GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,546
- 108,876
Kwanza nianze kabisa kukiri kuwa nami ni mmoja wa Wadau wenu wa Kipindi chenu cha 360 hasa kutokana na aina yenu ya Kipekee kabisa ya uwasilishaji wa ' issues ' ambazo mmezifanya ziwe na mvuto na unalazimika tu kuangalia kipindi chenu kila kukicha. Hongereni kwa hilo!
Naomba nitakachokiandika hapa msikipokee kwa ' jicho ' tofauti dhidi yangu bali mnaweza tu mkachukua lile ambalo mnaona ni jema na kama mtaona hakuna cha kuchukua pia si vibaya japo najua nitakuwa nami nimewasilisha maoni yangu kwenu.
Tunajua kuwa Mtangazaji wenu Hudson Kamoga sasa yupo huku Mbulu akiwajibika ' kiserikali ' baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais hivyo mlikuwa mnahangaika labda kumtafuta ' mbadala ' wake hapo kitu ambacho kwa sisi Wadau wa Habari na Mawasiliano huwa si kitu rahisi kama ambavyo Watu wengine hufikiri.
Naona leo mmeanza rasmi na Utambulisho wa Mtangazaji wa Clouds fm Bwana Mdogo Michael Lukindo kama mtangazaji mwenza wa Program Host wenu mpya Dada yangu Babie Kabae huku Comrade wangu Samuel Nathaniel Sasali akibakia pale pale katika ' magazeti ' huku akichagiza na kupendezesha Kipindi chenu kwa ' ukomedi ' wake.
Namkubali mno Michael Lukindo hasa kutokana kwamba namfahamu na najua uwezo wake ila ' technically ' sishauri huyu Kijana awe Co Host wa Babie Kabae na badala yake ningeshauri mtafuteni Mtu mwingine ambaye anaweza akawa sambamba na Babie Kabae hasa ' kimtazamo '.
Kuna tofauti kubwa sana ya Utangazaji wa Tv na wa Redio na kwa Wadau wa Tv watakubaliana nami kuwa hakuna kitu kibaya kama kumfanyia Mtu ' majaribio ' ya Utangazaji katika Television kwani impact yake kwa audience kama akionekana tu ' kuharibu ' inaweza kuwa kubwa na kujikuta unaanza kuwapoteza ' walaji ' wako wote.
Michael Lukindo anaoneka dhahiri kusumbuliwa na haya yafuatayo:
Sina mengi zaidi ya haya na nawatakieni majukumu mema na nakaribisha pia ' kukosolewa ' kama na Mimi ' nimekengeuka ' juu ya hayo niliyoyaeleza kwani humu Wote tunaelimishana na kukosoana kwa Hoja.
Akhsanteni.

- Bado ana ' utoto '.
- Siyo ' knowledgeable '.
- Hana Media ' exposure '.
- Hayuko ' natural ' hasa katika Sauti yake na nadhani kuna Mtu anamuiga.
- Ana bana mno ' sauti ' kitu ambacho ' sometimes ' kinatufanya tuhisi kuwa wapo watangazaji wawili ( 2 ) wa Kike wakati kumbe kuna Mwanume na Mwanamke.
- Ni ' mkurupukaji ' na anapenda ' kudakia dakika ' pasipo kutafakari kwanza.
- Hayuko ' serious ' na anafanya hapo Studio kama ' Kijiweni ' tu.