Rosweeter
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 1,171
- 4,432
Nimekuwa nikiguswa sana na hali ya mazingira ya Shule ya msingi Muhimbili. Imekuwa ni kawaida kwa maji machafu kufurika na kumiminika katika mazingira ya shule hiyo. Hali inakuwa tata zaidi inyeshapo mvua. Nina miaka saba katika maeneo haya na siku zote hali imekuwa ikijirudia mara kwa mara.
Mazingira haya ni hatarishi sana hasa kwa watoto wadogo wanaosoma shule hapo. Ninaamini afya za watoto hawa zinalindwa kwa kudra za mwenyezii Mungu tu kwani wako katika mazingira hatarishi sana hasa yatokeapo magonjwa ya milipuko. Ninachoshangaa ni jinsi ambavyo wahusika wamelifumbia macho suala hili na kuonekana kuridhika kwa kukaa bila kuboresha miundo mbinu katika shule hiyo na mazingira yanayoizunguka. Uongozi wa shule na kamati ya shule hawalioni jambo hili? Wazazi mnaosomesha wenye watoto katika shule hii mmeridhika na hali hii? Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, ni wajibu wenu kuhakikisha miundo mbinu inaboreshwa.
Wito wangu naomba Halmashauri husika ilifanyie kazi suala hili siyo kusubiri mpaka maafa yatokee ndiyo ionekane kuna tatizo kama ambavyo tumeshazoea.
Nawasilisha.