Siasa za Igunga na vituko vya Tendwa!

waache woga; kwanini hakusema hivyo siku zote zilizopita au ndio wanatafuta kisingizio? Mbona hakuja na wazo kama hilo wakati kuna watu walikufa na kumwaga damu uchaguzi mkuu mwaka jana? Hana mpango.
 
Kuna kila dalili za uchaguzi mdogo katika jimbo la igunga kufutwa, Katika taarifa ya habari ya TBCI Msajili wa Vyama Mr.Tendwa ameonesha pendekezo la kufutwa kwa uchaguzi huo kwa kigezo kwamba watu wengi watakufa siku ya uchaguzi hivyo kufuta uchaguzi huo kutaokoa maafa. Jambo hili lina ukweli kiasi gani, mnaofuatilia uchaguzi huo kwa karibu naomba mtujuze kulikoni, nini kinaendelea huko na kama kweli hoja ya Tendwa ya kufuta uchaguzi ina msingi wowote.

Ukina manyoya ujue kaliwa.
 
Sikutarajia comment yako Mwita25! Kweli mmeshikwa pabaya, mnaombea uchaguzi ufutwe!!! Baado Kidoogo ya Zambia yanakuja.
 
Tendwa amepewa rungu, ila amepewa masharti ya kulitumia. Sharti mojawapo ni kutowatwangwa ccm kwakuwa ni ndugu.
 
Kuna kila dalili za uchaguzi mdogo katika jimbo la igunga kufutwa, Katika taarifa ya habari ya TBCI Msajili wa Vyama Mr.Tendwa ameonesha pendekezo la kufutwa kwa uchaguzi huo kwa kigezo kwamba watu wengi watakufa siku ya uchaguzi hivyo kufuta uchaguzi huo kutaokoa maafa. Jambo hili lina ukweli kiasi gani, mnaofuatilia uchaguzi huo kwa karibu naomba mtujuze kulikoni, nini kinaendelea huko na kama kweli hoja ya Tendwa ya kufuta uchaguzi ina msingi wowote.
Mkuu ccm wana hali mbaya hawakubaliki kabisa, hakuna viashiria vya maafa kama mambo yote yatafanywa kwa haki!
 
Kiashiria cha hatari ni hiki, ccm wamejipanga kushinda hata kwa hila, wamesha mwambia mkurugenzi kuwa kama hawezi tangaza ccm kuwa imeshinda hata kama haijashinda aseme mapema wa wamwamishe!
 
Inamaana Tendwa ana kikosi cha "intelijensia" kikali kuliko cha Mwema na Manumba? Wao wako wapi kuyaona hayo maafa yanakuja naTendwa ayaone! Ingawa kasema kweli hakuna polisi na serikali haipo ziko Msoga
 
Kiashiria cha hatari ni hiki, ccm wamejipanga kushinda hata kwa hila, wamesha mwambia mkurugenzi kuwa kama hawezi tangaza ccm kuwa imeshinda hata kama haijashinda aseme mapema wa wamwamishe!

Hicho ndio cha kushangaza Tendwa kuwa na intelijensia kuliko polisi,ombwe la uongozi Serikalini ni Kama pango la kambale kila mmoja ana ndevu.
 
Tarehe 3 mwezi October 2011 watanzania kuvaa nguo nyeus kulaani utendaji wa serikali kama kama unaguswa na mambo yafuatayo basi na wewe vaa na umwambie na mwenzako kama yana muhusu naye avae.
1.ukosefu wa ajira
2.kupanda kwa gharama za maisha
3.huduma mbaya za afya, elimu na maji.
4.ukosefu wa umeme
5. Ufisadi
6.mikataba mibovu
7. Ubaguzi kwenye mikopo ya elimu ya juu
8.malipo duni ya wafanyakazi wa serikali
9.ufujaji wa mali ya umma kwa watendaji wa serikali kwa safari zisizo na tija.
10. Kuwakumbatia wawekezaji katika kuiba ardhi na rasilimali ya wanyonge

Huu ni ujumbe unao zunguka kwenye Mitandao ya kijamii twitter, facebook na myspace pia sms kwa njia ya simu zimeanza kusambaaa nchi nzima.
 
tbc1 wamerusha mahojiano na mh tendwa na pia mkutano wa tume ya uchaguzi na waandishi wa habari. Ingawa habari zenyewe zimekuwa fupi fupi tu, nimemshangaa tendwa kwa kulalamikia kuwa sarakasi za kampeni na kuishia hapa kana kwamba hana lolote analoweza kufanya. Ameishia kusema kuwa angetamani uchaguzi huo ufutwe.

Tume nayo imeishia kulaani fujo zinazoendelea bila kueleza hatua watakazochukua!!

ooh kumbe yeye (tendwa) hana uwezo wa kustopisha????????????
 
TBC1 wamerusha mahojiano na Mh Tendwa na pia mkutano wa Tume ya Uchaguzi na waandishi wa habari. Ingawa habari zenyewe zimekuwa fupi fupi tu, nimemshangaa Tendwa kwa kulalamikia kuwa sarakasi za kampeni na kuishia hapa kana kwamba hana lolote analoweza kufanya. Ameishia kusema kuwa angetamani uchaguzi huo ufutwe.

Tume nayo imeishia kulaani fujo zinazoendelea bila kueleza hatua watakazochukua!!

Sasa kama wao wanaishia kulaani fujo na kutamani uchaguzi ufutwe wanataka nani achukue hizo hatua? Hawana lolote! Kwa vile wanajua mwanzishaji wa hizo fujo ni nani ndio maana wanaogopa kuchukua hatua! Sijui haya mambo ya kulindana na kupendeleana Tanzania yataisha lini. Kuna majitu yanakera sana!
 
Source TBC-1 taarifa ya habari saa 2.00kamili usiku 26-09-2011,Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa alisema hivi,"Kama ningekuwa na mamlaka kwa yanayotokea Igunga ningefuta uchaguzi ule hata sasa ninavyozungumza",akaendelea,"yanayotokea pale ni kama Polisi hakuna,Serikali haipo,kila kitu hovyo kabisa".Sasa sijui kama amejianzia au ndio wakuu wamemtupa,maana maumivu ya kichwa hawa Magamba huanza polepole!

Alinimaliza zaidi pale aliposema hata ofisi ya msajili huko ni kama haipo, hii iko chini yake kabisa, sasa nini kinachomzuia kuchukua hatua, hata kwa watu walio chini yake?
 
Habari bwana!

Nimeona nikusahihishe kwa sababu saini yako ya kudumu ni ya lugha ya kiingereza japo si kwa usahihi!

'Petty' as an adjective is neither superlative nor unique which means that you can't use definite artice 'the'. In your second phrase "...to public office"; the office is either single and unique (a'la presidential office) or they are many(plural = public offices) both of which either need or don't need a definite article 'the' consecutively. Your signature should have read as "We jail petty thieves; we put the great ones to public offices."

Haya, nishakusahihisha tayari na kama ukiuliza; ndio! Sikuwa na kazi ya kufanya ni saa 12 jioni.
 
Naona ni afadhali ufutwe tu
Hahahahahahaaaaa! teheteheteheee! kwikwikwikwikwiiiii! Mwita,mwita25,hakuna kufyata mpira kwapani,hadi 90min ziishe hapa.mmeyavulia nguo muyaoge sasa.Hali ni tete babaaaaaa!, ungekua na uhakika wa ushindi kwa CCM,usingetamani uchaguzi ufutwe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom