Shule nyingine inayo wasuta viongozi wetu na mashangingi yao (picha)

Andindile

JF-Expert Member
Mar 18, 2009
304
16
4800d1244646684-shule-hizi-zipo-tanzania-ya-mashangangingi-namtumbo-1-.jpg


nimeattach hiyo picha nimeshinndwa kuibandika ili ionekane moja kwa moja. Mwenye uwezo wa kufanya hivyo anaweza kuibandika upya. Enjoy
 

Attachments

  • Namtumbo[1].jpg
    Namtumbo[1].jpg
    236.9 KB · Views: 768
Last edited by a moderator:
Du hivi hawa mbunge wao nani au hawana hata muwakilishi wao bungeni? Leo mkuu wa kaya anazungumzia Stimulus package....kwanini hawafikirii kuwastimulate kwanza raia wao wanapata mateso haya kwenye nchi yao ya ahadi?
 
Hizi shule zipo nyingi Tz, na zinasikitisha sana.Ukienda kwenye vijiji vingi kuna type ya hizi shule.
 
..Namtumbo ni jimbo la Raisi Mkapa.

..alishawahi kuwa Mbunge huko kabla hajawa Raisi.
 
Na sasa Mkapa amehama kule amejenga Mansion Lushoto! Nani awe na uchungu na Namtumbo?
 
Last edited:
Mnashangaa nini wakati unaelewa wazi wale jamaa mjengoni wanawakilisha matumbo yao tuu?Watakujali kitu gani we mtoto wa kabwela wakati wametumia mapesa yao kununua ubunge!Cha kushangaza zaidi wewe uliyeleta picha hii bado utawapigia debe na kuwafagilia wakati wa kampeni zijazo,amkeni jamani wakati wa mageuzi ni sasa.
 
Inauma sana na kusikitisha Kweli Miafrica ndivyo tulivyo.
Utaona hao hao waliopo kwenye maeneo magumu kama hayo ukienda kuwapa elimu hawakuelewi na wakipewa kofia ya kijani basi umewaloga kura zote ni zako. Tunasafari ndefu.
 
Du hivi hawa mbunge wao nani au hawana hata muwakilishi wao bungeni? Leo mkuu wa kaya anazungumzia Stimulus package....kwanini hawafikirii kuwastimulate kwanza raia wao wanapata mateso haya kwenye nchi yao ya ahadi?

Lol! Mbunge wao anaitwa VITA KAWAWA, mtoto wa waziri mkuu mstaafu Mh Kawawa. Ila sishangai kwani hata baba yake(mh kawawa) yuko kule kijijini madale tegeta hata maji ya bomba hana, anapelekewa tu kwenye vibuyu vilivyobebwa na malori!! sasa kama hamjali baba yake atawajali wapiga kura wake?
na mkapa shame on you! unakula bata Lushoto wakti watu wako huko wanateseka!! Lol! Mijiongozi ya kiafrika ndivyo ilivyo!!!
 
Tatizo ni viongozi wote kuanzia kiongozi wa nyumba kumi hadi hukooo juuuuu kabisa. Wanakasoro ya kufikiri. Hawaoni aibu wanapoona uozo wa namna hiyo. Kazi yao ni atajisifu kuwa mwendo mpya na kasi mpya na kuigizo kutoa hotuba za matumaini kama zekomedy. Chakushangaza ni kuwa majimbo kama hayo yanawabunge waliojichagua wenyewe na familia zao. Na wanao-ongozwa hawawezi kusema hapana maana kijiji kizima yupo huyo. Tunao weza basi tuamke wao ni wachache kuliko sisi.
 
kila siku na sema viongozi wetu wamegombea nafasi za serikalini hili kugomboa maisha yao sio maisha ya mtanzania.hawana elimu ya kutosha ya kuweza kuhudumia wananchi kwani ni waoga mno wa maisha yao binafsi.wanaona kwamba bila kuiba pesa serikalini hawatafanikiwa.huwezi kuniambia billioni 200 za kuibiwa na mafisadi zipo na bila mtu kuwajibika na hela za kujenga shule na kuweka madawati hamna.
 
