Siasa, Siasa, Siasa. Jamani tumechoka na threads za Siasa. Jukwaa la Siasa LIFUNGWE?

Je Jukwaa la siasa

  • Lifungwe

    Votes: 4 19.0%
  • LiSifungwe

    Votes: 14 66.7%
  • Lirekebishwe

    Votes: 3 14.3%

  • Total voters
    21
Allah's Slave ushasikia kitu..
UHURU WA MAONI?

Next time ukianzisha thread kama hii sema "nimechoka" sio "tumechoka".Shukran.
 
Kazi hipo. Watu wanauchungu si mchezo. JF ni siasa tu. Kufunga siasa ni sawa na kufunga JF. Labda sema irekebishwe.
 
Kazi hipo. Watu wanauchungu si mchezo. JF ni siasa tu. Kufunga siasa ni sawa na kufunga JF. Labda sema irekebishwe.

Hakuna kitu hapa .Irekebishwe iwe nini ? Anaweza kuanzisha blogu yake huko akafanya mabadiliko hayo huko na watu wake .
 
Nimekuwa nikifuatilia jukwaa la siasa kwa muda sasa na nimeshindwa kuvumilia. Limejaa uzushi, uongo, upuuzi na habari za kusingizia viongozi wetu. Pia nimegundua kuwa halina faida maana tunachoona hapa ni mashambulio na maelezo ya upande mmoja tu.

Kwako wewe kijana na wengine kama wewe, let me say this, enough of this nonesense, ninasema hivi kabla hujalaumu JF kwa kuwa na wapinzani wengi, hebu laumu bunge kwa kuwa na wabunge wengi wa CCM kuliko upinzani, kama kweli una huzuni kuona hapa JF wapinzani kuwa wengi kuliko CCM, nenda do something ili uli-balance bunge liwe na wabunge sawa kila upande, untill then please hebu nyamazeni na this empty argument. I do not care hapa Jf kuna wapinzani wangapi au CCM wangapi, inayosimama hapa ni hoja nzito, by the way mkuu I am CCM and I love this JF thing, kwa sababu ukweli ni ukweli, ubovu ni ubovu, na Yes chama changu kina mabovu mengi, lakini pia kina mazuri mengi sasa hii ni nafasi yangu pekee kuyasema mazuri yasiyosemwa kwa taifa, na pia kukubali mabaya ya CCM bila kinyongo, exeprience inaonyesha kuwa baadhi ya mabaya yaliyosemwa hapa yamefanyiwa kazi, kwa mfano tulisema kuhusu:-

1. Richimonduli, 2. Mama Meghji, 3. Karamagi, 4. Msabaha, 5. Mungai, 6. Ngasongwa, 7. Balali, 8. Umeme-Tanesco, 9. Lowassa, 10.Mkapa, 11. Sita-(Safari ya US wakati wa kamati ya Mwakyembe presentation).

Mkuu haya yote yamefanyiwa kazi na taifa, na chimbuko lake ni hapa JF. Mkuu mwezi huu nimeamua kuyakusanya magazeti yote ya bongo ambayo ninayo hapa, ukweli ni kwamba almost 90% ya habari zake za siasa ni za kutoka hapa JF, kumezuka waandishi wengi wa kutumia e-mail, lakini wanazitoa hapa JF, na ninaweza kukuchambulia moja baada ya nyingine, kwa hiyo mkuu hoja yako ni finyu sana on ukweli na uzito wa hoja zinazojadiliwa hapa JF. Tena unatakiwa uishukuru hii JF kwa uchambuzi makini wa habari za kila siku za siasa za taifa letu, can you imagine kusoma magazeti ya Rostam bila huu kuchambuliwa wa JF?

Mkuu wangu nafikiri unchanganywa na how demokrasia works, yes ni haki ya kila mwananchi kusema analotaka, na ndio maana tuko hapa cha muhimu ni pamoja na kuwekana sawa, si umeona jinsi hoja yako inavyochambuliwa, sasa JF tungekuwa kama unavyosema basi hoja yako ingeachwa tu na kuifunga sekta ya siasa hapa JF, hayo ni mawazo hapa JF tunaita mgando, na nafikiri wachangiaji wengi waliotangulia wamekuweka sawa kwenye hilo.

