Siasa za CDM zimefika MWISHO, NANI ATASHIKA HATAMU?

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,904
6,904
Hbr wana Jamvi.

Nitangaze kukipenda CDM. Nilipata kadi ya CDM mwaka 2007 wakati Dr. Slaa, Prof. Baregu na wengine wengi walipofanya mdahalo ukumbi mmoja pembeni ya mliman city, eneo la survey ilikuwa 2007, Kipindi hicho nilikuwa 2nd year. Niliamua kuchukua kadi yao kwa kuwa niliamini CDM kimebeba matumaini ya watanzania. Na kwa kazi waliyoifanya kipindi kile CDM walistahili pongezi na ndo iliwafanya wafike hapo walipo leo.

Siku zote maisha ni kupanda na kushuka. Katika medani za siasa,
(i) NCCR Mageuzi ilipanda chat sana, lakini baada ya muda ikashuka 1995-2000
(ii) Kushuka kwa NCCR, kukatoa mwanya wa CUF kupanda ambapo wameshika hatamu kwa vipindi viwili mfululizo hasa kwa kuwa na idadi ya wabunge wengi. 2000-2010. Kuingia kwao kwenye makubaliano na CCM,ndo ukawa mwisho wao wa kushika hatamu kwa vyama vya upinzani Tanzania.
(iii) CHADEMA, wakatumia mwanya huo, mpaka wameshika hatamu ambayo itawafikisha 2015, lakini naamini watafika 2015 wakiwa hoi kama hawatafanya mabadiliko ya kiutendaji ndani na nje ya CHAMA. Kinachowaua ni kile kilichowaua CUF, KUINGIA MIKATABA YA KILAGHAI na CCM

Swali langu ni je, iwapo CDM ambacho kimekuwa kikitumainiwa na wananchi waliowengi, na kilikuwa mbioni kuaminiwa kupewa nchi, kama hawatabadilika na kupotosha matamko yaliyotolewa na Mnyika baada ya wao kuingia makubaliano maalum na CCM, ya kutoshiriki kwa namna yoyote ile mchakato wa kupatikana katiba mpya, na kusitisha MAANDAMANO yaliyowafikisha hapo walipo. NANI ATASHIKA HATAMU? WATANZANIA WATAMWAMINI NANIU TENA? TLP? UDP? UPDP au SAU?

Naona akilini mwangu nashuhudiwa kuwa Tanzania hakuna upinzani, bali wote wamekuwa ni vibaraka wa CCM. Mrema alianza vizuri, mwisho karudi nyumbani=CCM, Maalim Seif alipanda chat, lakini karudi CCM, CDM, wamepanda chat mwisho wake wamerudi CCM, hii ni kwa makubaliano waliyoyafanya na kisha kumtuma MNYIKA kuwa msemaji wa CHAMA.

Dr. Slaa na Zitto vipenzi wa wengi nchini na wenye ushawishi, wako wapi?

Tujadili kwa manufaa ya kukuza demokrasia nchini
 
Katika Hoja ullzozitoa mbona hakuna uwiano na Ndoa za CCM ambazo zimekuwa zikiingiwa na vyama vya upinzani??Mimi naona Chadema awaongozwi na kelele za watu bali wanaongozwa na taratibu,kanununi na katiba yao pia kwa kuheshimu sheria za nchi.
 
sawa mkuu, kutoshiriki mchakato wa katiba ni kuheshimu sheria za nchi? kutokuandamana kwa kudai kitu kinachoigusa jamii/waliowengi ni kuheshimu sheria za nchi? kuna sheria inayowakataza kutokuandamana? kuna sheria inayowakataza kushiriki mchakato wa kupatikana katiba mpya?
 
Ukiwa na negative attitude na CDM huwezi kuijadili CDM in positive attitude!

nilikuwa na ve+, kwa sasa niko dialema, nakosa nguvu za kuwaamini hasa kufuatia kitendo chao cha kuingia ikulu ambacho si shida sana, lakini kitokanacho na makubaliano ya ikulu
 
Mkuu,
Inaonekana wewe huifahamu cdm vizuri! Wamemtega JK nae akaingia kingi. Wamewathibitishia watz kwamba JK sio msikivu kama wanavyosema wapambe wake. Wame prove beyond reasonable doubt kwamba ni mnafiki mkubwa na halitakii mema taifa. Sasa kazi iliyobaki cdm ni rahisi sana. Kuwaita wananchi na kuwaeleza unafiji huu! Halafu wao wataamua hatima yao. Kimsingi cdm wamepanda chati zaidi kuliko unavyowaza!
 
Taarifa za namna hii, nazipenda, nazikubali lakini si alichokisema Mnyika, sijui alisema upuuzi ule kwa manufaa ya nani.

