Siasa za CHADEMA kama za CCM

Hao vijana ndiyo balaa kwa kuporomosha "mistari" bila vina wakiulizwa kulikoni wanajitetea eti ni wapiganaji. Kwa taarifa yao wanamtandao waliomweka Kikwete madarakani mwaka 2005 ndiyo walikuwa wanajiita wapiganaji labda hili la "makamanda" ndiyo jipya.


Ni kweli kwa sababu watu wenye umri mkubwa wanajua mengi wanakumbuka tangu enzi za AMNUT mpaka Mtikila alipotuletea misamiati ya "walalahoi" na "magabachori" huku akituchombeza na kauli mbiu "Saa ya ukombozi ni sasa. tumeona mengi.



Hapo kwenye kuvumilia CDM kukosolewa ndipo udhaifu wa CDM ulipo. Zamani huko amerika ilikuwa ukitaka kumaliza mpinzani wako kisiasa unamwita Mkomunisti, basi Kwisha kazi. Hata kama jamaa alikuwa na hoja kiasi gani akishaitwa Mkomunisti inakuwa ndiyo mwisho wake kisiasa. Sasa hapa bongo tunaona watu wakiikosoa CDM basi inakuwa kama vile umeingiza mkono kwenye mzinga wa nyuki. Magamba huyo, fisadi, umetumwa, una njaa maneno mengine meengi yasiyo na maana.

kwi kwi kwi kwi kwi.Naona mada ifungwe sasa ili tujadili makundi yanayovuana nguo ndani ya Magamba.
 
Back
Top Bottom