Shule ya Msingi Msoga na Mgodi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,185
307
Wadau,

Katika vyombo vya habari leo kuna habari kubwa mbili, uzinduzi wa shule iliyojengwa kwa msaada wa serikali ya China na nyingine ni ile inayohusu mgodi wa makaa ya mawe Mchuchuma.

Naona kama kuna dots zinaungana hapa.... Hapo nyuma kuliibuka tetesi kuwa kampuni moja ya jijini Dar (inayomilikiwa na watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi katika kashifa nyingi zinazolikabili taifa hili) ndiyo imepewa mgodi huu, kulikuwa pia na tetesi kuwa nyumba ya mkulu ilijengwa na kampuni hiyo iliyokuwa imepata mgodi wa makaa ya mawe.

Swali langu je hii kampuni ya uchina siyo ya aina ya Dowans? Wachina wametumiwa kama kinga dhidi ya hasira za wabongo??

Na kwa nini vitu hivi vyote vitangazwe siku moja??

Tafakari
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom