siasa inapochanganywa kwenye sheria!!

Ms Judith

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
2,563
918
Dereva wa DC Mwanga matatani Send to a friend
Sunday, 04 March 2012 13:02
0digg
Na Daniel Mjema, Moshi
DEREVA wa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, ameingia matatani baada ya kudaiwa kukiri kumpa mimba mtoto wa bosi wake huyo.Taarifa za dereva huyo (jina tunalo) kumjaza mimba mtoto wa bosi wake ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu, zimezua gumzo katika ofisi za serikali.

Habari zilizolifikia Mwananchi Jumapili, zilidai kutokana na uzito wa tuhuma hizo, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ilikutana kujadili suala hilo.

Mkuu huyo wa Wilaya, Athman Mdoe ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo, alilifikisha suala hilo mbele ya kamati hiyo akimlalamikia dereva wake huyo.

“Baada ya kamati ya ulinzi na usalama kujadili jambo hilo kama siku nne hivi zimepita iliamuliwa suala hilo lipelekwe ngazi za juu kimkoa,”kilidai chanzo hicho.

Chanzo hicho kilieleza kuwa baada ya dereva huyo kuitwa mbele ya kikao hicho na kuhojiwa inadaiwa alikiri kumpa mimba mwanafunzi huyo.

“Baadaye alitakiwa kuandika barua ya kujieleza ambapo pia alikiri kwa maandishi kumpa mimba mtoto wa bosi wake huyo,”alieleza afisa mmoja wa serikali.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa wilaya alikaririwa akisema amemsamehe dereva huyo, lakini anaviachia vyombo vya dola na kiserikali kuchukua hatua stahili.

Taarifa zaidi zilieleza kwamba, Kamati ya ulinzi na Usalama ilimwagiza Katibu Tawala wa Wilaya hiyo (DAS), Zuhura Chikira, kupeleka mashitaka ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro (RAS) ambayo inashikiliwa na Hassan Bendeyeko.

Taarifa kutoka ndani ya ofisi ya RAS zilipasha kuwa suala hilo lilijadiliwa juzi na Ijumaa na iliamuliwa dereva huyo aandikiwe barua ya kusimamishwa kazi.

Mahusiano yao yalivyoanza
Habari zinadai dereva huyo alianza mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi huyo kwa muda mrefu baada ya kuzoeana naye kila anapompeleka shule.

“Unajua huyo dereva ndiye alikuwa anatumwa mara kwa mara kumpeleke shule, wakati mwingine alikuwa anatumwa mpaka kwenda kumlipia ada, kwa hiyo ni kweli kuwa alikuwa karibu na huyo mtoto,”ilidaiwa.

Ilielezwa kuwa baada ya mwanafunzi huyo kugundulika ni mjamzito, dereva huyo alijitahidi kumshawishi aitoe mimba hiyo, lakini mtoto huyo alikataa katakata.

Baada ya wazazi wa mwanafunzi huyo kumbana mtoto wao, ndipo alipomtaja dereva huyo kuwa ndiye mhusika.

Msimamo wa sheria
Kwa mujibu kifungu namba 78 cha sheria ya elimu namba 25 ya mwaka 1978 kama ilivyotangazwa katika gazeti la serikali namba 265 la 2003, ni mkosa la kisheria kumpa mimba mwanafunzi.

RPC Kilimanjaro anena
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma alipoulizwa jana alionyesha kustushwa na jambo hilo, lakini akasema bado halijamfikia.

“Mbona hiyo ni balaa, mimba kabisa mtoto wa bosi wake?”alihoji Mwakyoma na kusema inaonekana labda jambo hilo halijaripotiwa polisi wilayani Mwanga.

Hata hivyo, alisema atafuatilia suala hilo kwa kuwa kumpa mimba mwanafunzi ni kosa kisheria na hakuna mtu anayeweza kukwepa mkono wa sheria.

DC Mwanga
Akizungumza na Mwananchi Jumapili mzazi wa mtoto huyo, Athumani Mdoe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa madereva hawawajibiki kwake.

Pia alivyotakiwa kuzungumzia suala hilo kwa upande wa kifamilia kwa kuwa aliyepewa mimba ni mtoto wake, alisema suala hilo ni la kifamilia na linaendelea kufanyiwa uchunguzi katika ngazi ya kifamilia.

''Hizo habari nani kawaeleza na mnachotaka haswa ni kipi…, hili ni suala la kifamilia siyo la umma na mambo ya familia yangu ni yangu binafsi,'' alisema Mdoe.

Alieza pia kuwa kutokana na suala hilo kuwa la kifamilia hawezi kulifafanua zaidi kwa umma.

mtazamo binafsi

haikuwa sahihi kwa baba mzazi ambaye pia ni mkuu wa wilaya na mwenyekiti wa kamati ya ulizi na usalama ya wilaya ku-channel hiyo kesi kupitia kamati yake amabayo yeye mwenyewe ndiye mwenyekiti wake. hatua hiyo si ya kisheria na pia si sahihi. nakubaliana na maoni ya baba mzazi kuwa japo ni masuala ya kisheria, ila pia ni mambo binafsi ya familia yake. ila hilo lisizuie sheria kuchukua mkondo wake!

mbarikiwe sana wapendwa,

Glory to God!

chanzo:
Dereva wa DC Mwanga matatani
 
Back
Top Bottom