Siasa zetu zinatengeza Bomu la vijana

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo ya chuo kikuu (UDSM) miaka ya 90 nilikutana na rafiki yangu tuliyesoma naye nikamuuliza mwezangu umeshapata kazi? akasema, tena kazi niliyonayo ni kubwa nikamwambia hongera sana ni kazi gani hiyo jibu alilonipa ndilo limenifanya kuandika makala haya akasema, nafanya kazi kila siku kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 11 jioni lakini silipwi mshahara, unajitolea? hapana ila 'Kazi yangu ni kutafuta kazi'.

Jibu hilo ni matokeo ya sera na mazingira ya siasa ya nchi yetu yaliyowafanya vijana wengi waonekane kana kwamba ni wazembe hawataki kufanya kazi kumbe maskini wa Mungu kazi yao ni kutafuta kazi. Vijana wamenyimwa fulsa ya kutawala mawazo yao, popote wanapokwenda wanakutana na ukuta mkubwa uliojengwa ili wasipite, iwe kwenye sekta rasmi au isiyo rasmi, iwe kwenye siasa au kwenye kazi za kitaaluma. Mazingira ya kisiasa yamejenga hisia za watu kiasi kwamba kijana anaonekana yeye kama part of the problem badala ya kuwa part of the solution in decision making, kijana ametengwa na system hana sehemu ya kutolea mawazo yake anayodhani yanaweza kuchangia maendeleo ya taifa lake. Kijana huyu akibahatika kupewa nafasi inaonekana kama hisani tu (privilege) kwake na wakati wowote anaweza kunyang'anywa.

Msekwa_Nape_Nnauye.JPG


Sera hizi za kuwabana vijana kuwaona hawana uwezo wa kujisimamia ndizo zilipolifikisha taifa lilipo, taifa linazalisha wamachinga wasomi (wenye taaluma) kama huyo rafiki yangu na wamachinga wasio na taaluma. Kijana anapojitahidi kupenya kwenye sekta hizi kwa elimu yake au kwa bidii na nguvukazi yake anaambiwa hana uzoefu hajakomaa asubiri muda wake anataka kuleta fujo anaambiwa anyamaze wakati mwingine anatishwa kwa bunduki au kupigwa risasi kabisa. Machinga msomi anazunguka na vyeti vyake mitaani jioni anarudi nyumbani bila matumaini yeyote, machinga asiye na taaluma anazunguka mitaani akiuza tai mbili mkononi bila kupata mtu wa kununua na akibahatika kupata askari wa jiji anamnyang'anya hata kile kidogo alichopata.

vurugu10.JPG


(Mtoto(kushoto) akimshangaa kaka yake kuwashambulia askari wenye bunduki
kwa kijiwe kidogo angalia nyuso na matumaini ya watoto wote wawili)

Kundi hili linazidi kuwa kubwa siku hadi siku na sioni uongozi ukiandaa mikakati yoyote ya kulipunguza. Ni hatari sana itafika wakati serikali itashindwa kulidhibiti. Hatari kubwa iliyo mbele ni pale haya makundi mawili yatakapogundua kuwa yana matatizo yanayofanana na kudhani adui wao pia ni mmoja ni wale wanaowanyima fulsa ya kujitafutia kipato. Watasema enough is enough hawataogopa risasi kijana atadhani kijiwe kidogo alichonacho mkononi kitamsaidia dhidi ya asikari mwenye siraha na hakuna wa kumzuia atasema liwalo na liwe.

Sitaki kijana afikie hatua ya kusema liwalo na liwe, Serikali iliangalie hili kama tatizo kubwa ikiwezekana ilishughulikie kama janga la taifa iwape vijana fulsa ya kushiriki kwenye ngazi mbalimbali za maamuzi kama vile bunge, ianzishe mabaraza ya vijana, ibuni sera nzuri za michezo ili kuwavutia vijana na kuwaacha waamue wanataka wajiendeshaje wazee wawe washauri tu. Hii logic ni simple sana mtu hawezi kulaumu matokeo yoyote yale iwapo alishiriki kuyaandaa. Vinginevyo bila mikakati mizuri ya kuwapa vijana uhuru wa kujiamlia mambo yao wenyewe watafikiri matatizo wanayoyapata yametengenezwa kwa makusudi na kundi fulani ili wao waumie hivyo kuletea vijana kuilaumu serikali na kwa serikali kutowasikiliza vijana itakuwa inajitengenezea bomu lake yenyewe BOMU LA VIJANA.

Makala haya yametayarishwa na Luteni member wa JamiiForum.
Aksanteni.
 
Serikali imewasahau sana vijana haina sera madhubuti za kumwendeleza kijana,
vijana wanaunga na kuanzisha shughuli ya kujiingizia kipato lakini madhalani kigenge cha chips
bila kujali hasara watakayopata wanakuja wanawamwagia vyakula vyao au kuvichukua.
Huyo machinga hatafanya kitu lakini kitendo hicho hatakisahau lazima siku moja atakuja kulipiza kisasi.
 
Back
Top Bottom