Siasa katika elimu yetu.

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
271
Nani alaumiwe kwa matokeo mabovu mwaka huu? Hapa nina hoja kuu tatu. 1. Serikali kuingiza siasa kwenye elimu,mfano, sera nikuwa watoto wote wanao maliza darasa la saba pia wamalize kidato cha nne. Hili limesababisha wanafunzi wengi wasio na uwezo kuwa sekondari na kuwapa wakati mgumu walimu wetu. Serikali kufuta mchujo wa kidato cha pili pia imesababisha wale wasio na uwezo kufika kidato cha nne na mwisho wanafunzi hawa kupata sifuri. Hizo ndio siasa za tutahakikisha watoto wote wanapata elimu ya sekondari. 2. Serikali kuandaa walimu wa muda mfupi maarufu kama vodafasta pia nitatizo kwani walimu hawa wanakosa maadili na mbinu za kukabiliana na wanafunzi wazito kuelewa. Walimu hawa wa muda mfupi wengi wao wameathirika na utandawazi kwa kiasi kikubwa na hawana maadili ya kiualimu hivyo wanafunzi kukosa kuwaamini walimu hawa ambao pia ni kiigizo kwa wanafunzi na jamii. Kiukweli walimu hawa wanalalamikiwa sana na jamii hasa vijijini. 3. Wanafunzi wameathiriwa kwa kiasi kikubwa sana na utandawazi,wengi hupenda maisha ya mafanikio kwa mkato pasipo kujitahidi katika masomo.Mfano wanafunzi wengi wanapenda kuwa wasanii wa bongoflava,kuvuta bangi na madawa ya kulevya. Tatizo kubwa ni mapenzi shuleni kwa wanafunzi, mfano kidato chapili hadi channe utakuta wanafunzi wamegawana wapenzi shuleni yani kila mtu na wake. Pia baadhi ya walimu kujiingiza katika mapenzi na wanafunzi,utasikia mwalimu anaitwa shemeji! Wanafunzi hapa nidhamu ndio hakuna tena. Na kwa mawazo ya ngono na kuandikiana jumbe fupi kwenye simu wanafunzi hawa watamsikiliza mwalimu? Wanafunzi hawa wanamuda wa kujisomea? Watavuna nini mwisho wa safari kwa tabia hizi? Mi nadhani hatupaswi kulaumu Necta bali kwanza wanafunzi wenyewe kisha serikali na sera zake juu ya elimu ya sekondari.
 
Lakini pia walimu kukosa mtaala wa kufundishia nalo ni tatizo hasa ktk shule zetu za kata. Mfano, unaweza kukuta shule X wanatumia kitabu A kufundishia mathalan somo la Geography lakini ukienda shule Y unakuta kitabu kinachotumika ni B. Mfano ulio hai ni huu hapa. Mwezi mei 2010 nilikuwa naongea na mwl flani hivi kuhusu elimu yetu. Basi yule mama mwalimu akanieleza kuwa anashindwa kujua maana kila anapoongea na walimu wenzake wanamueleza kuwa riwaya za No longer at ease, things fall apart na the river between vimefutwa. Wakati wenzake hawavitumii, yeye alikuwa bado anaendelea kuwafundishia wanafunzi wake. Nikamuuliza mtaala unasemaje, akaniambia kuwa hajawahi kuuona mtaala shuleni kwake na hivyo anatumia uzoefu tu. sababu ni nyingi sana.
 
Back
Top Bottom