nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
25/10/2012
0 Comments
Awali ya yote namshukuru mwenye twitter ID ya "Mabala The Farmer" @Decenttz kwa kuni-tag kwenye tweet-video ambayo imepachikwa hapo chini.
Kwa ufupi, katika video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube, Novemba 14, 2010 na hadi sasa ninapoiweka 'post' hii, imeshatizamwa mara 81 tu, msikilize anayejitambulisha kwa jina la Marie Francis, mwasisi-mwandaaji Mbio za Marathon za Mlima Kilimanjaro akizungumzia Kilimanjaro Marathon anayoiandaa.
Katika mambo aliyoyazungumzia, kwa mtizamo wake anadhani chaguo la Watanzania kutumia Kiswahili punde tu walipopata Uhuru lilikuwa la makosa. Ametolea mfano wa watu wanaokwenda kuomba viza za kusafiria kuwa wanazungumza Kiingereza kibovu au kutokuweza kabisa kujieleza katika lugha hiyo, katika mfano wake, amewalinganisha na majirani zao wa Kenya wanaowapiku.
Pia amezungumzia tabia ya udokozi na wizi wa hata chupa za maji.
Vile vile amezungumzia tabia ya baadhi ya viongozi kutumia nafasi na nyadhifa zao kuingiza ndugu na jamaa zao katika mbio hizo, ?pengine wa nia ya kujipatia vya bure.
Mabala the Farmer@Decenttz
Mmemsikia huyu mama anayemiliki kilimanjaro Marathon? Kawaua watanzania! youtube.com/watch?v=MadUiA…@Chahali@subinukta@JMakamba@zittokabwe
Preview of Mt. Kilimanjaro Marathon - Running Network - GLSP - YouTube
Matamshi ya Mary katika video hiyo dakika kwa dakika yanasomeka yamenukuliwa hapo chini. Maandishi haya yanaweza yakawa na makosa madogo madogo kwa kuwa tafsiri (auto transcription) inafanywa na software moja kwa moja na lafudhi huweza kuisababisha software ikabandika neno lisilo sahihi. Nimejaribu kuyarekebisha kadiri nilivyoweza... changanya za kuambiwa na zako... utapata maana kamili tu!
---
Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2AJ86Q5JS