Si bure, tumerogwa!

Mwendabure

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,138
1,040
Salam Wakuu! Ni kwa muda mrefu nimekuwa nikifanya uchunguzi ktk majengo yetu muhimu na baadhi ya ofisi hasa zile zilizopo jijini Dar. Kwa muda huo wote nimegundua udhaifu wa kiwango cha kutisha ktk suala la ulinzi wa majengo na mali zilizomo ktk majengo hayo. Kwanza ni kwa upande wa walinzi walio katika sehemu hizo ni wazi wanafanya kazi kwa mazowea kuliko taratibu na kanuni za kazi yao. Ni kawaida kuona mlinzi akimuachia mtu apite langoni bila kumkagua eti kisa ni mfanyakazi au ni jamaa anakuja hapo mara kwa mara, na hivyo salam inageuka kuwa ukaguzi. Ni kawaida pia walinzi wa sehemu hizi kuona anakubali kuachiwa kifurushi/mzigo bila kufahamu vema kilichomo. Pia wakati mwingine huwa unaweza hata kushuhudia anakubali kupeleka mzigo huo kwa mhusika baada ya mletaji kuamua kuishia hapo langoni. Mbaya zaidi walinzi wetu ni wepesi kulaghaiwa hasa kwa haiba na mwonekano wa mtu. Mfano ktk jengo la IPS Bulding, Mlimani City, Milenium Towers, Jengo la Akiba ninao ushahidi wa Video niliyorekodi kwa kutumia simu yangu kuhusu udhaifu wa ulinzi nje na ndani (sina ujuzi wa kuambatanisha hapa) Kwa hali ilivyo nazikumbusha mamlaka zinazohusika kuwa macho na hali ya ulinzi ktk majengo yetu kwani iwapo itatokea watu au mtu mwenye nia ya kufanya hujuma iwe ngumu kufanya hivyo na iwe kwa kiwango kiwango kingine si kama nilivyojionea kwa macho yangu. Tujadili wakuu!
 
Back
Top Bottom