shukurani yake kwa tovuti ya Facebook

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Baba mmoja nchini Misri amempa mtoto wake mchanga jina la Facebook kama shukurani yake kwa tovuti ya Facebook kwa kusaidia kuwaunganisha Wamisri katika kumung'oa dikteta rais Hosni Mubarak aliyeitawala Misri kwa miaka 30.
Katika kusherehekea mapinduzi ya kumng'oa rais Hosni Mubarak, baba mmoja nchini Misri ameamua kumpa jina Facebook mtoto wake mchanga.

Jamal Ibrahim alikuwa miongoni mwa vijana nchini Misri walioshiriki kikamilifu katika kumshinikiza Mubarak aachie ngazi katika mapinduzi makubwa yaliyoanzia januari 25.

Kwa mujibu wa gazeti la Al-Ahram la nchini Misri, Jamal katika kuishukuru tovuti ya Facebook kwa kuwa chanzo cha kuwaunganisha waandamanaji, aliamua kumwita binti yake Facebook.

Jina kamili la mtoto wake litakuwa Facebook Jamal Ibrahim na tayari ndugu na jamaa wameanza kukusanyika nyumbani kwa Ibrahim ili kumuona mtoto Facebook.

Nchini Misri kuna watumiaji wa Facebook milioni tano, idadi ambayo ni kubwa kuliko nchi zote za mashariki ya kati.

Jumla ya makundi 32,000 yalianzishwa na Wamisri kwenye Facebook wakati wa kipindi cha mapinduzi ya kuuondoa utawala wa rais Mubarak.
 
mmh,face book.imagine,face book,facebook uko wapi face book.njoo ule face book.beatrice "nipo mwalim",mary "nipo mwalim"face book,mmh.maybe hilo jina litampa umaarufu
 
na hapa atakayelianzisha tutamuita "sura kitabu" ndilo litakuwa la mtanzania wa kwanza kuwaunganisha wapigania uhuru
 
Back
Top Bottom