Siasa za Kenya na Jumuiya ya Africa Mashariki

Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
682
323
Wadau heshima mbele,
Nimekuwa nikifuatilia siku za hivi karibuni siasa za kenya, nimegundua kwamba wenzetu hawa bado wana ugonjwa mkubwa wa Ukabila. Inakusudiwa kuwa ifikapo 2015 EA takuwa imeanzisha shirikisho la kisiasa, wenzetu Kenya bado wana ugonjwa mkubwa wa Ukabila Je hatuoni kuwa watatusambazia matatizo yao ya ukabila ikiwa tutakubali political federation?GEMA, Kalenjini! unaweza kuona hapa
GEMA and Kalenjin Strategy Meeting - YouTube
 
Why are we so scared with the so called Federation? Hoja ya ukabila wa wakenya yaweza kuwa moja ya sababu za kutuzuia kuingia huko lakini what I believe is that EAC Federation shall prevail be it now or later..

Muhimu kwa upande wangu ni kujipanga na kuwekeza katika elimu na kuwa na sheria bora za kulinda ardhi na rasilimali asili tulizonazo, lakini iwapo viongozi wataendelea kuwa 'dogs in a manger' tukiingia huko itakula kwetu..

Wao wan ukabila sisi hatuna, unaonaje basi kama sisi hatuna ukabila katika kiwango chao basi huenda tukameza mapungufu yao hayo??
 
Mkuu uwezo wetu wa kuwameza ni mdogo sana kwa mtazamo wangu, jaribu kufuatilia siasa za Kenya uone jinsi jamaa wanavyojipanga na wako strategical sana, pia kiuchumi wako juu mno na kuna transparency kubwa kwenye kamati zao za Bunge na hata vyombo vya habari vinaripoti bila uoga. Pamoja na udhaifu wao mkubwa kwenye mambo ya ukabila but nadhani watatumeza vibaya mno
 
Tatizo la East Africa Federation ni moja. Wanaofanya integration ni viongozi kwa kujifungia Hilton,Kempisk, etc na kula vitumbua na chai na kujadili hiyo Federation. Lakini je mkulima wa Tandahimba anakutana na mkulima wa Meru kujadili na kufanya mipango ya pamoja ya namna ya kuinua kilimo? Tukifika hapo ndopo tutakuwa na Federationya ukweli. Hii nyingine ya viongozi ni ya kihunihuni tu. Kwa nini wanafanya federation kama vile ni project? Project ina mwanzo na mwisho, lakini kazi ya kuunganisha watu ambao wanatofauti za kisiasa na za kiuchumi na hata kifalsafa inahitaji kuwa programmatic zaidi! Mfano Kenya wametengeneza katiba mpya na wanaitekeleza sasa, na wanafanya jitihada kwelikweli. Lakini Tanzania zoezi katiba mpya limeanza kwa mizengwe, hapa wakautita ni "Constitutional Review Act" na sio "New Costitutional Act". Yaani ni uhuni tu hasa kwenye mambo ya msingi.Sasa kama jirani yako unayetaka kushiriakiana naye amefanya jambo zuri na wewe unataka kufanya jambo hiliohilo huwezi kumuuliza akakupatia uzoefu? Sasa mbona hatujawauliza wenzetu wamefanyaje kupata katiba mpya? Je kama hatuwezi kuulizana,kusaidiana na kushiriakiana kwenye mambo ya msingi kama haya tutasaidiana wapi? Sio ndio intergration yenyewe hiyo? Si ndio intergration process hiyo Tatizo la viongozi wetu ni kufikiri na kutenda kiimla na kijumla zaidi kwa sababu ya mawazo mgando. Wanataka Federation ifanyike leo au baada ya muda mfupi badala ya kuweka utaratibu ambao utazaa federation, hata kama itachukuwa miaka mia,but it has go to be done right!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom