Si kweli? Watanzania wachambwa: Kiingereza, Wizi, Viongozi kujipendelea...

nimeshakutana na wachina bongo wanaongea kiswahili kizuri kuliko wanavyoongea kiingereza...sikuamini maskio yangu nilivyowasikia siku hiyo

Kiswahili kimejengwa kwa logic kubwa kuliko Kiingereza, angalia rules na exceptions tu katika lugha zote.

Ni rahisi kwa mchina kujifunza Kiswahili kuliko Kiingereza, kwa sababu Kiingereza kimekaa arbitrary zaidi.

Na kama unaona navutia lugha ya nyumbani kwangu msome George Bernard Shaw on the subject.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Anza kwa kuacha kutumia maandishi ya Kirumi basi, anzisha maandishi ya Kiswahili, uende kuanzisha na internet ya Kiswahili etc.

Utopia is good only in the abstract. Try to live it and you will see how quixotic shunning english is.

Ingawa sikubali utumwa wa mawazo, pia sikubali kwamba inabidi tuwe isolationists ili kuushinda utumwa wa mawazo.

Ikumbukwe kwamba hawa wanaoongoza chumi za dunia hivi sasa hawajafika hapo kwa kujifungia. Na kwa kweli Mchina bila kujifungia angekuwa mbali zaidi sasa hivi.

Pamoja na kukubaliana na hii argument lakini si wakati wote kujifungia kuna tatizo...Tunatakiwa kufanya transfer of technologies lakini pia kumbuka usipoweka mipaka ya kuingia na kutoka hawa weupe hawatakubali kukuacha ukaendelea bila kuingiza virusi kuchafua damu ya maendeleo yako..Hope you read my mind!
 
Wewe kwa kutumia teknolojia za watu huonyeshi kujifungia.

Practice what you preach.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kila mtu na mtazamo wake, kwangu mimi kuambiwa kuwa hatujui kingereza huku akikili kuwa tumebobea kwenye kiswahili ni sifa nzuri. kama ilivyo kwake na wazungu wenzake hawajui kiswahili huku wakiwa wamebobea ktk kingereza. Ujinga wetu uko namna hii : mwingereza akiongea kiswahili akachanganya nyakati , viunganishi vibovu na hata matamshi mabaya yenye kupoteza radha ya kiswahli, wa Tz tunamsifu kwa kusema kajitahidi maana kaeleweka. Lakini acha mTz aongee kingereza kwa kuchanganya tenses, kushindwa matamshi, na hata kutumia neno la kingereza mahala pasipo pake, utasikia taanguka na vicheko, kejeli na kusema anatuaibisha hata kama kaeleweka. HUO NI UTUMWA WA FIKRA

Hili la luga hata mimi halinipi shida kwani kama mtu anaweza ku-communicate inatosha sihitaji kujua luga ya watu kwa level yake kama ndivyo hata yy ajifunze ya kwangu ili awe comfortable..Lakini kwenye hii tube kuna vitu vya msingi kama tabia ya udokozi...Hii sifa hata ss tuna lalamikia sasa mambo ya EPA etc na inaondoa uaminifu wetu mbele ya mataifa kwani wote tunajulikana kama mishe mishe...Mfano hata mm nikutana na m-nija nakuwa makini maana najua saa yoyote ile anaweza niingiza mjini...Lakini si kweli huko kwao hakuna watu honest na rebutable ila kwa ujumla wao hiyo ndiyo tabia kuu..Sisi kwa huku nje tunakuwa grouped pamoja na hao matapeli wetu maarufu barani bila kutofautishwa lakini mtu anayetaka kujaribu kuwa objective anashindwa kuondoa hiyo dhana kama hata na viongozi wetu wanakiri hadharani ss ndivyo tulivyo kwa matendo na maneno yao..

Inabidi kujenga taswira fulani kama Taifa..Mfano si kweli wakati wa Julias wote tulikuwa smart lakini alitubeba wote tukaonekana watu wenye hadhi na heshima zetu
 
Nimemsikiliza huyo mama lakini sijaona kama amekusea sana kwa vile anavyojieleza,ni kweli wakenya wanajua kuongea kiingereza kuliko watanzania na pengine pia watanzania wanajua kiswahili kuliko wakenya,sijaona ubaya wowote, na kwa sisi tunaokaa hapa arusha pia tunaliona hilo,hata kwenye interview mbali mbali wanafeli pia,amesema kuna waizi wa maji lkn mi nilivyomuelewa ni kweli kuna waizi wa vitu vidogo vidogo kama maji,soda,kuku,hela mfukoni,kamera,simu,chakula hawlipi sometime(ndio maana wakati mwingine wezi wanachomwa si kwamba wameiba kitu cha gharama)Pia katika tanzania kuna mikoa imeizidi mikoa mingine kwa mfano Arusha wanaongea kiingereza na kutumia internet kuliko mikoa mingine hii ni kutokana na kazi zao nyingi kuhusisha wageni/watalii.
Please note:hamaanishi kuwa hakuna wasiojua kiingereza vizuri,ila idadi ya wanaojua na wasiojua wasiojua ni wengi,kwa mfano watumiaji wa jamii forum wengi wanajua,lakini wakazi wa jimbo wanalotoka raisi hawajui,by the way kiingereza inaweza ikawa ni mojawapo wa tatizo kwa watanzania na wana riadha kwa ujumla mi sidhani ni tatizo,tatizo ni mfumo wa utawala ambao haujali maslahi ya wengi.

Hivi wajapan, wachina, warusi, waarabu, wabelgiji, wafaransa, na wa-filipino wote wanaongea kiingereza kama muingereza au mmarekani?
Ishu ya kuongea kiingereza kama wakenya sioni kama ina pointi hapa, kama mkizungumzia kuhusu uwezo wa mtu kiakili katika kudadavua mambo kuwa una walakini naweza kuelewa lakini swala la lugha mimi sioni kama ni tatizo.

Mimi nimewahi kufanya kazi na waarabu, wafaransa, wajerumani na wafilipino, kiingereza kilikuwa kinawapa tabu usipime lakini uwezo wao kiutendaji ulikuwa juu...............

Mbona tunajidharau kiasi hiki jamani.Kiingereza sio lugha yetu, tukubali hilo, na kama swala ni kufanya presentation kwenye mikutano mikubwa ya kimataifa, tuna uwezo wa kuchagua lugha ya kiswahili na tunasongesha vile vile na ndio maana kuna ma-interpreter.......

Kwakweli sijui tufanyeje kwani hata mimi wiki jana nimesononeka sana baada ya kushindwa kuaminiwa kuwa nasema ukweli kwakua tu ni mwafirca-mtanzania..Ilibidi waniombe radhi wakafanye utafiti kidogo kujua who is right kati yangu mimi niliye waambia ukweli wangu na huyo mwingine aliyeamua kupinga kwasababu tu ya pre-conceived mind kwamba wengi wetu waongo na hatuko honest...

It pained me a lot kwani kwa muda mrefu nimekuwa katika hiyo situation ya kutokuwa fully trusted (japo naona wananipa benefit of doubt lakini hawamini kama naweza fanya jambo mwenyewe bila unagalizi wa karibu) nami nimejitahidi kwa nguvu na uwezo kutokufanya hata kitu kimoja kuhalalisha mawazo yao hivyo nimekuwa makini kwa kila usemi tendo hata wakati mwingine kukwepa baadhi ya malumbano ili nisije tia neno kwa hisia nika-justfy hisia mbaya iliyo juu ya watu wa jamii yangu (waafrica na hasa watanzania) kutokana na mawazo yaliyomo ndani ya hawa ninao ishi nao kwa muda...

Huwezi amini it took something like a week kuamuliwa kwa jambo ambalo lingetakiwa kuwa la dakika mpaka walipothibitisha ndiyo wakanipa go ahead....Najiuliza kama kusingekuwa na evidence kwenye authentic sources ingekuwaje?

Siwalaumu hawa kwa hisia zao kwani pia kuna mambo ambayo kama nchi tumeshindwa kuyasimamia na hivyo kutoa mwanya wa sisi kutoaminika..Ni juzi hapa jf kulikuwa na andiko lenye neno 'a country with high rent seeking behaviour...' Hivi sijui kama watu wanalielewa hili neno kwa usahihi wake...Kwa wachumi inamaana watu wanaopenda malipo wasiyostahili..Ama hata kupenda vya chee...Its very bad kwakweli ebu tufikie wakati tukataye huu ujinga na tusimame kama jamii kuwapinga wote wanaotuchafulia jina la taifa letu...

Nakubaliana na hapo kwenye red, haswa kwa wanasiasa wetu (wabunge, na viongozi wa nyanja mbalimbali, jumuisha mawaziri, mpaka wakuu kabisa) hawa wanakula malipo wasiyostahili, na wanayapigania haswa. Hawafanyi kazi kulingana na malipo yao.
 
No Comment... KIKULACHO ki NGUONI MWAKO!!!

Mkuu rekebisha kidogo pale juu kwenye post yako, anasema tulifanya kosa kubwa kuchagua KISWAHILI kama lugha ya taifa baada ya uhuru tofauti na kenya waliochagua KIINGEREZA
 
Kila mtu na mtazamo wake, kwangu mimi kuambiwa kuwa hatujui kingereza huku akikili kuwa tumebobea kwenye kiswahili ni sifa nzuri. kama ilivyo kwake na wazungu wenzake hawajui kiswahili huku wakiwa wamebobea ktk kingereza. Ujinga wetu uko namna hii : mwingereza akiongea kiswahili akachanganya nyakati , viunganishi vibovu na hata matamshi mabaya yenye kupoteza radha ya kiswahli, wa Tz tunamsifu kwa kusema kajitahidi maana kaeleweka. Lakini acha mTz aongee kingereza kwa kuchanganya tenses, kushindwa matamshi, na hata kutumia neno la kingereza mahala pasipo pake, utasikia taanguka na vicheko, kejeli na kusema anatuaibisha hata kama kaeleweka. HUO NI UTUMWA WA FIKRA
kweli mkuu ?
Ila sasa isiwe kama ile ya pemba na zimbabwe.
 
Umesema kweli. Wakorea, wafaransa, wareno, waarabu, wajapani na wengine wengi hawana issue na kiingereza na mambo yanaenda

Chunguza zaidi, huko kote Kiingereza ni nambari wani bila hivyo mambo yasingeenda. Ili mradi kila utakacho kipo kwa Kiingereza, huna kwa kukimbilia kwingine.

Tatizo hapa CCM imeondoa nidhamu ya kila kitu. TZ hakuna nidhamu hata iwe kwa kutumia Kiswahili ama Kiingereza, ama kikabila, hata viongozi wetu (pamoja na Raisi) ambao ndio mfano wetu utaona wanavyochekacheka tu kuashiria kua wao wanajua zaidi kuliko watu wengine ama kua sisi TZ tunajua zaidi kuliko watu wengine Duniani - kumbe ni OMBAOMBA tu.
 
Mimi kwa sasa naishi hapa Vienna Austria, kingereza wala sio issue hapa ni kijerumani, na hawa watu wanapenda lugha yao. Lugha ambayo ninaweza kujivuni mbele ya hawa watu ni Kiswahili tu na sio lugha nyingine, na mpaka sasa nimekwisha pata mwanafunzi mmoja ambaye anapenda kujifunza Kiswahili. Hii imemvutia kwa jinsi ninavyoipenda lugha yangu na kumwambia kuwa ndiyo lugha pekee ambayo inaweza kulitambulisha bara la Afrika ambapo makabila mengi yanaasili ya lugha ya kibantu. Ninapokosea kuongea kiingereza sioni aibu kwani sio lugha yangu ila nikiongea kiswahili kwa makosa hapa ni lazima nione aibu kwasababu ni lugha yangu. Kama wao wanavyokosea kuongea kiswahili na siwashangai kwa kuwa sio lugha yao nami pia wasinishangae ninapokosea kuongea kiingereza kwani sio lugha yangu, nimejifunza tu darasani. TUIPENDE LUGHA YETU NA TUIONEE FAHARI POPOTE PALE.
 
Tunahitaji kuongeza juhudi za makusudi kuimarisha kiingereza kwani kujua lugha zaidi ya moja ni faida kubwa kwa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla. Kiswahili ni kwa ajili yetu sisi (tz) lakini ukitoka nje na hata mawasiliano mengi ya kiuchumi na mambo ya kigeni tunahitaji ku-improve kiingereza.

Hata hicho kiswahili ni cha mtaani tu sio cha kusomea kwani ukiangalia idadi ya watz walioajiriwa BBC swahili service wengi ni wakenya. Hata ma-lecturer wengi wa kiswahili Amerika/ Uingereza sio wa-tz. We need really to pull up our socks na kuacha porojo za siasa. Vigogo wengi watoto wao wanasoma nje au international schools/academy na ndio wenye kazi nzuri. We have to look back we walalahoi.
 
Mkuu rekebisha kidogo pale juu kwenye post yako, anasema tulifanya kosa kubwa kuchagua KISWAHILI kama lugha ya taifa baada ya uhuru tofauti na kenya waliochagua KIINGEREZA

Asante nikerekebisha kuwa KISWAHILI...

Huyu Mama hajui MANUFAA tuliyonayo kwa kuongea KISWAHILI; Haya pamoja ya kuwa tunalipua wakati wa kuomba viza Lakini wanazitoa hizo VISA; Sio Nchi zote zinazoomba VISA nchi za KIINGEREZa zinaongoa ENGLISh mfano CHINA inaongoza kwa kupata VISA nchi zinazoongea KIINGEREZA; Ina Maana Wanaongea kiingereza???

Kama amachoka AVUKE MPAKA TULIZANE KENYA
 
Tunahitaji kuongeza juhudi za makusudi kuimarisha kiingereza kwani kujua lugha zaidi ya moja ni faida kubwa kwa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla. Kiswahili ni kwa ajili yetu sisi (tz) lakini ukitoka nje na hata mawasiliano mengi ya kiuchumi na mambo ya kigeni tunahitaji ku-improve kiingereza.

Hata hicho kiswahili ni cha mtaani tu sio cha kusomea kwani ukiangalia idadi ya watz walioajiriwa BBC swahili service wengi ni wakenya. Hata ma-lecturer wengi wa kiswahili Amerika/ Uingereza sio wa-tz. We need really to pull up our socks na kuacha porojo za siasa. Vigogo wengi watoto wao wanasoma nje au international schools/academy na ndio wenye kazi nzuri. We have to look back we walalahoi.
asikudanganye mtu eti ajira za kiswahili ni kipimo cha ubora katika lugha hii, lahasha. Wewe hujaona kila mahali duniani watu wasio na sifa wakipata ajira huku wenye sifa wakiachwa kando? bado nasisitiza kuwa ni ubovu wa fikra. umesha jiuliza kwa nini sisi tunahangaika kujifunza lugha zao ili tukienda kwao tusisumbuke na kwa nini wao wasijifunze yetu ili wakija kwetu wasisumbuke?
 
Hili la luga hata mimi halinipi shida kwani kama mtu anaweza ku-communicate inatosha sihitaji kujua luga ya watu kwa level yake kama ndivyo hata yy ajifunze ya kwangu ili awe comfortable..Lakini kwenye hii tube kuna vitu vya msingi kama tabia ya udokozi...Hii sifa hata ss tuna lalamikia sasa mambo ya EPA etc na inaondoa uaminifu wetu mbele ya mataifa kwani wote tunajulikana kama mishe mishe...Mfano hata mm nikutana na m-nija nakuwa makini maana najua saa yoyote ile anaweza niingiza mjini...Lakini si kweli huko kwao hakuna watu honest na rebutable ila kwa ujumla wao hiyo ndiyo tabia kuu..Sisi kwa huku nje tunakuwa grouped pamoja na hao matapeli wetu maarufu barani bila kutofautishwa lakini mtu anayetaka kujaribu kuwa objective anashindwa kuondoa hiyo dhana kama hata na viongozi wetu wanakiri hadharani ss ndivyo tulivyo kwa matendo na maneno yao..

Inabidi kujenga taswira fulani kama Taifa..Mfano si kweli wakati wa Julias wote tulikuwa smart lakini alitubeba wote tukaonekana watu wenye hadhi na heshima zetu

La udokozi na mimi naungana nalo bila wasiwasi lipo tena linatia dosari shughuli za utalii sana. Mfano mimi nikiwa Arusha mjini nimeshuhudia mara kwa mara watalii wakinyang'anywa vitu vyao mchana kweupe wakiwa katika kutalii hapa na pale katika mitaa ya mji. Hii ilipelekea mpaka kutangazwa kwenye mtandao wa google kupitia gruop moja maarufu kwa kutoa mambo yanayojiri hapa arusha ijulikanayo kama arusha mailing group. Watalii walitahadharishwa kutembea kimakundi na kwamba wakiwa matembezini wakiona kundi la vijana mbele yao walikwepe kwa namna yoyote ile. Sasa hiii si ni aibu kubwa jamani.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mjinga sana huyo mama Mary, nimeiona hiyo clip ya Youtube.
Tatizo wzungu wajinga wajinga wakija Afrika wana mentality ya watu wote kuwa ni mazezeta wa kudoea mlo wa mchana.
 
