Siasa ni nani? - Nyakarungu

Nyakarungu

JF-Expert Member
May 1, 2011
472
375
Siasa ni jamaa mwenye tabia na zifuatazo,

...Siasa ndie kila kitu, wala TUSIPOTOSHANE kuwa siasa pekee haiwezi kuokoa nchi, siasa ndo mfumo wa kuwapata viongozi, viongozi kama Rais, rais ndiye anawateua mawaziri wote, hawa mawaziri ndio wanaotengeneza sera za nchi wakishirikiana na makatibu wao wakuu ambao nao huteuliwa na rais, rais ndo humteua katibu mkuu kiongozi, huyu katibu ndo mtendaji mkuu wa serikali (msimamizi wa watumishi wa umma) huyu ndo anawajibika kwa kila hatua ya utumishi, kuanzia ngazi ya ukatibu wa wizara, mikoa hadi wilaya...sasa wapi unaweza kuepusha siasa na ubora/ujenzi wa nchi imara?

Kumbuka kuwa mfumo mbovu wa siasa utatuletea rais mbovu, rais mbovu, atatuteulia viongozi wabovu watakaotunga sera mbovu na maisha ya watz yatakuwa mabovu, hapo hatuwezi kusema tujadili nchi au taifa letu huku tukiitenga siasa mbali, ni lazima tuhakikishe tunajenga mfumo bora utakaotuwezesha kumpata rais mwenye uwezo na dhati ya utaifa wetu... macho yetu tuyaelekeze kwenye kutoa maoni ya katiba mpya,huyu ndiye jamaa anaeitwa siasa....

Nyakarungu 2012.
 
SIASA ni dhana inayogusa nyanja zote za maisha yetu.Mtu kwa kutoelewa maana na uzito wa dhana hii aweza kutoipa uzito lakini hawezi kuepuka madhara ya kufanya hivyo...

Unapozungumzia mchakato wa ugawaji wa rasilimali kwa wananchi hapo unaikuta siasa...yaani 'who gets what,why,how and when.
Panapotokea mgongano wa kimatabaka 'class conflicts' kutokana na conflicting interests kati ya wanyonyaji na wanyonywaji, hapo nyenzo iitwayo siasa hutumika kusawazisha tofauti hizo.

Patokeapo matatizo ya kiuchumi,kama vile mfumko wa bei,ukosefu wa nishati ama curreny devaluation kama ilivyotokea Ugiriki hivi karibuni,huchukuliwa masuluhisho ya kisiasa amabayo wakati fulani hutafutwa concesus ama compromises kati ya makundi yenye itikadi, falsafa na imani tofauti.

Siasa ni kila kitu.
 
Back
Top Bottom