Shule ya NIMROD MKONO

Nimeuliza..

....kwani unafikiri kafanya nini?

Umeuliza huyu Mkono "tumuiteje fisadi ama kiongozi bora"?

Na mimi nasema, kwa sababu wewe una wonder whether jamaa ni fisadi, labda eleza, kafanya nini?

Nini kilichokufanya ku wonder whether Mkono ni fisadi?
 
Sawa kila mmoja awe fisadi halafu tuamue kila mmoja afanye nini, wengine aweke pesa ulaya, wengine asilimia 2 ya pesa zo wajenge shule, zingine waagize magari na wasafirishe kwa ndege.

The same MKONO mnayemsifia hapa ni yule yule anayeweka order ya gari kiwandani, na anasafirisha kwa ndege. Shule ni kitu kidogo sana, ila kwa sababu MNT(NN):Miafrika Ndivyo Tulivyo (Nyani Ngabu).

Then sawa tu, hata akija kijijini akagawa kanga basi watu mtamchagua tu !
 
Huyu tumuiteje fisadi ama kiongozi bora?
niliuliza sikusema kuwa ni fisadi..

wewe ukalukia
Kwani kafanya nini?

Ufisadi gani?
Umeuliza huyu Mkono "tumuiteje fisadi ama kiongozi bora"?

Na mimi nasema, kwa sababu wewe una wonder whether jamaa ni fisadi, labda eleza, kafanya nini?

Nini kilichokufanya ku wonder whether Mkono ni fisadi?
bado tu unaniwekea maneno.....nani kasema mkono fisadi?

......
 
Umeuliza huyu Mkono "tumuiteje fisadi ama kiongozi bora"?

Na mimi nasema, kwa sababu wewe una wonder whether jamaa ni fisadi, labda eleza, kafanya nini?

Nini kilichokufanya ku wonder whether Mkono ni fisadi?

refer: list of shame,

MWAMBIE amshtaki Slaa
 
Correction. Mkono ndio most succesiful lawyer in TZ in terms of money. Waliosoma naye darasani was an avarage student. Baada ya kupata LL.B hakufanya masters ya sheria.(sorry the omission)

Kwa mengine yote, samahani.

Pasco,

Nimekupa link ya Bunge yenye evidence kuhusu masters degree ya Business Law ya Nimrod Mkono.

Halafu unarudia tena kwamba Mkono hakusoma masters, huku unajifanya kuomba msamaha.

Kwa nini unaleta intentional misrepresentation?
 
Swali la msingi, je ni kweli hiyo shule kajenga Mkono?? kama kweli fwedha katoa wapi? Acha ligi za kitoto......

Okay, ahsante.

Kwa hiyo ishu siyo ufisadi, sijui BOT, sijui hukuwa na kichwa darasani, sijui list of shame, and all that jazz.

Ni shule ya Mkono.

Ha ahahahahahaa.

Okay, naona tumerudi kwenye mada, kwenye kichwa cha thread.

Shule ya Nimrod Mkono!
 
Kwa kweli jamaa ameukata. Ni very enterprising na wakati huo huo anatoa misaada sana. Yeye ni kama Robin Hood.

Kitu kilichonishangaza sana ni pale Mkono alipowania uenyekiti wa Umoja wa Wazazi. Licha ya yeye kuisaidia sana CCM in numerous occassions tena kwa fedha nyingi bado Kamati Kuu na Halmashauri Kuu za CCM zilikata jina lake. Nadhani CCM ina ajenda ya siri kuuuwa Umoja Wazazi na hawataki mtu mwenye uwezo aiendeshe. Kumbuka walimkataa Iddi Simba wakampa Malegesi akaishia kuiba pesa. Sasa wamemkataa Mkono sijui watampa nani..
 
mpe hongeni zake huyu mzee kwa kutumia elimu yake na fedha zake kwa manufaa ya wananchi walio maskini.

sio hela zake bali ni hela zetu alizoiba benki kuu wacha upumbavu...

Mpaka sasa amelipwa $80m na benki kuu na kesi ni za kutengeneza na hamna hata moja aliyoshinda
fisadi mtupu

Anakujengea shule ili uumpe ubunge apate kukuibia vizuri.......

Atashinda ubunge hapo kijijni mpaka afe

HIYO SHULE NI YA KAWAIDA SANA
 
Last edited:
A. WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI



6. NIMROD ELIREHEMA MKONO

Mheshimiwa Nimrod E. Mkono ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijiji na Mshiriki Mkuu wa kampuni ya mawakili ya Mkono & Company Advocates ya Dar es Salaam. Barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali inaainisha kuwa Benki Kuu imekuwa ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co. Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia ambapo Benki Kuu inadaiwa jumla ya shilingi bilioni 60. Kwa mujibu wa barua ya wakaguzi tayari Mkono & Co. Advocates wamekwishalipwa shilingi 8,128,375,237 kwa fedha taslimu kwa kesi hiyo ambayo bado iko mahakamani. Malipo haya ni sawa na asilimia 13.5 ya deni lote inalodaiwa Benki Kuu. Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni kuwa kesi hii haina muda maalumu wa kumalizika na hivyo inawezekana kabisa malipo ya wanasheria yakazidi kiasi cha fedha inachodaiwa Benki Kuu.

