Elections 2010 Side Bar: CHAKACHUA

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,547
19,411
Neno chakachua leo hii linajulikana kama njia ya Kikwete na CCM kujipatia idadi ya kura rasmi za NEC zaidi ya kura halisi walizopigiwa na wapiga kura. Lakini hasa asili ya neno Chakachua ni nini?

Chakachua ni neno lililobuniwa na aliyekuwa mwanamziki mashuhuri na kiongozi wa bend ya Urafiki Jazz band aliyejulikana kama mtoboa siri au Juma Mrisho. Chini ya Uongozi wa Juma Mrisho, bendi ya urafiki ambayo ilikuwa inamilikiwa na kiwanda cha nguo cha urafiki walibuni mtindo uliokuwa ukiitwa "Mchaka Mchaka." Walitumia mtindo huu kwa muda mrefu kuanzia nadhani mwishoni mwa mwaka 1969 au mwanzoni mwa mwaka 1970 (sina uhakika sawasawa) hadi mwishoni mwa miaka ya sabini wakati waliopoharibikiwa vyombo vya mziki na kushindwa kupata vyombo vingine. Baadhi ya nyimbo maarufu zilizotolewa na Juma Mrisho chini ya mtindo huo wa Mchaka Mchaka ni pamoja na "Gezaulole", "Mauaji ya Soweto", "Papara Zako Acha", "Eva Umeumbika", "Mpenzi Acha Kunitesa," na "Tucheze Mchakamchaka." Mtindo huu utakumbukwa sana na wapenzi wa muziki wa wakati huo kutokana na jinsi ulivyokuwa unatumia mdundo mzito sana wa gitaa la rhythm, ambalo sikumbuki lilikuwa linakung'utwa na nani. Mpigo wao ulikuwa ni tofauti sana na bendi nyingine zilizokuwa zinatumia sana gitaa la solo.

Sasa uchezaji wa mtindo huo wa mchaka mchaka ndio ulipewa jina la "kuchakachua." Ilikuwa ni kawaida sana kwa bwana Mrisho kumalizia ubeti wa mwisho wa wimbo wowote akipokea ule mdundo wa rhthym na kusema "Chakachua!!!"
 
Back
Top Bottom