EasyFit said:
CHADEMA imesema licha ya Rais Jakaya Kikwete kutia saini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya mwaka 2011, itafanya kila linalowezekana kuhakikisha Tanzania inapata Katiba bora.

Matamko haya yametolewa jana na viongozi wa Chadema walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina ya siku moja ya viongozi wa chama hicho kutoka katika mikoa 26 ya Tanzania Bara.
EasyFit said:
Slaa:

"Sisi tuliomba tuonane na rais ili tumshauri aache kusaini katiba ile lakini hatuna uwezo wa kumzuia kwa kuwa katiba yenyewe inamruhusu, hivyo kama ameisaini shauri yake, sisi bado tunaendelea na msimamo wetu wa kuipinga sheria hiyo," alisema.

Alisema kuwa kitendo hicho kimeonesha kuwa Kikwete hakujali hoja za Watanzania na wadau wengine kwa ujumla. Alisema pamoja na yote yaliyotokea, CHADEMA wataendelea kupeleka maoni yao kwa ajili ya marekebisho hayo kama ambavyo walikubaliana kwa pamoja.

Zitto:

"Ni vema juhudi hizi ziendelee, tusikubali kushindwa kupata mwafaka wa kitaifa," alisema Zitto na kusisitiza; "Kwa namna yoyote ile Chadema itaendelea kuchukua hatua zote muafaka kuhakikisha Watanzania wanapata Katiba nzuri na yenye manufaa kwa taifa.

"Watanzania waelewe kwamba hakuna ushindani katika jambo hili. Tunaandaa mazingira mazuri ya kuliandaa Taifa letu liwe na demokrasia zaidi na liweze kutumia rasilimali za nchi kwa maendeleo ya Watanzania," aliongeza.

"Nimewahi kusema na ninarudia kusema tena, Katiba ya nchi inaweza kutafutwa barabarani, lakini kamwe haiandikwi barabarani. Katiba huandikwa mezani kutokana na mazungumzo yanayozaa mwafaka wa Kitaifa," alionya Zitto

Lissu:

"Ninachosema ni kuwa Rais alitukatalia mapendekezo yetu kwa sababu katika kikao kile hatukukubaliana kuwa hataisani muswada huo," alisema Lissu na kuongeza:

"Sisi tunaendelea kufanya efforts (juhudi), kuendelea kusimamia hoja zetu na tunajiandaa kupeleka hoja bungeni kubadilishwa kwa sheria hii," alisema.

"Tutawaambia wabunge waangalie maslahi ya wananchi, wapige kura kwa maslahi ya wananchi na si kwa maslahi ya chama fulani," alifafanua.
 
Wewe mwenyewe unaoneka umekata tamaa kama mtu alie katwa kichwa mbona unatanguliza kushindwa hivi wewe unaweza kujihita mwanachama wa cdm kweli acha ukumbusha tulipo anguka atutafika je ww unafanja nn bahada ya kuchukuwa kadi hii ndo umeona ni kazi ya wanacdm sio
 
Hbr wana Jamvi.

Nitangaze kukipenda CDM. Nilipata kadi ya CDM mwaka 2007 wakati Dr. Slaa, Prof. Baregu na wengine wengi walipofanya mdahalo ukumbi mmoja pembeni ya mliman city, eneo la survey ilikuwa 2007, Kipindi hicho nilikuwa 2nd year. Niliamua kuchukua kadi yao kwa kuwa niliamini CDM kimebeba matumaini ya watanzania. Na kwa kazi waliyoifanya kipindi kile CDM walistahili pongezi na ndo iliwafanya wafike hapo walipo leo.

Siku zote maisha ni kupanda na kushuka. Katika medani za siasa,
(i) NCCR Mageuzi ilipanda chat sana, lakini baada ya muda ikashuka 1995-2000
(ii) Kushuka kwa NCCR, kukatoa mwanya wa CUF kupanda ambapo wameshika hatamu kwa vipindi viwili mfululizo hasa kwa kuwa na idadi ya wabunge wengi. 2000-2010. Kuingia kwao kwenye makubaliano na CCM,ndo ukawa mwisho wao wa kushika hatamu kwa vyama vya upinzani Tanzania.
(iii) CHADEMA, wakatumia mwanya huo, mpaka wameshika hatamu ambayo itawafikisha 2015, lakini naamini watafika 2015 wakiwa hoi kama hawatafanya mabadiliko ya kiutendaji ndani na nje ya CHAMA. Kinachowaua ni kile kilichowaua CUF, KUINGIA MIKATABA YA KILAGHAI na CCM

Swali langu ni je, iwapo CDM ambacho kimekuwa kikitumainiwa na wananchi waliowengi, na kilikuwa mbioni kuaminiwa kupewa nchi, kama hawatabadilika na kupotosha matamko yaliyotolewa na Mnyika baada ya wao kuingia makubaliano maalum na CCM, ya kutoshiriki kwa namna yoyote ile mchakato wa kupatikana katiba mpya, na kusitisha MAANDAMANO yaliyowafikisha hapo walipo. NANI ATASHIKA HATAMU? WATANZANIA WATAMWAMINI NANIU TENA? TLP? UDP? UPDP au SAU?