Mkuu either changia ukweli kwenye ishu unayoiona kuwa ina uongo, au changia ukweli period, otherwise, huenda hapa sio mahali pako.

Ahsante Mkuu.
 
Tukifunga Thread ya siasa,
nyingine zote zitafuata itabaki thread ya dini tu.
Huko kwenye Thread ya dini nako tutaambiwa Mungu ni mmoja na dini ni moja tu na mtume ni mmoja tu.
Kisha tutaambiwa dini ya kufuata, ukigoma shingo yako halali yao.

Thread ya siasa haifungwi ila wewe na wenzi wako ndo mtafungasha.
 
ep37_omar_bro_mouzz.jpg

Bro. Mouzone: I want to ask you a question.......... brother
Omar: No need to ask, that fool in Harlem right?
Bro. mouzone: Precisely.

ep49_crew.jpg

Marlo: Yo, count us in too. We got extra vacants.
Snoop: YERP!!!
 
Jukwaa la siasa halina faida baki ya kashfa za viongozi wetu na mimi nashauri lifungwe. Embu jiulizeni mara ya mwisho kiongozi kawekwa humu ili asifiwe ni lini?

Again, mkuu huna ukweli Rais wa jamhuri yetu alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa AU, tulimpongeza sana hapa, Rais alipomfukuza kazi Balozi Mahalu, alipongezwa sana hapa JF, alipowanyima mtandao vyeo vya CCM, tulimpongeza pia, kwa hiyo sio kweli kuwa hapa ni kupiga mawe tu, lakini hatuwezi kulazimisha kusifia uongo au matendo hewa, kama Lowassa, Karamagi, na Msabaha, wamejiuzulu kwa sababu ya kuhusika na rushwa na upotevu wa hela za sisi walipa kodi, na ripoti ipo rasmi ya bunge, ambayo mashahidi wengi walioshiriki kutoa ushahidi mbele yake walioutoa under oath, then kwa nini hawatingi mahakamani? Mbona hayo huulizi wala hayakusumbui? Mbona huulizi kwa nini Ditopile anatesa tu baada ya kuua mwananchi mlalahoi tena mbele ya wananchi walalahoi wengine kwa kutumia bastola, mbona hayo hayakuudhi? Lakini eti unaudhiwa na JF kwa kuwachambua viongozi waliomuachia huru Ditopile?

Wewe kweli ni m-Tanzania kama sisi wengine? Huna hata aibu? Exactly point yako ni nini hasa? Huchukizwi na habari kwamba Mkapa, na Yona walinunua Kiwira wakiwa madarakani tena kwa bei poa? Huchukizwi kwamba Karamagi, amepewa tenda kinyemela na Mkapa akiwa rais, kuendesha biashara ya makontena pale bandarini kwa miaka 25 ijayo bila ya kufuata utaratibu wa kisheria za taifa letu, haya hayakuuudhi ila umeudhiwa na sisi walalahoi JF kuuuliza kwa nini hatua hazichukuliwi against kina Mkapa na wenziwe?

Kuto habari za upande mmoja ni uonezi kwao. Kama jukwaa hili halifungwi lisimamishwe hadi hapo Kikwete, Lowasa, Mbowe na wengine mnaowasakama humu ndani wateue watu wa kuwawakilisha.

Mkuu aliyekuambia kuwa hao uliowataja hawapati habari zao kutoka hapa ni nani? Hebu niambie rais wetu alipokuwa akihutubia NEC iliyopita Dodoma na kulalamika kuhusu siasa za internent alikuwa anaongelea nini na yeye hajui kinachoendelea hapa JF? Hebu niambie kuacha hii JF rais alikuwa anaongelea forum ipi unayoijua inayochambua siasa zaidi ya hii? Lowassa alipokuwa akija JF kumjibu Mkulu Mwanakijiji ulikuwepo? Kama hayupo hapa alijuaje kuwa Mwanakijiji yupo hapa?

