Shule za Diwani Bujugo zakatiwa umeme

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]JUMATANO, AGOSTI 15, 2012 06:10 CHRISTINA GAULUHANGA NA JULIANA JOHN, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limekata umeme katika Shule za Green Acres, Salasala zinazomilikiwa na Diwani wa Kata ya Magomeni jijini Dar es Salaam, Julian Bujugo.

Shule hizo zimekatiwa umeme, baada ya kudaiwa zinatumia kwa njia ya wizi na kulisababisha hasara shirika hilo.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Mtaalam wa Mita kutoka TANESCO, Stewartness Makiko ambaye pia ni Mdhibiti wa Upotevu wa Mapato,alisema wamebaini matumizi mabaya yasiyo na tija kwa shule hizo jana, baada ya wafanyakazi wao kubaini mteja wao anatumia umeme kinyume na sheria.

Alisema katika uchunguzi wa awali, walibaini mmiliki huyo amefunga mita ya njia tatu, ambapo njia moja kati ya hizo inatumia umeme mwingi haipitishi kwenye mita, jambo ambalo linasababisha asilipe bili.

Alisema kutokana na hali hiyo, waliamua kukata umeme katika shule ya awali na sekondari na ndipo walipoanza uchunguzi wa shule zote anazozimiliki.

Katika uchunguzi uliofanyika jana, walibaini pia shule ya elimu ya juu diwani Bujugo, iliyopo eneo hilo, nayo inatumia umeme kwa njia ya wizi na kuamua kukata waya.

Mita ya umeme katika shule hiyo, ilifungwa mwaka 2005 ambapo kumbukumbu za TANESCO, zinaonyesha alikuwa akinunua umeme kwa kusuasua na mara ya mwisho alinunua umeme Februari, mwaka huu.

Wafanyakazi hao, waliokuwa wakitumia magari ya shirika hilo yenye namba za usajili yenye namba SU 35601 Mitsubish Pickup, SU 37308 Land Cruiser SU 37159, walijikuta katika wakati mgumu, baada ya wafanyakazi wa shule hizo kugoma kuwapa ushirikiano.

“Tangu jana, tumeshinda hapa kutwa nzima mmiki hataki kabisa kuonana na sisi na hakuna aliyetayari kutupa ushirikiano hivyo na sisi tumeamua kutimiza kazi tuliyopanga kuifanya,”alisema Makiko.

Waandishi wa habari walifanya jitihada ili kuzungumza na mmiliki wa shule hiyo, Bujugo hata hivyo alikataa kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari.

Hata hivyo, hasara ya matumizi ya umeme uliotumika kwa njia ya panya na mmiliki huyo, itafahamika baadaye baada ya kufanya mahesabu.

Wakati huohuo, shirika hilo limesema mwezi ujao litaanika hadharani majina ya vigogo, taasisi na watu binafsi wanaolihujumu shirika hilo.

Akizungumza jana na Waandishi wa Habari ofisini kwake, Meneja Uhusiano wa TANESCO, Badra Masoud alisema, ni vyema wanaolihujumu shirika hilo wakajitokeza hadharani ili waweze kuzungumza nao jinsi ya kulipa gharama walizokuwa wakikwepa.

Alisema ifikapo Septemba, mwaka huu waliochezea mita au kufunga umeme kwa njia zisizo, halali wataanza kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema watakaoshindwa kulipa madeni hayo watafikishwa mahakamani kwa sheria ya Tanzania , Amri ya 35 Kanuni ya 1(d), inayoipa mamlaka shirika hilo, kuzipiga mnada nyumba za wadaiwa ili kufidia deni ambalo shirika hilo linamdai mteja.

 
Huyu Diwani ni wa CCM au CHADEMA? Amegombea UDIWANI ili kuliibia Taifa? Lazima Aende Jela
 
Back
Top Bottom