Kwanza nashukuru ndugu yangu kwamba tumetoka kubishana hadi sasa kujadiliana, hayo ndiyo mabadiliko ya kweli na Uhuru wa Kweli ambao CHADEMA inaupigania.
Igunga hoja kubwa ilikuwa kama Igunga ni maskini au si maskini na kama ni maskini ni nani kausababisha huo umaskini. Kwa hoja hii CDM walishinda kwani wananchi wenyewe wa Igunga wanajua umaskini wao. Pia Igunga walikuwa hawawachagui hao niliowaorodhesha bali walikuwa wanataka kuchagua Kashindye mwana Igunga mwenzao na mwalimu maarufu anayefahamika na wengi.
CUF hawakuchaguliwa kwa sababu wenyewe waliwekeza kidogo kwenye upelekaji wa ujumbe wao kwa wananchi hadi wakashindwa kujitofautisha wao na CCM ambao wananchi wa Igunga walishaamini ndiyo wezi wa rasirimali zao na ndiyo waliosababisha wao wawe maskini.
Hakuna anayejua kwenye suala la kura ni za nani zilikwenda CDM. Kwa nini usifikiri kwamba za CUF zilikwenda CCM na CDM wao walichota za CCM?
Kura za CUF zilipungua kwa sababu walikuwa hawana hoja mahsusis inayokubalika kwa wananchi. Halafu kumbuka ndoa ya CCM na CUF ni mzigo unaowatesa CUF huku Tanzania Bara.
Hivi vyama vyote ulivyovitaja uwekezaje wake wa kifedha na rasirimali watu huwezi kuufananisha na CCM na CDM. CDM walikuwa na Helkopta moja wenzao wa CCM walikuwa nazo mbili. Igunga kuna kata 26 hivi vyama vingine hata magari walifanya kukodisha au walikuw nayo chakavu. kwa mantiki hiyo utaona ni kwa nini mvutano ulikuwa ni kwa CCM na CDM na CUF kwa Mbaaali.
Wabunge wa CCM na CDM walikuwa wanapishana mbugani na magari yao huku wengine wa vyama hivi hata kuzindua kampeni zao walikuwa na Horn speakers tu. heri yule wa UPDP alituburudisha kwa Mayenu.
umenijibu vema!