Shule zenye majina ya wanasiasa na matokeo ya mitihani

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Ilianza kwenye barabara na sasa imeenea mpaka kwenye sekta ya elimu. Siku hizi ni kawaida kukuta shule zenye majina ya wanasiasa nchini. Huu mtindo wa shule kuwa na majina ya wanasiasa ulianza wakati wa utawala wa Ali Hassan Mwinyi. Kwa sasa ni vigumu kukosa shule yenye jina la mwanasiasa kwenye kila mkoa.

Kwa mfano, mkoa wa Kagera tuu kuna Sumaye Secondary School, Magufuli Secondary School na Zakia Meghji secondary schoool. Kwa upande wa Dar Es Salaam, Benjamin Mkapa na Yusuf Makamba ni moja ya majina ya wanasiasa yanayotawala kwenye shule za serikali. Pia zipo shule zenye majina ya Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete na Julius Nyerere. Lakini performance ya hizi shule kwa kweli sio nzuri.

Moja shule ambazo matokeo ya kidato cha nne yalikuwa mabaya sana ni Yusuf Makamba Secondary School iliyopo jijini Dar Es Salaam. Shule hii bado inaendelea kushikilia rekodi ya kuwa na matokeo mabaya ya kidato cha nne. Katika matokeo ya mwaka 2010, kati ya wanafunzi 452 waliofanya mitihani, wanafunzi 414 walipata Division 0. Wanafunzi 25 waliobaki walipata kati ya Division I na IV. Matokeo ya mwaka huu yanatia aibu zaidi. Ikiwa imewekwa kwenye kundi la shule zenye watahiniwa 40 au zaidi, shule hii ya Yusuf Makamba imekuwa ya 1,481 kati ya shule 3,108 ikiwa na mwanafunzi mmoja tuu aliyepata Division I, saba Division II, kumi na nane Division III, 139 Division IV na 185 Division 0.

Lakini shule ya Yusuf Makamba ni afadhali kama ukilinganisha Ali Hassan Mwinyi Islamic Secondary School iliyoko mkoani Tabora. Katika matokeo ya mwaka huu, shule hii ilichukua nafasi ya 1,655. Kati watahiniwa 129, hakuna Division I wala II. Watahiniwa watatu tuu ndio waliofanikiwa kupata Division III, wakati 60 wamepata Division IV. Watahiniwa 60 wamepata Division 0.

Benjamin William Mkapa High School, japokuwa ilikuwa na watahiniwa kati ya 19 na 39 walipata Division I na II respectively, watahiniwa 189 wamepata Division IV na 137 wamepata Division 0. Jakaya Kikwete Secondary School ilikuwa na watahiniwa 98. Shule hii haina Division I. Ina Division II moja tuu, Division III zipo nne, Division IV zipo 54 na Divion 0 zipo 39.

Kwa kawaida, shule nyingi zimepewa majina ya wanasiasa kama heshima kubwa kwa wanasiasa husika ambao wanafikiriwa kuwa ni "role models" kwenye jamii. Hata hivyo, performance ya hizi shule kwa kweli inasikitisha tamaa na kuondoa kabisa mantiki ya "role model". Majina ya wanasiasa yanaweza yasi-reflect matokeo ya mitihani kwenye shule huzika lakini inaweza kuwa aibu kwa mwenye jina kama shule ikifanya vibaya. Sijui wanasiasa husika huwa wanajisiaje kwa shule zenye majina yao kufanya vibaya hivyo.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom