Shule: Wapi nimpeleke mwanangu?

Max,
Samahani kwamba sitaweza kujibu swali lako la msingi katika kukusaidia kupata shule, ilaninaomba nichangie kidogo kwenye huu mjadala.
Ni vyema jamii ya kitanzania, hasahasa jamii ya wasomi, ikawa inafanya maamuzi yake objectively. Kweli watoto wetu wanachohitaji ni hizi shule za kulipa dola 10,000 kwa mwaka? Ninaposema tuwe objective namaanisha tuwe result oriented. Je watoto waliosoma kwenye hizi shule wamefanya nini kinachotuvutia na sisi kutaka kuwapeleka watoto wetu huko? je, wale waliosoma kwenye hizo shule wana mchango gani kwenye jamii yetu ya sasa kutokana na kile walichojifunza kwa gharama kubwa kuliko medical degree? Nitatoa mfano hapa, Mzumbe Secondary na Ilboru imetoa wataalam ambao wamejaa kwenye mahospitali yetu, wanafundisha kwenye vyuo vyetu, watafiti etc. Hawa waliosoma IST na ISM wako wapi? Harvard University imetoa viongozi katika nyanja mbalimbali za kisansi, kisiasi nk. IST na ISM zilikuwepo kabla hata ya kuanzishwa kwa utaratibu wa shule za watoto wenye viapji maalum, inakuwaje waliosoma kwenye hizi shule za watoto wenye viapji maalum tunawaona kwenye jamii lakini waliosoma IST na ISM hatuwaoni? Hii inanirudisha kwenye soma la falsafa ya udaktari, what is the meaning of good?- hili siyo swali rahisi, lakini kila mtu anaweza kujipatia jibu litakalomfaa.
Nadhani shule nzuri kwa mtoto ni ile ambayo kwanza ni salama kwake, pili ambayo itampa ujuzi utakaomuwezesha kuyamudu maisha yake na kuwa na nafasi na uwezo wa kushiriki katika kuendeleza jamii. Je, katika maeneo unayoishi hakuna shule yenye kumwezesha kijana wako kuyapata haya? Kama ipo hakuna haja ya kusita kumwandikishe mtoto huko.

Pia nitaandika kidogo kuhusu wazazi wanaowatafutia watoto wao shule za A-level. Mtoto aliyemaliza form four anategemewa kufahamu zaidi kuhusu shule za A-level kuliko wazazi wake(of course kama wazazi sio walimu). Kuna swala la combination, mtoto anatarajiwa kufahamu zaidi combination anayoipeda na kuimudu kuliko mzazi. Kwa Tanzania wanafunzi humaliza form four na umri wa kama miaka 17 hivi. Ni vyema wazazi wakawa na moyo wa kuwaamini watoto na kuwaacha wasimamie mambo wanayoweza kuyamudu.Nadhani swala kutafuta shule ya A-level mwanafunzi aliyemaliza form four anaiweza, wazazi/walezi wampe guidence na kumuwezesha financially. Hii ni katika kumjenga mtoto kujitegemea.
 
Ila kitu kimoja ambacho nimeona humu: Kwa kweli TANZANIA kadri siku zinavyokwenda thamani ya elimu inayotolewa na serikali inazidi kushuka. Maana hakuna hata mmoja aliyeshauri jamaa aende shule za serikali. Jamani wananchi we need to do something..otherwise watoto wetu watakosa elimu bora na watakuwa wapagazi wa hawa wanaoenda IST na kwingineko. I can tell, mtu wa Kigoma huo uwezo wa IST hana..sasa jamani something must be done to help this poor guy..na yeye aje kucompete na wengine.

"Watoto wetu watakuwa wapagazi wa hawa wanaoenda IST," watoto wenu wewe na nani? Umepotea njia, ndugu Masanja, hapa sio pako hapa.

Huwezi ukawaambia wazazi wa watoto wa International School of Tanganyika wawajali watoto wa "mtu wa Kigoma" ili "aje kucompete na wengine." Hupati picha: wanataka watoto wao wa IST ndio washinde hayo mashindano, sasa huwezi kuwaambia wazazi hawa hawa ndio wakusaidie wewe kushindana na watoto wao.

Nenda Kigoma huko ukajaribu kujenga na kuimarisha hizo shule, sio kuja kuwaambia hawa hawa wazazi wenye neema wa Jamiiforums wanaojadili shule za kupeleka wanao ili waje wakasome nje baadae. Wanaongelea kufanyia usaili vitoto vya chekechekea kabla havijakubaliwa kuingia darasa la kwanza. Vinaanza kuchujwa na kubaguliana toka vinanyonya, wewe unaongelea vitoto vya Kigoma hapa? Huoni kwamba mko dunia mbili tofauti? Unawapigia mbuzi gitaa. Hawa ndio wale wale. Hawa wazazi na wenyewe walijisomesha wenyewe hawa. Hawakutumia kodi ya mkulima wa Kigoma hawa, sasa kwa nini wawe na uchungu na mtoto wako, kapuku wa Kigoma wewe? Au una gubu na neema yao?

Sio kwenye hili jamvi, la hasha. Kesi ya ngedere utaipelekaje kwa kima? Sio kwenye uzi wa majadiliano ya wazazi wa watoto wa International School of Tanganyika. Rudi kafanye harakati Kigoma huko. Nambie wapi.
 
Kuna shule zifuatazo but its the matter of choice whether you will like them or not pia ada nayo ina depend

1. IST (International School of Tanganyika) hii iko Masaki one of the best
school in this country
2. ISM (International School of Moshi) hii iko Moshi i guess its affiliated to IST
3. BROOKHOUSE INTERNATIONAL hii iko Arusha
4. DIS (Dar es Salaam International School) hii iko Mikocheni.

So far this are my best schools any one can come up with the list of schools ambazo anafikiri in one way or another zina mitaala mizuri ya kufundishia
 
mimi huwa nikitafuta shule naweka priorities katika vitu ninavyohitaji. Natembelea shule, naulizia wizarani matokeo yaliopita, naulizia tabia ya mkuu wa shule, naangalia uhamaji wa walimu, ukubwa wa darasa, masomo na sylabus inayotumika, mwelekeo wa kiimani wa uongozi wa shule, (ni lazima shule iwe na somo la dini) extracuricular activities zinazosimamiwa na shule.
nikiridhika huwa nahamishia watoto mara moja, manake shule za siku hizi ni kama saluni, inakuwa nzuri tu kama kuna mwalimu fulani, akiondoka imekufa, sasa ya nini wewe ubaki?
mwanangu wa darasa la 4 sasa ameshasoma shule 4 tangu babyclass,
 
Mtoto aliyemaliza form four anategemewa kufahamu zaidi kuhusu shule za A-level kuliko wazazi wake(of course kama wazazi sio walimu). Kuna swala la combination, mtoto anatarajiwa kufahamu zaidi combination anayoipeda na kuimudu kuliko mzazi. Kwa Tanzania wanafunzi humaliza form four na umri wa kama miaka 17 hivi. Ni vyema wazazi wakawa na moyo wa kuwaamini watoto na kuwaacha wasimamie mambo wanayoweza kuyamudu.Nadhani swala kutafuta shule ya A-level mwanafunzi aliyemaliza form four anaiweza, wazazi/walezi wampe guidence na kumuwezesha financially. Hii ni katika kumjenga mtoto kujitegemea.

Ze Marcopolo,

Thanks, you have said it all man and you seem to have good experience of raising and handling youths in academic affairs!
 
Hii thred na ile ingine ya Arusha ya shule yaani zimenifungua sana macho na kunipa mwanga!

Ndo maana napenda JF!
 
Max,
Samahani kwamba sitaweza kujibu swali lako la msingi katika kukusaidia kupata shule, ilaninaomba nichangie kidogo kwenye huu mjadala.
Ni vyema jamii ya kitanzania, hasahasa jamii ya wasomi, ikawa inafanya maamuzi yake objectively. Kweli watoto wetu wanachohitaji ni hizi shule za kulipa dola 10,000 kwa mwaka? Ninaposema tuwe objective namaanisha tuwe result oriented. Je watoto waliosoma kwenye hizi shule wamefanya nini kinachotuvutia na sisi kutaka kuwapeleka watoto wetu huko? je, wale waliosoma kwenye hizo shule wana mchango gani kwenye jamii yetu ya sasa kutokana na kile walichojifunza kwa gharama kubwa kuliko medical degree? Nitatoa mfano hapa, Mzumbe Secondary na Ilboru imetoa wataalam ambao wamejaa kwenye mahospitali yetu, wanafundisha kwenye vyuo vyetu, watafiti etc. Hawa waliosoma IST na ISM wako wapi? Harvard University imetoa viongozi katika nyanja mbalimbali za kisansi, kisiasi nk. IST na ISM zilikuwepo kabla hata ya kuanzishwa kwa utaratibu wa shule za watoto wenye viapji maalum, inakuwaje waliosoma kwenye hizi shule za watoto wenye viapji maalum tunawaona kwenye jamii lakini waliosoma IST na ISM hatuwaoni? Hii inanirudisha kwenye soma la falsafa ya udaktari, what is the meaning of good?- hili siyo swali rahisi, lakini kila mtu anaweza kujipatia jibu litakalomfaa.
Nadhani shule nzuri kwa mtoto ni ile ambayo kwanza ni salama kwake, pili ambayo itampa ujuzi utakaomuwezesha kuyamudu maisha yake na kuwa na nafasi na uwezo wa kushiriki katika kuendeleza jamii. Je, katika maeneo unayoishi hakuna shule yenye kumwezesha kijana wako kuyapata haya? Kama ipo hakuna haja ya kusita kumwandikishe mtoto huko.

Pia nitaandika kidogo kuhusu wazazi wanaowatafutia watoto wao shule za A-level. Mtoto aliyemaliza form four anategemewa kufahamu zaidi kuhusu shule za A-level kuliko wazazi wake(of course kama wazazi sio walimu). Kuna swala la combination, mtoto anatarajiwa kufahamu zaidi combination anayoipeda na kuimudu kuliko mzazi. Kwa Tanzania wanafunzi humaliza form four na umri wa kama miaka 17 hivi. Ni vyema wazazi wakawa na moyo wa kuwaamini watoto na kuwaacha wasimamie mambo wanayoweza kuyamudu.Nadhani swala kutafuta shule ya A-level mwanafunzi aliyemaliza form four anaiweza, wazazi/walezi wampe guidence na kumuwezesha financially. Hii ni katika kumjenga mtoto kujitegemea.

- Basi nakushauri pitia alumni zao. Soma majina. Kuna majina mengine ni very prominent nchini, ila wako very downlow (najua utakuja na sababu kwamba wana hela). Pia kumbuka graduates wa 80's, 90's ndio watu wazima sasa, wanajijenga, soon utawaona tu. Ila wapo walio kwenye 40's late 30's wanaingizia pesa nchi.
-Pia, wengi wanapenda kuwa self-employed na wapo wenye makampuni makubwa yana employ waTanzania. Utajikuta unaenjoy fast internet speed (present and future) na mitandao ya simu kutokana na product wa ISM/IST.
-Halafu kumbuka comparison unayotaka kufanya ni ya shule 2, ukilinganisha na shule nyingi za serikali. Ukitaka kufanya hivyo, vuka mipaka nje ya nchi, utakutana na product wa IB, kuna waTanzania wako kwenye medicine, engineering, pilots, economics etc na wanacompete on same level na wazawa wa nchi hizo.

Pia, kusoma sio lazima uajiriwe na serikali (au hata uajiriwe). Hayo mawazo yamepitwa na wakati. Hao madaktari unaosema wamesoma shule za kawaida na muhimbili, mbona wakipigwa posti vijijini hawaendi? Mtu unajenga maisha yako kivyako, mzazi anakufungulia tu milango.

Pia usifikirie mtu akimaliza form 4 anakubaliwa afanye IB, kuna wengine akili nzito walimu wanamwambia mzazi mtoto wako kafeli, IB haiwezi, anatemwa (hata kama una pesa ya kulipia IB).

Multiculturalism inasaidia sana. Ndio maana unakuta vijana wengi wakija kusoma nje ya nchi, wanashangaa shangaa 4 a few months if not a year, then the world has passed them. We umezoea kulishwa na kutunzwa na mzazi hujui kufanya kazi au kubeba maboksi. Kama huna international exposure kupitia kisomo cha shule, inakuchukua muda kuwa independent.

