Elections 2010 Siasa za Afrika na kashifa za majeshi yetu

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Kuna tabia ambayo inaanza kujengeka katika siasa za Afrika ambapo majeshi na vyombo vyetu vya usalama vinatumiwa na vyama tawala kuhakikisha kuwa vyama hivyo vinabaki madarakani, hii ni tofauti kabisa na miaka ya 60-80 ambapo majeshi yalitumika kuangusha tawala zilizokuwepo.
Kuna kitu kimoja cha muhimu kukijua na hiki ndicho nadhani watawala walijifunza baada ya mapinduzi ya kijeshi ya miaka hiyo, kitu hicho ni kuwashirikisha wakuu na watu mhimu katika majeshi katika kuchota cake ya taifa!
Kwa Tanzania kwa mfano tuhuma za majeshi yetu kuhusika na ufisadi kupitia makambuni ya Meremeta na ununuzi wa siraha ni mojawapo ya mifano ambayo nataka tuijadiri.
Baada ya viongozi au watu mhimu katika majeshi yetu kushirikishwa katika uchotaji kwenye ufisadi kama ule wa Meremeta, wamejikuta wakitumiwa kuhakikisha kuwa washirika wao wanaendelea kubaki madarakani kwa gharama yeyote, wanajua kama dola ikichukuliwa na mtawala mwingine wasiyemjua na ambaye amejipambanua kama mpinzani mkubwa wa rushwa wanalazimika kuhakikisha kwa namna yeyote ile kuwa mtu huyo hachukui dola. Wanaamini kuwa kama utawala mpya ambao unapinga rushwa utaingia madarakani watawajibishwa.
Ukiangalia yaliyojiri Zimbabwe, Kenya na sasa Tanzania utagundua kuwa vyombo vya usalama vimetumika kwa kiwango cha juu sana kuhakikisha kuwa watawala wanaowajua, waliokula nao wanabaki madarakani.
Nadhani kuna umhimu wa kujipanga upya kwa wapiganaji kama Dr Slaa na wengine kabla ya kuanza kufikiri kuna siku wataiangusha CCM, wanatakiwa wapate support kutoka kwa majeshi na wawahakikishie kuwa watasamehewa vinginevyo tusitegemee kushinda chaguzi.

Naomba kuwasilisha
 
Niaonavyo mimi siasa za Afrika bado hazitabiliki,au zimekosa pakusimamia sababu kabla ya ukoloni
Uchifu, then muda mchache kabla na baada ya uhuru vyama vingi, tukaingia uatawala wakijeshi jumlisha chama kimoja ,mwishoni mwa miaka 80 na mwanzoni mwa 90 tukarudi vyama vingi sasa hivi serikali shirikishi jumlisha ujeshi kwa mbali.
Nadhani imefika wakati Afrika kuangalia mfumo unaofaa kutuongoza kutokana na mazingira yetu yakiafrika huku elimu ya uraia ikitiliwa mkazo.
Nchi za wenzetu imechukua muda gani kufikia democrasia walionayo leo hii?, ASANTE kuweka mada hii kwani inatufungua kutafakari zaidi ya pale ulipoanzia..........nawakilisha
 
Back
Top Bottom