Kipilipili
JF-Expert Member
- May 25, 2010
- 2,272
- 1,880
Neno kuoana lipo katika kauli ya kutendana,hivyo tunenapo kuwa"wameoana jana"si sahihi kwani mke haoi bali anaolewa,na mume ndo anaoa.
Lugha ni sauti za nasibu zinazozuka kibahati bahati tu na kutumika kwenye jamii bila makubaliano maalum..Hakuna fomula inayohakikisha kwamba tendo la "kuoa" lina uhusiano wa moja kwa moja na tendo la mwanamume kumtwaa na kummiliki mwanamke.Mimi naweza kusema hivi, kuoana ni kufanana tabia au sifa fulani fulani na bado nikawa sahihi vilevile, mfano nikisema,tabia za alex na musa zinaoana(zinafanana), au nikisema magari haya yanaoana(yanafanana)..je na hapa utasema nimekosea?Neno kuoana lipo katika kauli ya kutendana,hivyo tunenapo kuwa"wameoana jana"si sahihi kwani mke haoi bali anaolewa,na mume ndo anaoa.
Swadakta senior bachelor,ulisemalo ni zaidi ya sahihi.ila kaka katika kudumisha lugha yetu adhimu unaonaje kama hilo jina lako likawa kwa kiswahili mf.MSEJA MWANDAMIZI badala ya senior bachelor?