka wakati muafaka (definition yako ya urijali ni ya kishetani!)
5. Huyo ni wa Arusha na I guess ulienda kwa ndege maana ungepitia Moshi uwaone wa Kichagga..cjui kama ungerudi.
6. Huyo mtoto (regardless the lady u choose) kamwe usimpeleke boarding wakati ni mdogo hivyo..bado anahitaji malezi ya baba na mama.
7. On second thought, ni afadhali aend boarding..kwani u r not a father type! (unless ubadilike)
8. It takes more than love to be with someone. R u two compatible with each other??!
9. One measure of love is the time test: have you wintered and summered with the lady you have just met? ama ni kupagawishwa na mtoto wa kimbulu...unadhani umependa!!! atleast angekuambia yuko tayari kuishi na mtoto, kumlea kama mwanae, kumsaidia..etc! lakini hiyo ya boarding...ni kumfukuza bila kumwambia toka!
10. u need a thorough soul search!
11. usiache Dhahabu kukimbilia scraper! (huyo mwanamke aliyekubali kulala nawe even kabla ya ndoa au kufahamiana..kwangu ni malaya tu!) Sasa sijui ameshaenda conference ngapi since hiyo ya Arusha...tafakari!
12. Ebu nipige thanks kwanza!

samahani kama nimekukwaza...
 
..Thanks bht, lets agree 2 disagree!!

ndio, mimi siwezi kukusapoti bana,

its like u dont even know wat u want so far!!! maana una-intertain na hizo simu za kutwa mara tatu. umejiachia uanguke majaribuni kaka!!! vizuri haviishi, kesho utaenda mwanza mkutanoni ukutane na wakisukuma na huyo wa arush utammwaga.

hebu kuwa na msimamo bwana!! nikuulize, huyo mtoto ni wa huyo mchumba mtarajiwa ulizaa nae??

''with fire we test gold and with gold we test our servants''

test are there to make u strong babaa!!
 
Mimi ni mtu wa misimamo sana lakini katika hili najiona nimepigwa bao sielewi ni mapenzi tu; KWANZA POLE SAANA. UMEKUWA NA UHUSIANO NA WASICHANA WATATU KAMA ULIVYOELEZA. NI VEMA UELEWE KUWA HAYO YANAYOKUSUMBUA SIYO MAPENZI MBALI NI TAMAA(LUST). TAMAA YA MWILI NI TATIZO KUBWA NA ILI KUPONA NI VEMA KUMWOA MPENZI WA ZAMANI NA KUACHANA KABISA NA HUYO MWARUSHA SIJUI...UWE MAKINI, HATA UKIOA WAZURI WATAKUWEPO TU. Wenye msimamo kamili ni waaminifu na hata hawatembei nje ya ndoa. Kabla ya kuoa au kuolewa huwa wana 'abstain' wanajinyima. YOOTE YANAWEZEKANA! ADIOS!



 
Majuto ni mjukuu! sajenti nakwambia tene na tena majuto ni mjukuu. Umesema mwenyewe kua unapendana na mpenzio, na wala hamjawah kukorofishana, hata mngekua mlishawah hyo ni kawaida2. Hakika utakuja juta kama utamwacha mpenzio wa sasa kisha huyo wa kurukia, yeye ni mwizi na wewe umelogwa2 mawazo unachotakiw ni kus2ka.rudi kwa mkeo mtarajiwa huna sababu ya kujustify kumwacha, pain utayomsababishia itatosha kuhalalisha laana kwako na kwa huyo mwanamke mwizi.

KAMA KWELI UMETAKA USHAURI TAKE THIS OF MINE NA THAT OF MY BROTHER ,MASAKI.
 
Ukimalizana na huyu unaemwita mpya utamwona mwingine mpya zaidi na anayekwambia atakujengea nyumba uishi bure, na usafiri juu yake!
Mwanaume usipokuwa na msimamo uko sawa na maiti!...utabebwa kwenda hata usikotaka!.Period!
 
Daa,haki ya nani,hii dunia imejaa kila aina ya vituko.Pole sana Mkuu.Jipe muda utafakari kwa kina juu ya mapenzi yako kwa hawa wadada.Inawezekana hujampenda huyu wa sasa ila ni mvuto tu ulionao juu yake na hivyo ukahisi kwamba unampenda kumbe la..Jipe muda jichunguze kwa makini..
 
Mke mwema mtu hupewa na Bwana, hapo kujudge ni ngumu sana, wewe sio wakwanza kufanya hayo mambo kuna watu wanafikia mpaka stage ya uchumba na ndoa inashindikana, JARIBU KUWA NEUTRAL, NA KUFANYA ANALYSIS ZISIZOKUWA BIASED KWA UPANDE WOWOTE NA KISHA FATA MOYO WAKO KATIKA HAKI NA UKWELI, UWEZI KUOA KWA SABABU UMEISHI NA MTU MUDA MREFU NA PIA HUWEZI KUOA KWA SABBABU MWANAMKE ANA AKILI YA MAENDELEO NA ATAKUSOMESHEA MTOTO
...Mkuu kituko nakubaliana na wewe. Umeongea mambo makubwa mawili yenye msingi sana. Nasikitika kuna baadhi ya wanaJF humu wamekuwa wepesi wa kuhukumu. Laiti ningekuwa na uwezo wa kusoma upande wa pili maisha yao nina imani ningeonekana bora maradufu..any way dunia ni watu na watu wenyewe ndio hawa hawa...Twende kazi.
 
Back
Top Bottom