..Namtumbo ni jimbo la Raisi Mkapa.

..alishawahi kuwa Mbunge huko kabla hajawa Raisi.

Nakumbuka Mkapa alikuwa mbunge wajimbo la Nanyumbu lililopo mkoani Mtwara.

Jimbo la (wilaya?) Namtumbo lipo mkoani Ruvuma na sikumbuki kwamba Mkapa alishawahi kuwa mbunge huko.I could be wrong, but my memory rarely serves me wrong I have been following parliamentary elections since the days of Gutram Itatiro and them, completely memorizing the faces off of "Daily News" as if it was a standard four exam requirement.

Of course this is not to absolve Mkapa of his responsibility in any way, far from it, as a president he was the "mbunge" wa nchi nzima.
 
Last edited:
mm nikiona hivi roho inaniuma.
Hivi kweli watoto wa waheshimiwa wetu yanawapata haya?
 
Hapa suala si ni la mbunge gani au shule kama hii iko jimbo gani. Suala ni kuwa shule kama hizo zipo nyingi bado nchini. Mkopo ule wa MMEM ulitarajiwa kumaliza shule kama hizo.

Tatizo ni kuwa shule kama hizo hazikuisha na MMEM hela zilikwisha na tutalipa to our asses pamoja na riba zake zote. Uliza katika budget ya mwaka huu kuna initiative gani ya kumaliza shule kama hizo? At least mazingira tu?

Pessa iliyotengwa inaweza kuwa nyingi tu. Lakini itaishia kwenye warsha, semina na makongamano kwa makamishna na wakurugenzi wa elimu hapo Dar es salaam. Nyingine itaishia kwenye kulipia safari za mafunzo kwa watu hao hao nje ya nchi pamoja na kuhudhuria mikutano mbali mbali ya kimataifa ya kuboresha elimu.

Hizo shule zipo na ni nyingi tuu. Watu wanasukumia kwingine eti ni kwa mikoa ambayo haijaamka kielimu, what a shame? This is Tanzania na hao watu watakuja siku moja kuuliza kwa nini mnajenga four lane roads Chalinze - Segera wakati wao hata shule ndo hizo.

It is our hypocrisy to the core. We cheat and cheat and cheat. Lakini mficha maradhi .......................
 
Hili ni tatizo la viongozi wetu kutotilia mkazo elimu, watoto wao wanasoma shule za private hawana mda wa kuangalia shule za serikari.
 
Kuna shule nyingine naijua. Ina majengo mazuri sana ya MMEM (wahusika hawakuiba huko) na ina watoto 500. Ila ina waalimu watatu tu (Mwalimu mkuu, mke wake na mwlimu mwingine mmoja). Darasa la kwanza hadi la saba. Kuna shule hapo? Let's be serious.

Ukiuliza serikali wanakwambia budget haitoshi. Kaangalie luxuries za masafari yasiyoisha na misafara ya rais. Ukifanya project moja ndogo tu, ukapunguza magari matatu katika msafara wa rais. Ukapunguza safari za rais nje ya nchi kwa nusu. Ukaondoa malipo ya per-diem kwa maofisa wa serikali wanaosafiri huku wamelipiwa full board (badala yake ukawalipa 20% incidental allowance); shule hizo itakuwa historia katika kipindi cha miaka mitano tuu.

Tunaomba kwa sababu tuna-mentality za kimaskini. We have all the money arround, ila haziendi huko zinapotakiwa kwenda. Hatuhitaji hata kuomba.

Kuna kodi nyingi mno kwa watanzania wa kawaida wanaopigania shilingi. Hizo hela zinakwenda wapi? We need a second independence!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom