mtatifikolo
Member
- Feb 9, 2008
- 43
- 7
Je, utaratibu wa shule maalum kwa wanafunzi wenye vipaji kielimu upo mpaka sasa?
Ninakumbuka miaka 5 iliyopita ndugu Mungai alitoa proposal ya kufuta utaratibu wa Ilboru, Mzumbe, Kibaha kuwa shule za vipaji.
Je, bado zimefutwa?
My take:
1. Tunahitaji shule za vipaji nchini ili kuwepo na 'centers of excellence'?
2. Kama mitihani ya NECTA inayofanywa na wote ni mirahisi kwa wanafunzi wa shule za vipaji, inabidi ianzishwe mitihani maalum ambayo ni migumu zaidi kwa ajili yao pekee.
3. Kuwa na shule kama hizo zinaweza wasaidia wanafunzi wake kupata admission katika vyuo mahiri duniani kutokana na publicity. Alliance High School na Starehe Boys Centre kule Kenya wanautaratibu mzuri. Hizi nazo ni shule za vipaji, na kila mwaka wanafunzi wake kadhaa wanachaguliwa kwenda kusoma nje kwenye vyuo 10 bora.
Shule za watoto wenye vipaji kufutwa
2004-01-03 22:35:31
Na Mawazo Malembeka, PST, Njombe
Wizara ya Elimu na Utamaduni inatarajia kufuta utaratibu wa sasa wa kuwepo na shule za sekondari za wanafunzi wenye vipaji maalum kiakili.
Waziri wa wizara hiyo, Bw Joseph Mungai amesema mjini hapa kwamba, uamuzi huo unatokana na changamoto iliyotolewa na wataalamu wa elimu katika mkutano mkuu wa elimu wa hivi karibuni ambapo wataalamu hao walisema kuwa utaratibu huo una mapungufu.
"Wataalamu hao waligawanyanyika mno na kuhoji kuwa ni vipi mwanafunzi mwenye kipaji maalum au cha pekee apimwe kwa mtihani ambao hata wanafunzi wengine wanaufanya," alisema.
Bw Mungai alisema kuwa wataalamu hao walisema kama kweli wapo watoto wenye vipaji maalumu, hakuna sababu ya basi ya kuwekwa tena katika shule moja badala ya kuwachanganya na wanafunzi wengine ili kuwepo na dhana ya kuwasaidia wanafunzi wadhaifu kiakili.
Alisema kuwa wataalamu hao pia walihoji uwezo au ubora wa shule zinazoitwa za wenye vipaji maalum au vya pekee na kwamba kama shule hizo ni bora au nazo ni za kipekee, na kwamba zinawafundisha nini hasa wanafunzi hao wenye vipaji vya kipekee.
Bw. Mungai alisema wataalamu hao walisema labda kungekuwepo na shule za wanafunzi waliofaulu vizuri mtihani ingawa pia walisema hata kama kungekuwa na
shule za namna hiyo haikupaswa wanafunzi waliofaulu vizuri warundikwe pamoja.
Bw. Mungai alisema wanauangalia upya utaratibu huo na kwamba baada ya kukamilika utaratibu mpya unaoandaliwa, utaratibu wa shule hizo utaondolewa mara moja.
Mpaka sasa kuna jumla ya shule sita za namna hiyo ambazo kwa wasichana ni Msalato, Kilakala, Tabora wakati kwa wavulana ni Mzumbe, Ilboru na Kibaha.