Shule za kata hizo

mwl

JF-Expert Member
May 25, 2011
1,101
913
Mwanafunzi mmoj wa shule ya kata alifanya jaribio la hesabu, swali la kwanza lilimchukua muda wote wa jaribio. Alitakiwa aandike 11, akaanza kuandika 1 kisha akawa anajiuliza moja nyingine aindike wapi kulia au kushoto ya moja ya kwanza?.
 
Unankumbusha kwenye mnada wa kuuza gari embassy ,walileta gari inauzwa: mwarabu akasema dola elfu saba, mwendesha mnada kadakia ,kwangu dola elfu9, mtoto wa mjini, bongo akasema dola elfu 9 na700, mwarabu akaona anaikosa gari akasema dola elfu kumi,yan $10,000 mwendesha mnada akashangilia,akasema dola elfu10 kwa mwarabu mara ya kwanza, mara ya pili, kabla ya mara ya tatu mbongo akasema dola elfu kumi na moja! Dah mwarabu kuona ivo ,hakuongeza akaona bora aende showroom apate gari ya uhakika kwa dola elfu kumi na 500,kwa kuwa yeye alitamani anunue kwenye mnada ila bei isizidi dola elfu kumi na mia tano,yan $10,500/=. Mwendesha mnada kwa mbwembwe anasema 'sasa gari inaenda kwa tajiri mtoto,dola elfu kumi na moja', kwa mara ya kwanza,kwa mara ya pili na ya tatu kwa mbongo. Mwarabu akawasha gari yake akaondoka kwa hasira na kurud zake na dola 10,500 mfukon. Sasa aliyeshinda mnada ,Mbongo kwa ujasiri akatoa bunda la $10,000 kwenye bahasha na akachungulia mfuko wa shati akachomoa dola $1 , jumla $10,001. Mwendesha mnada akamwambia ebu rudisha ufunguo,umesema $11,000. Mbongo akacharuka,akasema yeye katamka dola elfu kumi na moja,yan $10,001. Akasisitiza asifanyiwe usanii! Wote wakabaki midomo wazi,mbongo akaukwaa mkoko kwa dola moja zaidi!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom