Siamini kama report ya GAG ni sahihi

trplmike

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
701
775
Ndugu zangu, utendaji wa mashirika au taasisi za serikali tunazifahamu, mimi mpaka leo siamini kabisa kama report ya CAG ni sahihi, ninaamini imechakachuliwa mpaka mwisho,
Huyu Utoah ndiye aliemsafisha kiongozi fulani kuwa hahusiki na skendo fulani bungeni! Mnakumbuka issue ya Jairo?
Ili sisi watanzania tujiridhishe na report ya CAG tunaomba halmashauri moja tuu wapewe PWC au Erinest& Young au kampuni yeyote ya kimataifa inayofanya Audit ndipo utakapojua uozo uliojaa kwenye halmashauri zetu
 
Ni kweli, ripoti za CAG zitakua na mapungufu mengi kwa kuwa zitakua zimeficha uozo mkubwa zaidi ambao ungeweza kugunduliwa na wataalamu wengine ambao ni INDEPENDENT. Ni suala ambalo liko wazi kuwa wakaguzi ambao wapo chini ya CAG ni wala rushwa wakubwa na ndio wanaosababisha uozo mwingi ushindwe kugunduliwa. Mfano mzuri ni wilaya ya Tunduru ambayo iko katika mkoa wa Ruvuma ina 'opinion' nzuri wakati inafahamika kuwa ni wilaya isiyo na wenyewe kutokana na kuliwa. Hii ni kwa sababu madiwani karibu wote ni wale wa CCM tena ambao wameishia darasa la 7 na hivyo kutokua na uelewa wowote wakiutaalamu wa namna mambo mbalimbali yanavyoenda katika wilaya hiyo.
 
tayari CAG alishafanya special audit kishapu na kuibua mengi. kuhusu jairo CAG alipewa specific terms of reference. majibu yake yalikuwa ni kwa specific querries alizoombwa afatilie.

Ndugu zangu, utendaji wa
mashirika au taasisi za serikali tunazifahamu, mimi mpaka leo siamini
kabisa kama report ya CAG ni sahihi, ninaamini imechakachuliwa mpaka
mwisho,
Huyu Utoah ndiye aliemsafisha kiongozi fulani kuwa hahusiki na
skendo fulani bungeni! Mnakumbuka issue ya Jairo?
Ili sisi watanzania tujiridhishe na report ya CAG tunaomba halmashauri
moja tuu wapewe PWC au Erinest& Young au kampuni yeyote ya kimataifa
inayofanya Audit ndipo utakapojua uozo uliojaa kwenye halmashauri
zetu
 
cag ripoti zake ni nzuri ila kuna watu walitaka kumtumia kisiasa ili wasafishike kuhusu ripoti ya Jairo aliagizwa kukagua sehemu tu ya mambo badala ya kupewa utaratibu wa kuwa huru tofauti na kamati ya bunge ndio maana alisema kuanzia muda huo hatarudia kufanya ukaguzi kama huo kama unakumbuka kuhusu ukaguzi wa UDA aliagiza ukaguzi huu ufanywe na Price Water Cooper kwa sababu waliuleta kwa misingi hiyo hiyo CAG ni mhasibu mwandamizi ambaye anabanwa kimaadili hawezi kupika ripoti na siyo wilaya zote zilikaguliwa Tanzania walichukua baadhi
 
Huwezi kufananisha Ernst & Young au PWC na ofisi ya CAG!

Tukirejea swala la Jairo Utouh alifanya kazi ambayo bunge lilielekeza na hakukosea!
 
Hiyo heading vp? Labda tuchangie kwa mazoea maana ushachanganya
 
Hivi CAG anaendaga mpaka ikulu kuangalizia matumizi ya pesa za walipa kodi zinazotumika ikulu? hawa mawaziri ofisi ya rais na watendaji wengine katika ofisi ya Rais or Ikulu mbona hatupewi report yake au hawaruhusiwi kufika mpaka jumba kuu
 
Nafikiri una hoja, nzuri tu.

Kuwa ripoti ya CAG haijakamilika na pengine inakosa hadhi fulani. Lakini ili hilo litokee ni vizuri ungeainisha huo upungufu na kuweka ushahidi (wa kimaandishi), i.e. funua yaliyofichwa.

Mpaka hapo utakapofanya hivyo; hii ripoti ya CAG ndio nyenzo pekee tulonayo na madai yako yataonekana ni uzushi.
 
Back
Top Bottom