Mkuu umekurupuka, sasa labda uombe radhi kwa kutushusha hadhi forum nzima bila ya kuwa na hoja ya msingi, next time tulia kwanza mkuu kabla hujarukia hapa, pamewashinda vifaru wa siasa hapa, pamemshinda Lowassa na wafuasi wake hapa, wewe hupawezi!

Ahsante Mkuu!
 
Siasa, Siasa, Siasa. Jamani tumechoka na threads za Siasa. Jukwaa la Siasa LIFUNGWE

Nimekuwa nikifuatilia jukwaa la siasa kwa muda sasa na nimeshindwa kuvumilia. Limejaa uzushi, uongo, upuuzi na habari za kusingizia viongozi wetu. Pia nimegundua kuwa halina faida maana tunachoona hapa ni mashambulio na maelezo ya upande mmoja tu. Sidhani kama Kikwete, Lowasa, Mbowe na wengine mnaowasakama hapa watakuja kujitetea hapa. Sasa nawauliza ndugu zangu faida ya jukwaa la siasa ni nini? Hakuna elimu yeyote inayopatikana kutoka kwenye jukwaa hili. Section ya Dini/Imaan na nyinginezo ndio zibaki maana baki ya kutuelimisha ina present maelezo yaliyokuwa balanced. Wenye dini mbali mbali wanatetea wanachoamini.

294001LRTP_w.jpg
 
Nimesoma hii habari kwa masikitiko. Nahisi kuna njama na jitihada kubwa za kutaka kuisambaratisha au kupoteza mwelekeo wa JF, tangu ifunguliwe tena baada ya kufungwa kwa siku chache, kumekuwa na watu wa ajabu ajabu wakileta hoja za kutaka kuvuruga mwelekeo.

Sasa kwako ALLAH, na wenzako hapa mmepotea njia, tafuteni uwanja wenu. shughuli ndio kwanza zinaanza, mawazo yenu na hila zenu mnazoleta hapa zinaonyesha kuwa mna hila tofauti na jitihada za JF

IDUMU JF

Nawasilisha
 
Up to this stage, I think I have proved my point.Nashukuru kwa maoni yenu mengi ambayo nimeyaelewa kuhusu swala hili. What you felt about this article is exactly what I feel when people post threads\messages trying to close the Dini/Iman section. Naona wengi mme feel uchungu wa kuona mtu anataka kuondoa mnachokipenda. Mkuki kwa nguruwe enhe? Na mimi na feel hivyo hivyo.

Wengi mmejibu kwa jazba na wala hamkulijadili hili swala. Wengine mmeweka majibu mazuri sana. Nashangaa kuona wanaopost threads za kutaka kufunga section ya Dini\Iman wanashangiliwa lakini ki thread changu mimi hiki kimepigwa kibuti mpaka kwenye udaku chapchap. Kwa nini hatuwaambii wanaotaka ku close section ya dini/imani waondoke watuache kama mlivyojibu wengi hapa?

Naomba mods wawe very fair. Naomba wale wote wanaoanzisha threads za kujaribu kufunga section ya Dini/Iman wapelekewe threads zao kwenye Udaku haraka iwezekanavyo. Tena kuna moja mpaka sasa inaelea kwenye jukwaa la Dini/Imani. Ile thread ina tofauti gani na hii? Tumefikia point kuwa hatutaki kukosoana hapa JF kuhusu ujumbe wa majukwaa tofauti. If that is the case then let it be.

Ushauri kwa wale wanaoanzisha threads kutaka jukwaa la Dini/Iman lifungwe ni kama ifuatavyo. Please someni chini.

Umetukuta na umekuja na viroja na vioja ukaacha hoja naona sasa una surrender so tupo tu sisi .Endelea tuache .
JF kila siku inaibuka na vijimambo, hivi ndugu kuna mtu kakushikia bastola kwamba lazima usome haya yaliyopo kwenye thread ya DINI?

kama ufanyavyo tumekushtukia umeikuta JF tuachie ama azinzisha ya kwako DINI FORUM ushauri tu maalimu

We nani wa kutuambia nini tusome,tusisome au nini tuchangie au tusichangie!!

FUNGASHA VIRAGO..... HUJASHIKIWA KWA GUNDI HAPA JAMBO FORUM....

