Siasa za kinafiki kama za ccm zinafaida gani kwa taifa?

Noti mpya tz

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
974
244
Nitatoa mifano michache ya kinafiki iliyopatwa kufanywa na ccm na viongozi wake wa serikali.
Baada ya slaa kutangaza majina ya mafisadi ile list of shame rais kikwete alisema kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala lakini baadae alikuja kukubali serikali yake kuanguka baada ya waziri mkuu el kubwaga manyanga bungeni... Haya tukaendelea, ikaja issue ya samwel sitta kupambana na mafisadi akataka kunyang'anywa hadi kadi ya ccm kisa anakimaliza chama baadae tunaambiwa kuna magamba ambayo kwa ukweli ndiyo sam sitta alikuwa anapambana nayo na wanatangaza hadharani kuwa wameyatosa, hapo nani alikuwa anadidimiza chama? Mbona sitta wamemwacha? Kuna issue ya zito na karamagi kusaini mkataba london na zito kusimamishwa bungeni na baadae ccm kumtosa karamagi. Ukitaka kujua ccm kiongozi wake wa juu hana msimamo angalia hili.. Alisema chadema wanaandamana ili kumwondoa madarakani baada ya muda akaanza kutekeleza madai ya cdm kwa kupita kila wizara akiwakumbusha kuwajibika na wengine hata alifikia kuwaambia wapunguze bei ya huduma zao, mfano tanesco.. Huo sio unafiki?
 
Back
Top Bottom