Si madaktari pekee

Shansila

Senior Member
Jan 28, 2012
189
36
Hakuna ubishi kuwa madai ya madaktari ni ya msingi na yanayohitaji mrejeo wa haraka toka serikalini ili kunusuru maisha ya wagonjwa masikini.Ingawa haiwezekani wakagoma wote kwa sababu ya tofauti za kimaslahi,lakini hii iwe kengele ya kuiamsha serikali toka usingizini kuwa maslahi ya watumishi wa sekta za umma na binafsi yanapaswa kuboreshwa ili kuendana na mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha.Aidha mfumuko wa bei unatakiwa kudhibitiwa kwa nguvu.Kupuuza hili ni kualika migomo zaidi kuanzia kwa watumishi wa umma,sekta binafsi na hata wananchi kwa ujumla na yaweza kuwa vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa.Kisingizio cha kudai serikali haina fedha hakina mashiko,kwani tunaona jinsi fedha zinavyotumika vibaya!Amka Tza.
 
Back
Top Bottom