Siasa za udini ni hatari kwa umoja wetu

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
katika uchaguzi wa 2005, Waislam walikuwa 3 (Kikwete, Salim na Kigoda) na Wakristo zaidi ya 10 walijitokeza kugombea Urais kwa tiketi ya CCM. Kati ya hao waislam 2 ( Kikwete na Salim) na Mkristo 1( Mwandosya) ndio waliopenya kufikia tatu bora. Ndani ya mkutano mkuu wa CCM wakristo ni robo tatu zaidi ya waislamu lakini walimchagua Mwislamu kugombea Urais kwa tiketi ya CCM na baadaye ndiye akawa Rais wetu. Wakumbuke akina Sumaye, ambaye wakati huo alikuwa waziri mkuu na ushawishi wa kutosha lakini hakufua dafu mbele ya nyota ya kikwete.

Chunga sana ulimi wako, leo hii baadhi yetu tunageuka kwamba Wakristo wanaichukia serikali ya awamu ya nne. oooh my God tunakwenda wapi Tanzania?

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2005, MBowe alikuwa ni mkristo mwenye nguvu kutoka chama cha upinzani lakini Maaskofu wengi akiwemo msaidizi mkuu wa Pengo Askofu Kilaeni walisema Kikwete ndiye chaguo la Mungu. Hii ilikuwa habari njema kwa mshikamano wa wakristo na waislamu. Wapenda amani tunaona ni jambo jema.

Mwaka 2010, wakristo hawakujitokeza kumpinga kikwete ndani ya kura za maoni za CCM wakiamini kwamba bado Kikwete ndiye bora hata kama walikuwepo WAKRISTO wenye sifa na vigezo vya kutosha. Hii ni habari njema kwa umoja wetu.

Mwaka 2005, Rais wa Tanzania aliyekuwa anamaliza muda wake na mwenyekiti wa CCM alikuwa Mkapa ambaye ni mkristo na Mkatoriki chini ya Pengo na Katibu mkuu wa CCM alikuwa Philip Mangula mkatoriki mwingine. Hawa wote waliona kwamba Mwislamu Kikwete ni bora zaidi kuongoza nchi yetu. Kilikuwa ni kitendo cha upendo mkubwa kwa taifa letu.

Upofu huu wa kukumbatia udini na kuhamasisha udini ni janga la kitaifa, moto utawaka na mbaya zaidi wote tunaishi ndani ya nyumba moja inayoitwa Tanzania tutakuwa sehemu ya wahanga wa udini huo.

Yesu na mtume Mohammed wakitumwa na Mungu kuja kueneza dini za Ukristo na Uislamu. Hawa mitume walikuwa na nguvu zaidi ya binadamu yoyote lakini mpaka wanakufa hawakumaliza kazi waliyotumwa na Mungu ya kuifanya dunia kuwa na dini moja.... sembuse sisi? sasa ni miaka zaidi ya 2000 tangu kazi ya Yesu na Mohammed ilipofika duniani lakini ajabu Uislamu na Ukristo unazidi kukua duniani kwa kasi ya ajabu, kwa maana ya idadi ya watu na jiografia ya kusambaa kwa dini hizo.

Ndugu zangu watanzania, kuikumbatia dini yako ni jambo jema lakini dini yako ikikutuma kuichukia dini ya mwenzio ni hasara ya maisha kwani kitendo hiki kimewagharimu wengi. Watu wenye matendo hayo ama wakristo au waislamu nendeni kuchungulia majumbani mwao utakuta wameacha kabisa kutumia muda wao kuboresha uchumi wa familia zao hadi wanakufa watoto wanateseka kwa sababu walitumia muda wao mwingi duniani kupambana na dini nyingine.

Kamwe Ukristo na Uislamu hautatoweka duniani hadi siku ya kiama.
 
Back
Top Bottom