Lakini hoja nyingine ya kimsingi ni kama malipo haya kwa mawakili yanaruhusiwa chini ya Kanuni za Malipo ya Mawakili na Uamuzi ya Gharama za Kesi za mwaka 1991, Tangazo la Serikali Na. 515 la mwaka 1991 (Advocates’ Remuneration and Taxation of Costs Rules, 1991). Kanuni hizi zimeweka kiwango cha malipo ya mawakili katika kesi ambazo fedha inayodaiwa ni zaidi ya Shilingi milioni 10 kuwa ni asilimia tatu. Kwa kufuata masharti ya sheria hii ya malipo ya mawakili, kampuni ya Mkono & Co. Advocates ilipaswa kulipwa Shilingi bilioni 1.8.

Kampuni ya mawakili ya Mkono & Co. Advocates imekuwa ikitajwa kuhusiana na kashfa kubwa za ufujaji na/au ubadhirifu wa fedha za umma kwa muda mrefu. Kwa mfano, ‘Taarifa ya Uchunguzi Kuhusu Tuhuma Dhidi ya Makampuni ya Tanfarms Ltd., Makinyumbi Estates Ltd., Centrepoint Investments Ltd., na Arusha Farms Ltd. Yanayomilikiwa na V.G. Chavda Kuhusiana na Matumizi Mabaya ya Fedha za Debt Conversion Programme’ iliyotolewa Bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Edward Oyombe Ayila mwezi Novemba 1994 ilisema yafuatayo kuhusu Mheshimiwa Nimrod Mkono: “Mhe. Spika si nia yangu kulichosha Bunge lako tukufu na hotuba ndefu lakini ni vizuri nikaelezea juu ya uhusiano unaotia mashaka kati ya V.G. Chavda na Mashamba yake na Subash Patel mwenye makampuni ya DECO ART, MM Motors, MM Garage, Hotel Sea Cliff, City Bureau De Change na Nimrod Mkono, Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Mkurugenzi katika makampuni ya AZANIA AGRICULTURAL ENTERPRISES, LIBERTY LEATHER SHOE LTD., AZANIA EXIMCO, n.k. (AIMS GROUP OF COMPANIES)

Baada ya kuelezea uhusiano huo ulivyokuwa Mheshimiwa Ayila alimalizia kwa kusema yafuatayo: “Mheshimiwa Spika, ni vigumu kabisa katika hali ya kawaida kwa mtu yeyote kuamini kwamba makubaliano haya na uhusiano uliojitokeza hapa haukuwa wa hila. Chavda kwa kupitia wakili wake Nimrod Mkono, aliomba Mahakama Kuu kuzuia kabisa shughuli za Kamati (permanent injunction). Aidha ni wakili huyo huyo ambaye ameshuhudia uuzaji wa deni la Deco Art (reassignment) kwa Chavda. Mheshimiwa Spika, hali hii ukiitazama kwa undani utaona kwamba pengine kuna kitu kinafichwa. Nimrod Mkono alikuwa Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Oxford Services Ltd. na pia anamiliki Kampuni ya Marcus Ltd., makampuni ambayo kwa pamoja yamefaidika kwa kuupata jumla ya Shs. 4,477,870,279.61 chini ya utaratibu wa DCP.”

rudi...
 
Siko impressed na michoro. Kama watajenga kama inavyoonyeshwa kwenye michoro wataharibu mandhari ya Butiama kama vile lile kasri lilivyofanya. Kile ni kijiji na majengo yanatakiwa kwenda na hali ya kijiji. Hii haimaanishi kuwa yawe duni bali hayatakiwi kujitokeza mno. Mfano mzuri ni nyumba ya kwanza ya marehemu Mwalimu. Ni jengo zuri lakini haliharibu mandhari. Hii college kama vile ilivyo ile kasri ni jengo la majigambo. Linafunika kila kitu. Vile vile maslahi kwa Butiama sioni. Hii itakuwa shule kwa wenye nazo na wengi wa wanakijiji wataishia kuosha vyombo na kutambua uduni wao mbele ya wanafunzi, walimu na wafanyakazi wa chuo hicho. Hii ni tofauti na falsafa ya huyo ambaye wanadai wanataka kumuenzi. Wakitaka kuwasaidia, kijengwe chuo ambacho kitalengwa kwa wanakijiji na wazazi wao! Kinachofanyika hapa ni kutafuta sifa!

Amandla...............
 
Huyu jamaa kajitahidi.. sasa kwa nini Chenge akapeleka 'vile visenti' New Jersey Islands, asijenga hata shule ya sekondari kule Tabora?

Kwao ni Bariadi na alijenga pale alipotaka kugombea ubunge,otherwise hakuwa na mpango kabisa wa kujenga nyumbani kwao na mpaka leo kwao kijijini bwana vijisenti hajajenga
 
Mkjj leta mistari tukate ishu! mie nasema Nimrod ni Fisadi lililobobea na ni hatari kuliko RA, yeye kajificha kwenye capsule ya uzawa na taaluma yake, pia ili aendelee kujenga wigo mpana ndipo alipojiingiza kwenye siasa ili kupata ulaji kwa ulaini akishirikiana na kale kakundi ka...."kila mtu na kamhogo kake"
 
Back
Top Bottom