Naona akilini mwangu nashuhudiwa kuwa Tanzania hakuna upinzani, bali wote wamekuwa ni vibaraka wa CCM. Mrema alianza vizuri, mwisho karudi nyumbani=CCM, Maalim Seif alipanda chat, lakini karudi CCM, CDM, wamepanda chat mwisho wake wamerudi CCM, hii ni kwa makubaliano waliyoyafanya na kisha kumtuma MNYIKA kuwa msemaji wa CHAMA.

Dr. Slaa na Zitto vipenzi wa wengi nchini na wenye ushawishi, wako wapi?

Tujadili kwa manufaa ya kukuza demokrasia nchini
Tujadili kitu gani? uwezo wako wakufikiri umegota kama mwenyewe ulivyo jieleza! CHADEMA ni chama kikubwa sana kwa hiyo hakiwezi kuendeshwa kwa mawazo yako mfilisi na ya kukata tamaa, sana sana unashuriwa ujitoe nauanzishe chama chako sie tuachie CHADEMA yetu. Kama unachuki binafsi na Mnyika liweke wazi tu!
 
kaka mimi naona cha mhimu si maandamano ,kwanza mazungumzo then kwa vile jk kageuka kuziwi tuombe uzima.Kama hawatarekebisha hiyo sheria aliyosaini vumbi lake kaka silipatii picha.In short always cdm are protocally.Long live CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO.
 
Mkuu,
Inaonekana wewe huifahamu cdm vizuri! Wamemtega JK nae akaingia kingi. Wamewathibitishia watz kwamba JK sio msikivu kama wanavyosema wapambe wake. Wame prove beyond reasonable doubt kwamba ni mnafiki mkubwa na halitakii mema taifa. Sasa kazi iliyobaki cdm ni rahisi sana. Kuwaita wananchi na kuwaeleza unafiji huu! Halafu wao wataamua hatima yao. Kimsingi cdm wamepanda chati zaidi kuliko unavyowaza!

rejea matamushi ya Mnyika akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya CDM. Alisema, CDM, haitoshiriki kwa namna yoyote ile, means hata kuwaita wananchi na kuwaeleza wao hawamo, hawatafanya hivyo. Lakini nimefarijika na mtamshi ya Zitto na Slaa, yanonesha matumaini siyo yale ya Munyika, MUNGIKI ndani ya chama
 
Tujadili kitu gani? uwezo wakufikiri umegota kama mwenyewe ulivyo jieleza! CHADEMA ni chama kikubwa sana kwa hiyo hkiwezi kuendeshwa kwa mawazo yako mfilisi na ya kukata tamaa, sana sana unashuriwa ujitoe nauanzishe chama chako sie tuachie CHADEMA yetu. Kama unachuki binafsi na Mnyika liweke wazi tu!

ninachuki na matamshi yake ambayo yatapelekea nimchukie. ".....CDM haitoshiriki kwa namna yoyote ile mchakato wa kupatikana katiba mpya...." J. Mnyika
 
nilikuwa na ve+, kwa sasa niko dialema, nakosa nguvu za kuwaamini hasa kufuatia kitendo chao cha kuingia ikulu ambacho si shida sana, lakini kitokanacho na makubaliano ya ikulu
Fuatiia kwa makini statement yao kabla ya kukutana ikulu walisemaje

Nadhani walienda ikulu kwa manufaa ya wananchi ili kumueleza Rais kwa nini walitoka nje ya bunge, kutoa maoni yao na misimamo yao, Nafikiri wamekubaliana mengi na hawajakubaliana mengi pia. Labda tatizo ninalo liona ni usiri uliopo ktk mazungumzo yao hili ndilo tatizo Maana hata wenzao CUF nao imekua SIRI hatujui ikulu kujadiliwa nini
 
rejea matamushi ya Mnyika akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya CDM. Alisema, CDM, haitoshiriki kwa namna yoyote ile, means hata kuwaita wananchi na kuwaeleza wao hawamo, hawatafanya hivyo. Lakini nimefarijika na mtamshi ya Zitto na Slaa, yanonesha matumaini siyo yale ya Munyika, MUNGIKI ndani ya chama
CHADEMA ni wamoja hawajagawanyika kama unavyowagawa wewe. Acha chuki zako dhidi ya mh. Mnyika.
 
No wonder Dr Slaa hakwenda ikulu alishaona choo cha stendi hicho wanaingia! CDM dead dead dead!
 
utasubiri sana tazama kwa macho utatoa majibu siku si nyingi cdm hawatumii nguvu akili kwanza then other altenative zinafuata
 
Wakianza msije sema wanahatarisha amani ya nchi......pinda rudisha 280000/yetu
 
sioni pahala CDM waliposhindwa...they are in the right track! tatizo la siasa za tanzania watu wamekuwa wakizichukulia kama mpira wa SIMBA na YANGA!
 
Unajua ni bora usijiingize kwenye uchambuzi kama una low IQ,
Ngoja nikusaidie kidogo.
Utakumbuka CDM mara baada ya kutoka bungeni iliandamwa sana kuwa ni watu wabinafsi wanaotaka kukumbati muswada wa sheria hiyo kama wao. Hoja hiyo ilipikwa na wanafiki CCM na kuishia kumshambulia Tundu Lissu badala ya katiba.
CDM kwa upole na taadhima ikaona ngoja waunde jopo kukutana na rais kumweleza ubaya wa muswada ule ili atumie akili zake achanganye na mbayuwayu asiusaini.
Habari zisizo na mawaa zinasema JK alielewa sana mabaya ya muswada ule lakini ameogopa kutousaini kwa maana kungehatarisha kibarua chake chamani!!!!
Huo ulikuwa ni mtego kwa JK, lakini vilevile kumbuka CDM walipigwa marufuku mikutano yao yote ya kisiasa.
Kwa nafasi hiyo wamepiga ndege wawili kwa jiwe moja, kuonyesha ukomavu wao wa kisiasa na kufunguliwa mikutano yao indirect.
 
Hbr wana Jamvi.

Nitangaze kukipenda CDM. Nilipata kadi ya CDM mwaka 2007 wakati Dr. Slaa, Prof. Baregu na wengine wengi walipofanya mdahalo ukumbi mmoja pembeni ya mliman city, eneo la survey ilikuwa 2007, Kipindi hicho nilikuwa 2nd year. Niliamua kuchukua kadi yao kwa kuwa niliamini CDM kimebeba matumaini ya watanzania. Na kwa kazi waliyoifanya kipindi kile CDM walistahili pongezi na ndo iliwafanya wafike hapo walipo leo.

Siku zote maisha ni kupanda na kushuka. Katika medani za siasa,
(i) NCCR Mageuzi ilipanda chat sana, lakini baada ya muda ikashuka 1995-2000
(ii) Kushuka kwa NCCR, kukatoa mwanya wa CUF kupanda ambapo wameshika hatamu kwa vipindi viwili mfululizo hasa kwa kuwa na idadi ya wabunge wengi. 2000-2010. Kuingia kwao kwenye makubaliano na CCM,ndo ukawa mwisho wao wa kushika hatamu kwa vyama vya upinzani Tanzania.
(iii) CHADEMA, wakatumia mwanya huo, mpaka wameshika hatamu ambayo itawafikisha 2015, lakini naamini watafika 2015 wakiwa hoi kama hawatafanya mabadiliko ya kiutendaji ndani na nje ya CHAMA. Kinachowaua ni kile kilichowaua CUF, KUINGIA MIKATABA YA KILAGHAI na CCM

Swali langu ni je, iwapo CDM ambacho kimekuwa kikitumainiwa na wananchi waliowengi, na kilikuwa mbioni kuaminiwa kupewa nchi, kama hawatabadilika na kupotosha matamko yaliyotolewa na Mnyika baada ya wao kuingia makubaliano maalum na CCM, ya kutoshiriki kwa namna yoyote ile mchakato wa kupatikana katiba mpya, na kusitisha MAANDAMANO yaliyowafikisha hapo walipo. NANI ATASHIKA HATAMU? WATANZANIA WATAMWAMINI NANIU TENA? TLP? UDP? UPDP au SAU?

Naona akilini mwangu nashuhudiwa kuwa Tanzania hakuna upinzani, bali wote wamekuwa ni vibaraka wa CCM. Mrema alianza vizuri, mwisho karudi nyumbani=CCM, Maalim Seif alipanda chat, lakini karudi CCM, CDM, wamepanda chat mwisho wake wamerudi CCM, hii ni kwa makubaliano waliyoyafanya na kisha kumtuma MNYIKA kuwa msemaji wa CHAMA.

Dr. Slaa na Zitto vipenzi wa wengi nchini na wenye ushawishi, wako wapi?

Tujadili kwa manufaa ya kukuza demokrasia nchini

maneno kibao lakin hamna cha msingi ulicho andika zaid ya porojo... 2nashukuru viwavi kama nyinyi hampo ndan ya chama.... Na kad ye2 uirudishe kama unayo... Kuna aina ya vijana wanaohitajika cdm, uzuri ukisha jua ufiti utajichuja mwenyewe... Ukishindwa 2nakuondoa kwa lazima..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom