Bahati nzuri nilipiga kura jimbo la Ubungo, niambie ni wanafunzi gani waliompigia kura Mnyika?
mkuu,usihangaike na hawa viruka njia wasiojitambua!
Bahati nzuri nilipiga kura jimbo la Ubungo, niambie ni wanafunzi gani waliompigia kura Mnyika?
Chadema ingekuwa kimbilio mngeenda kujificha kwenye UKAWA?
CCM - Wanaiogopa CHADEMA na kutumia nguvu kupita kiasi kukidhibiti: Wamesahau/wameifunika itikadi yao imara ya 'Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea'
Je ni kwasababu wametekwa na woga wa kivuli chao kinacho sababishwa na mwanga wa CHADEMA? Au ni makusudi kwakuwa viongozi wake wamekiuka miiiko ya chama na wanahangaikia mapenzi yao binafsi? Je vingozi hawa wanaopotosha misingi imara ya Chama cha Mapinduzi wanahofia kuadhbiwa ndo maana wanapambana chama kubaki madarakani au wana nia ya kweli ya nchi hii? chama hiki kitapona na shutuma za undugu?
CHADEMA- Wanadai mabadiliko, yapi? Sikumbuki kuona orodha! Na wanaletaje mabadiliko hayo wanayodai? Wamefanikiwa kuwatisha viongozi wa CCM, kwakuwa wako gizani wamewamulika na tochi ya ghafla, Mwanga wa CHADEMA unatokana na kurunzi yenye tochi imara au za muda tu ambazo zinaweza kufifia kutokana na jazba badala ya sera? Chama hiki kitapona na shutuma za ukabila?
CUF- Walilewa mapenzi ya CCM huko Zanzibar, wanaibuka na kukumbuka wakati wa uchumba, mambo yalikuwa machungu, lakini wakakubali ndoa, sasa wanashtuka kuwa ndoa yenyewe inaweza kuwa chungu kama ile ya uchumbani? Je wameanzisha itikadi ileile ya misingi ya "Kufa baadhi ili wengine waishi milele"? Hawa waliozinduka ni watoto wa kambo wa bara? Wa Zanzibar wana hisia zile zile bado? Je wamegundua kuwa kuna Mke mpya anakutarajiwa kuolewa na CCM? Na wivu umewajaa wanaanzisha kampeni za kumchukia mume wao ili hata huyo mrembo mpya asiingie? Safari Hii CUF itapona na shutuma za udini?
Nia yao ya kugombania kushika madaraka ya nchi hii ni dhati na ya kweli? Au tutaona ya nchi jirani za Zambia na Malawi ambapo waliogombania madaraka kutoka upinzani walifanya madudu zaidi ya yale tuliyoyaona?
Nani kati ya hawa watatu ambao bila ubishi wanashikilia hatamu ya siasa za Tanzania, atatupeleka kwenye nchi yenye neema na amani kwa watu wote bila kujali itikadi, hali yao kiuchumi, kisasa, kidini au kiasili? unahitaji nini kati yao, moja wapo ya chama hiki au Kiongozi kati yao atakaebadilisha upepo na kutuepusha na mgao unaofanywa na vyama vyote hivi (kwa manufaa ya hao wanaoongoza vyama hivi kwa kuwa wanataka kuendelea kuwepo madarakani?) Huko madarakani kuna nini?
Nani atatuambia tutatokaje na siku moja itakayolengwa kwa sisi kuwa sehemu ya taifa Afrika, au Duniani imara kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kimaendelo kwa ujumla (sayansi, usalama wa chakula, nafasi sawa ya elimu kwa wote, huduma za afya wote, maji safi kwa wote, ziada ya fedha, dhahabu na mafuta ambavyo tunavyo na kila mtu akimvumilia mwenzake na kumheshimu).
Kama ungependa kunukuu makala hii kwenye gazeti, wasiliana nami kwa kuni PM.