Uingereza ipi hiyo iliyo hoi kimaendeleo?

Hiihii unayoijua ww, usiangalie maendeleo waloyapata zamani, ss hivi hali yao unaijua vizuri? Ht ss tunasema tanzania ilikuwa na maendeleo zamanikuliko ss, wapo wanaosema kwa kuangalia ppp, thamani ya dola kwa shs, viwanda vilivyokuwepo zamani, social services zilizotolewa na serikali free
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwa maisha ya sasa mtu unataliwa ujue japo lugha nee za kimataifa kiuafasaha sio kiingereza tu, Japo twaweza endelea bilaenglish mfano china na japan
 
Unaweza kusema hivi kama una mitaala yako ya maana ya Kiswahili, vitabu vyako, viwanda vyako, watu wa nje wanatafsiri vitabu vyao kwenda kiswahili kwa wingi etc.

Leo hii hutengenezi hata pini unataka kujilinganisha na China?

Mchina anaweza kuingia kwenye internet akafanya kila kitu kwa kichina.

Wewe kutengeneza computer ya Kiswahili tu kazi, sembuse kuwa na e commerce network ya kiswahili kwenye internet.

Halafu unataka kujilinganisha na mchina?

African languages face the destiny of dinosaurs: Things of the past. For the national, African and even global good, the prevailing power relationships of languages and cultures, has to be challenged and hopefully even shaken up. Let's decolonize our minds
 
25/10/2012
0 Comments

Awali ya yote namshukuru mwenye twitter ID ya "Mabala The Farmer" @Decenttz kwa kuni-tag kwenye tweet-video ambayo imepachikwa hapo chini.

Kwa ufupi, katika video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube, Novemba 14, 2010 na hadi sasa ninapoiweka 'post' hii, imeshatizamwa mara 81 tu, msikilize anayejitambulisha kwa jina la
Marie Francis, mwasisi-mwandaaji Mbio za Marathon za Mlima Kilimanjaro akizungumzia Kilimanjaro Marathon anayoiandaa.

Katika mambo aliyoyazungumzia, kwa mtizamo wake anadhani chaguo la Watanzania kutumia Kiswahili punde tu walipopata Uhuru lilikuwa la makosa. Ametolea mfano wa watu wanaokwenda kuomba viza za kusafiria kuwa wanazungumza Kiingereza kibovu au kutokuweza kabisa kujieleza katika lugha hiyo, katika mfano wake, amewalinganisha na majirani zao wa Kenya wanaowapiku.

Pia amezungumzia tabia ya udokozi na wizi wa hata chupa za maji.

Vile vile amezungumzia tabia ya baadhi ya viongozi kutumia nafasi na nyadhifa zao kuingiza ndugu na jamaa zao katika mbio hizo, ?pengine wa nia ya kujipatia vya bure.

Mabala the Farmer@Decenttz
Mmemsikia huyu mama anayemiliki kilimanjaro Marathon? Kawaua watanzania! youtube.com/watch?v=MadUiA…@Chahali@subinukta@JMakamba@zittokabwe

Preview of Mt. Kilimanjaro Marathon - Running Network - GLSP - YouTube

Matamshi ya Mary katika video hiyo dakika kwa dakika yanasomeka yamenukuliwa hapo chini. Maandishi haya yanaweza yakawa na makosa madogo madogo kwa kuwa tafsiri (auto transcription) inafanywa na software moja kwa moja na lafudhi huweza kuisababisha software ikabandika neno lisilo sahihi. Nimejaribu kuyarekebisha kadiri nilivyoweza... changanya za kuambiwa na zako... utapata maana kamili tu!
---

Source:
http://www.wavuti.com/#ixzz2AJ86Q5JS

"Linguistic and cultural feudalism is the view consciously or unconsciously held that some languages between and even within nations, are of higher order than others; that they constitute an aristocracy while others, in a descending order of being, occupy lesser positions, different degrees of minions"-Ngugi wa Thiong'o
 
Back
Top Bottom