.Mie nimepinga mawazo yako na wengi wamekupinga ,

Shutdown

Hajazoea mambo na utamu wa uhuru uliopo hapa JF.

NI rahisi sana kwa watu kupotezwa focus... ushauri wa DrWho hapo juu ndilo pendekezo ambalo angeachiwa kulifanyia kazi.

Sasa nipingane nawe kwa nguvu zote, eti siasa zifungwe ubinafsi tupu, we si mdau wa forum ya DINI waache wadau wake.

Huyu ama ana pepo ama ni kipofu anahitaji maombi .Shetani lake likemewe maan anataka kuua roho za watanzania .

And so on.

Honestly hii response niliitegemea. Ushauri kwa wana JF wenzangu tuache kushabikia mtu akitaka jukwaa lolote lifungwe maana kuna watu wanaopenda jukwaa hilo unalochukia wewe kupita kiasi and viceversa.
 
Ulichokitaka umekipata.
Nafasi jamvini zipo jalo, tuendelee na gumzo letu la nguvu dini, siasa, udaku vyote ndani.
 
Ndiyo tatizo la mambo ya kuiga, no authenticity whatsoever; duuh..... hadi thread title mtu anageza!!

(angalia thread hii: http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=7849)

Pamoja nakuwa imitatation is the sincerest form of flattery, but one ought to be careful katika hiyo gezageza yake. Si unajua tena, wahenga wetu walishasema ukimgeza tembo k..... utaishia kupasuka msamba!

Free advice sunshine; be sincere to yourself and in doing so - it would be rather wise if you take a look before you leap!

Kuna wakati natamani kweli kutumia signature ya Invisible, ila inabidi tu kumezea ili kuepusha 'machafuko', maana ni vigumu kutabiri hatua anayoweza kuchukua mtu anayependa kugeza - mara nyingi nijuavyo, hatua hizo huwa unproportional, supererogatory na za kusikikitisha kama si kushangaza.

Allah's Slave, nimimi niliyeanzisha hiyo thread, na ingekuwa bora tu kama ungenitaja mojakwamoja. Kufananisha siasa na dini/imani ni haki yako, na sihivyo tu, bali nihaki yako pia kuandika fikra au hoja zako. Majibu kutoka kwa WanaJF umeyapata. Majibu kwenye hoja yangu ya kufunga/kurekebisha/kutofungwa bado naendelea kuyapata na kuyasikiliza.

Nakutakia mwisho wa juma mwema!

SteveD.
 
Nakupa full support. Siasa ifungwe. Nimevote Ifungwe pia. Tuko pamoja kwenye hili kama muislam mwenzangu niko na wewe.
 
Nakupa full support. Siasa ifungwe. Nimevote Ifungwe pia. Tuko pamoja kwenye hili kama muislam mwenzangu niko na wewe.
(utani)KUMBE BOEING 370 WEWE ISLAM.......AU NDO MAANA UMEEKA ALAMA YA ULIPUAJI KWENYE AVATAR YAKO?......!NA ALAMA YA KIDOLE CHA KATI JUU INAMAANA GANI KATIKA UISLAMU.....?
...AULIZAYE ANATAKA KUJUA..........!
 
Jamani achaneni na hao watoto mnabishana na watu ambao hawajui tunachangia kwa manufaa ya nani hapa ni jukwaa la kutoa hoja, maoni na dukuduku mbalimbali zinazowahusu waTanzania....so kama jukwaa la siasa (MKOMBOZI WA WANYONGE) linakukera basi kuna majukwaa mengi ingia unapotaka na tuache sisi tuendelee bwana....wasalimie waliokutuma waambie hata Manumba nae anajaribu kama wewe ila tusimama imara kama kawaida....Poleni
 
Soma maelezo sio unakurupuka tu. Jamani watanzania tukubali kukoselewa.

TATIZO MOJA KWENYE UHUSIANO NI KWAMBA... MAPENZI HAYANA FORMULA. KILA MTU ANATAKA VYAKE HAKUNA GENERAL... KWAHY HUWEZ KUSEMA NINA PREFER MIMI NA MPENZI WAKO ayapende
 
Back
Top Bottom