Anyways, kufanikiwa maishani sio lazima uspend pesa nyingi, ni drive ya mtu, ushapu na bahati. Ila kama pesa ipo ya kumsaidia mtoto milango ifunguke, then why not?

Also, life is about connections. Wewe ukikutana na mtu uliyepita naye jeshini, au shule moja, story kibao mnakumbushana (cos you have something in common). Now, imagine, mimi nakutana na Mchina au Mbrazil, au Mrusi kasoma IB, how much do you think I will be able to achieve in terms of connections and common outlook to things?
 
-

You are very right....

Former British Deputy Prime Minister John Prescott once said in Britain 85% of Top Jobs have people who went to Private School and top Universities like Oxford, Cambridge, London etc. Not only education in those institutions is of high standard but mainly because of lifetime friendships that are formed and become very valuable at later stage in the real world. I couldn't agree more with John.

- Basi nakushauri pitia alumni zao. Soma majina. Kuna majina mengine ni very prominent nchini, ila wako very downlow (najua utakuja na sababu kwamba wana hela). Pia kumbuka graduates wa 80's, 90's ndio watu wazima sasa, wanajijenga, soon utawaona tu. Ila wapo walio kwenye 40's late 30's wanaingizia pesa nchi.
-Pia, wengi wanapenda kuwa self-employed na wapo wenye makampuni makubwa yana employ waTanzania. Utajikuta unaenjoy fast internet speed (present and future) na mitandao ya simu kutokana na product wa ISM/IST.
-Halafu kumbuka comparison unayotaka kufanya ni ya shule 2, ukilinganisha na shule nyingi za serikali. Ukitaka kufanya hivyo, vuka mipaka nje ya nchi, utakutana na product wa IB, kuna waTanzania wako kwenye medicine, engineering, pilots, economics etc na wanacompete on same level na wazawa wa nchi hizo.

alumini wa hizo shule wananafasi nzuri kwa ajili baba zao walikuwa kwenye system na bado wako kwenye system, mzazi ambaye anaweza kumlipia mwanae 10,000 secondary school ni mtu ambaye anapesa sana kwa maisha ya TZ kwa hiyo atamchomeka mtoto wake hata kama hana akili.

wako self employed kwa ajili wakimaliza shule wanakuta baba zao washawaandalia kampuni au mtaji wa kufungulia kampuni...
umemaliza shule tu utatoa wapi hela ya fungua kampuni hata kazi ujafanya

tofauti ya hizo shule na zingine ni english tu.......

vijana wengi wanapata kazi TZ wakiwa wametoka shule za kawaida tu na wengi wa wanafunzi wa IST sio wachapa kazi na wanabebwa na baba zao
 
Max, nakushauri umpeleke huyo mtoto shule ya msingi Muhimbili. Kama siyo Muhimbili, basi Bunge, kama siyo Bunge, basi Oysterbay.

Mimi nimesoma vidudu mpaka secondary kwenye shule zetu kawaida hapa Bongo, leo hii naangalia nyuma na kuona bahati niliyokuwa nayo.

Teknolojia imekua ndugu. Yale ambayo watoto wa shule za kawaida walikuwa hawawezi kuyapata zamani, leo hii yanaweza kupatikana kwa asilimia kubwa...haswa pale mzazi unapoonesha uwezo wa kumpeleka mtoto wako shule yoyote ile bila kujali gharama. Mambo ya exposure ya kimagharibi ndiyo hayo yaliyotutofautisha sana sisi na watoto wa IST au ISM nyakati hizo, though tulikuwa tuna hang nao tu mitaani. Kiingereza sijui kifaransa kwa siku hizi inategemeana na mzazi tu kwa kweli. Kama ni mwenye kupenda mtoto wake aongee Kiingereza mapema na anauwezo kipesa, basi mtoto ataongea hata kama mtoto anasoma Mbuyuni au Ushindi au Mikoroshoni au Makongo au Magomeni au Kawe primary schools.

Kikubwa ni shule za sekondari. Hapa chaguo ndiyo muhimu. Maana age ya 13 - 17 tabia zinazoweza kubakia na mtoto maisha na kumdefine ndiyo hukomaa. Shule ambayo naweza kuipendekeza ni Aghakhan Secondary School. Kuna mbinde katika kuingia, lakini ukiwa na tupesa ulitotutunza kutokana na kuepukana na gharama za mtoto akiwa msingi au vidudu, basi hapa ni pahala dhahiri pa kutumia tu pesa huto.

Good luck either way.

SteveD.
 
alumini wa hizo shule wananafasi nzuri kwa ajili baba zao walikuwa kwenye system na bado wako kwenye system, mzazi ambaye anaweza kumlipia mwanae 10,000 secondary school ni mtu ambaye anapesa sana kwa maisha ya TZ kwa hiyo atamchomeka mtoto wake hata kama hana akili.

wako self employed kwa ajili wakimaliza shule wanakuta baba zao washawaandalia kampuni au mtaji wa kufungulia kampuni...
umemaliza shule tu utatoa wapi hela ya fungua kampuni hata kazi ujafanya

tofauti ya hizo shule na zingine ni english tu.......

vijana wengi wanapata kazi TZ wakiwa wametoka shule za kawaida tu na wengi wa wanafunzi wa IST sio wachapa kazi na wanabebwa na baba zao

Tofauti ya hizo shule ni English tu? Shule zipi unazoongelea? Inabidi utofautishe academy na real international schools. Kama unaongelea hizi bubblegum academy, hata hiyo english ni ya kusoma tu, percent kubwa ya hao wanafunzi hawawezi ku-construct sentence za maana wala kujieleza vizuri, na mara nyingi (majority) wakitoka nje ya nchi wanapigwa foundation year university na english course juu na wanaishia college au university mbuzi. Ndio maana nikasema, up to form 4, mpeleke mtoto wako shule yoyote, nikasema, if you can afford, IB ni investment nzuri.

Pili, dont hate, nilijua mtu atakuja na argument ya kuwa kwenye system. Mzazi ampeleke mtoto hapo, usitegemee huyo mtoto atakuja afanye kazi na mshahara wa serikali. Wazazi wengi wanaopeleka watoto ISM au IST, tena unakuta aidha ni madaktari, engineers au lawyers waliopata kisomo enzi za mkoloni kwa taabu. Hawa wakiwa ndio wasomi wa kwanza nchini wametengeneza pesa zao clean and through hard work na kujinyima. Wanaona wawapatie watoto wao vitu ambavyo hawakupata. Thats what you, me, Yebo Yebo or Maxence will offer a child, the best you can afford in anything (na ndio maana mtu anajikuna anapoweza kufikia). Pia, nimesoma na watoto ambao wazazi wao ni wafanyabiashara wa miaka nenda rudi. Wazazi wengine hata kusoma ripoti hawajui, lakini wamehangaika kutafuta pesa through generations (if you come from an industrious family, you will be industrious by nature, unless you just dumb). Clean money!! IF they made money through loopholes in the system dont blame them! Blame your country!! Dont blame the system, get on the system godamnit!! Every country has loopholes (clean and dirty loopholes).

Mtoto hata kama hana akili atachomweka yes, ila akifika form 4, akibugia haruhusiwi kuingia IB (5 and 6), na IB ndio inatofautisha appeal to the whole world. Uingereza wenyewe wanafikiria kuscrap GCSE (A-Level) wawe na IB. I got a $5000 knock off (per year) offer from a University in the USA just because I had IB!! Nikienda interview, mara nyingi wanataka kujua experience ya IB.

Pia, alumni wana michango kwenye mifuko ya scholarships ambazo hutolewa kusaidia vijana wenye akili sana kutoka familia zisiyojiweza na kuwaingiza wafanye IB. So usifikirie watu wako selfish.

Finally, walio kwenye system kwa kuiba, wanapeleka watoto wao boarding za primary hata secondary nchi za ulaya (cos they got something to hide), ingawa sio wote mafisadi (but thats the trend). Kwahiyo tofautisha hard-earned money and fisadi money within a system. Pia, huwezi ukakuta product ya ISM au IST wako sehemu kwa undugunization kama BoT! You are there cos you can do the job, even if by referral.
 
Back
Top Bottom