Shukrani zangu za dhati kwa wanaJF baada ya Uchaguzi

Huo ni mwanzo mzuri Dada, tuko nyuma yako na tutaendelea kukuunga mkono daima.
 
Mimi Pia nakupongeza kwa jitihada ulilizozifanya ili kupata fursa ya kuwatumikia wananchi.

Lakini napenda kuwa Muwazi, SIJAFURAHISHWA NA APPROACH YAKO YA KUANIKA MAJINA YA BAADHI YA WATU HADHARANI. Amini usiamini jambo ulilolifanya lina tafsiri nyingi sana na hasa kutokana na baadhi ya watu uliowataja wana-influence kubwa kwenye jamii. Najua nitapingwa kwa hili lakini ndo hivo dada Regia nakupa constructive feedback.
Mwisho kabisa ukisoma between lines utagungua kuna issues nyingi za kuwafungua watu macho zimezungumzwa. Msinichukie Kwa sababu lengo ni kujengana pale mtu anapokosea, badala ya kujifanya kipofu!
 
regia... congrats and pole

nadhani kazi ndio inaanza sasa na tunataka hizi shukrani zije tena na tena katika kila step utakayopita

kazi ndio kwanza imeanza
 
naona wametajwa wakubwa tu tena waheshimiwa wabunge, waliotoa financial support na ma-airtime! sie wengine tuliokuwa tukichombeza jee? please usituchakachue...............

back to the point, wote tulikusupport na tunapokea shukrani zako kwa mikono miwili........ pamoja daima
 
kumbe saidi kubenea ni mkereketwa wa chadema!!! Silisomi tena gazeti la mwanahalisi maana litakuwa upande wa chadema tu badala ya kuandika hakika!!!!
Umeambiwa kaisaidia Chadema au kamsaidia Regia? Usikurupuke mkuu, Mbona kamshukuru Kafulila ambaye ni Mbunge mteule wa NCCR? Hizo ni shukrani tuu kama zile alizotoa JK kumshukuru kwanza Mke wake kabla ya kukishukuru chama chake
 
hivi umekata rufaa?

asante kwa ujasiri wako

mimi nilukusapot sana siku ile walipogoma kutangaza matokeo kumbe walikuwa wanachakachuau

tuko pamoja
 
Nikushukuru pia dada Regia kwa kutambua mchango wa wote walioshirikiana nawe katika hatua moja ama nyingine, iwe kwa namna inayoonekana au isiyoonekana.

Japokuwa wengi wetu tulitarajia ungeweza kupata nafasi ya kutangazwa mshindi. nasema kutangazwa kwa sababu naamini ulishinda ila haki ikawekwa kando. Najua iko nafasi nyingine...kwa maana "when one door is closed, the other is opened"...na pia kwa wale tulioshirikiana nawe kwa njia ya Maombi tunaamini kwamba sala zetu hazitapita bure...kwa maana Mungu wetu hawahi na wala hachelewi, yeye hujibu kwa wakati.

Tunakuamini na tunakuhitaji ukatuwakilishe bungeni na najua itakuwa hivyo kwa namna moja ama nyingine....Si tu eti kwa sababu tunakufahamu, ila kwa sababu tunajua unaweza kuleta mabadiliko yatakayowasaidia wananchi walio masikini kupitia mchango wako ndani na nje ya bunge.

Binafsi tunafahamiana tangu SUA na japokuwa niko nje ya nchi kwa muda sasa ila makazi yangu kikazi ni Ifakara na nilitamani sana uwe mbunge wangu...lakini sasa waweza kuwawakilisha hata wale walio nje ya Kilombero...yote ni mema mbele za Bwana...kwa kuwa mwisho wa siku sifa ni kwake yeye.

Mwisho niseme; uwe na moyo mkuu..ukatende kama kwa Bwana.
Uwasaidie na kuwajenga wengine ili kwa pamoja tufikie pale tunapotarajia.
 
Ndugu zangu wanaJF,habari za majukumu mbalimbali mliyonayo.

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wale wote kwa njia moja ama nyingine mmeshiriki kuniunga mkono kabla,wakati na baada ya uchaguzi.Ninathamini sana sapoti mliyonitendea sina cha kuwalipa ila Mwenyezi MUNGU atawalipa kwa niaba yangu.

Hapa ninawashukuru members wa JF tu wale walionisapoti nikiwa sijui na wale ambao nilikuwa ninafahamu.Napenda kuchukua fursa hii kuwatambua kwa majina.Samahani kwa wale ambao nitakuwa nimewasahau,orodha ni ndefu.

1.David Kafulila-ndiye aliyenihamasisha niingie CHADEMA Makao Makuu.
2.John Mnyika-Ndiye aliyenilea nilipofika makao makuu na kunisapoti mpaka dakika ya miwsho
3. Zitto Kabwe- ndiye aliyefundisha siasa za nje ya makao makuu,alinitetea kwa nguvu zote kwenye Kamati Kuu jina langu lisichakachuliwe baada ya kushinda kura za maoni
4.Dr Slaa-Amekuwa akinitia moyo na kunishauri
5.Freeman Mbowe- ndiye aliyeshauri nishiriki kwenye operesheni za chama nje ya makao makuu mfano Sangara n.k
6.John Mrema-Ushauri
7.Mzee Mwanakijiji-Alinitetea jina langu lisichakachuliwe baada ya kushinda kura za maoni,alipitia Ilani yangu na kuiboresha pamoja na kunifanyia kampeni.
8.Remmy-mchango wa hali na fedha
9.Dr Ndege ya Uchumi-Financial support
10.Erck Ongara-Financial support
11.Ben-Financial support
12.Saed Kubenea-Financial support
13.Dark City-Financial support
14.Maxence Melo-Muda wa maongezi
15.The invincible-Muda wa maongezi
16.FirstLady-Financial support
17.Firstlady1-Maombi mbele za MUNGU na kunipigia simu au kunisms kunipa moyo.
18.Bht-sms za kunitia moyo

Hawa ni wale walionisapoti nikifahamu wananisapoti lakini natambua kwamba kuna wengine mmenisapoti nikiwa sina habari,asanteni sana wote.

Nina washukuru sana wote na MUNGU awabariki sana.Tupo pamoja.Kwa wale ambao nitakuwa sijawataja majina yenu na mliniunga mkono kwa namna moja ama nyingine ninaomba radhi sana,sio lengo langu kuwasahau.

Aluta continua.
With Love Regia

Asante Regia kwa shukran. Hongera kwa kupambana hadi mwisho, wewe ni jasiri sana. Hongera kwa kuwa mfano wa kuigwa na wengi. Umeni-inspire mimi pia na Mungu akipenda nitagombea 2015. Mimi ni CCM, ninafuatilia kwa makini yanayojiri katika chama changu kabla ya kufanya uamuzi wa kuhama au kubaki. Inategemea mambo mengi sana. Mfano, kama Chenge akiwa Speaker nitakihama chama changu na possibly tutakuwa wote CHADEMA. Kama Lowasa akiwa PM nitahama chama pia. Lkn hata kama wawili hao hawatachagulia hizo nafasi, bado nitaangalia jinsi Kikwete anavyo endelea kulea mafisadi na atakavyochagua baraza la mawaziri, kama sitaridhika nitafanya uamuzi mgumu pia.
 
Dada Regia na Keil;

Kwa miaka mingi nimekuwa mpinzani wa vyama vya siasa na nikaamua kujikalia bila chama. Ila kitendo cha Said Nkumba kushinda tena na kuwa mbunge wa Sikonge, kumenitibuwa sana na sasa nataka kufanya mikakati ya kuanza kumtoa mwaka 2015.

Ningeliweza kusema nijiunge na CCM ila nafahamu kuwa huko ana mizizi yake mirefu sana na ni vigumu kumtoa. Hivyo itakuwa vema kama ntaingia na gia ya kumshambulia ndani na nje ili mradi tu atolewe. Hadi mwakani nitakuwa nimeshajipanga tayari kuingia kwenye Siasa au lahh. Ndiyo maana hadi leo hii sina Chama na kwangu mie chama si muhimu sana ila cha muhimu ni maendeleo ya Wanyamwezi wangu wa Sikonge. Nitakuwa tayari kushirikiana hata na Shetani, kama tu atakuwa tayari kuwatumikia na kuwasaidia Wanyamwezi wangu hawa.

Ngoja kwanza nijiweke sawa kimawazo maana mwaka huu umekuwa mwaka wa kushindwa kwangu. Nimempigia kampeni Mwakalinga tangu mwaka jana, tukashindwa. Tangu miaka miwili iliyopita, nilianza kampeni za Dr. Slaa for President, uppsss!!! Inasemekana tumeshinda au kushindwa kwa point chache sana ila matokeo ya mwisho, NEC wamechakachua.
Hii inanipa wasiwasi mzito sana kwa hatua nzima ya kuacha shughuli zangu na kuingia kwenye Siasa. Kuna jamaa yangu mmoja ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi na mwakani akirudi Tanzania, tutakaa na kujadili kwa kina hili swala. Tutakubaliana kati yangu na yeye nani aende na aende kwenye chama gani.

Tatizo la chama kwa Sikonge / Wanyamwezi ni kubwa sana. Kule watu wanafahamu CCM tu na hakuna zaidi. Kitendo cha kuingia kwa kutumia chama kingine inakuwa ni kujipa kazi ya ziada. Ila kuwepo tu vyama vya upinzani, kutaanza kuwapa watu wa huko Mwanga wa kufikiri kuwa Mtanzania anaweza kuwa kwenye chama chochote kile na hakuna vita itatokea. Hiyo tu inaweza kuanza kuwafungua watu macho na kuanza kufikiri au kuona mbali zaidi ya Sikonge.

Nitaendelea kuwa karibu na Kila Mtanzania bila kujali Chama ili mradi anaweka Maslahi ya Taifa mbele. Sintataka kuwa fanatic wa Siasa ambaye hata akisikia chama chake ni Mafisadi, Majambazi, wezi, wauwaji, watoa hongo, wazembe nk yeye bado anasimama na kusema bila wasiwasi Chadema Oyeeee!!!!!!

KEIL: Kabla sijanunua kadi ya Chadema, utakuwa wa kwanza kusikia na hapo ujuwe TUMEANZA KAZI. Kabla sijaenda Chadema, nafikiri nitataka kwanza kuwa na mazungumzo marefu na wewe maana msaada na ushauri wako, utakuwa ndiyo RISASI ya kwanza kwa Said NKUMBA.
Mpaka mwakani ndio ujiunge na CHADEMA,why?uko mbali sana?
 
tuko pamoja ,mapambano bado yanaendelea

Naam dada watu walipambana sana hapa kujua hatma yako jimboni.Tunakupongeza kwa changamoto uliyoionesha na usikate tamaa tumia miaka hii mitano kama alivyofanya Mnyika Ubungo, kuwekeza kwa kuwa karibu na wananchi, kusikiliza na kushirikiana nao. Naamini utashinda tu.

Safari nyingine, mi nitajitolea ushauri katika eneo moja muhimu la kitaalamu litakalosaidia kuanzia sasa hadi uchaguzi ujao. Tuwasiliane tu
 
Mimi Pia nakupongeza kwa jitihada ulilizozifanya ili kupata fursa ya kuwatumikia wananchi.

Lakini napenda kuwa Muwazi, SIJAFURAHISHWA NA APPROACH YAKO YA KUANIKA MAJINA YA BAADHI YA WATU HADHARANI. Amini usiamini jambo ulilolifanya lina tafsiri nyingi sana na hasa kutokana na baadhi ya watu uliowataja wana-influence kubwa kwenye jamii. Najua nitapingwa kwa hili lakini ndo hivo dada Regia nakupa constructive feedback.
Mwisho kabisa ukisoma between lines utagungua kuna issues nyingi za kuwafungua watu macho zimezungumzwa. Msinichukie Kwa sababu lengo ni kujengana pale mtu anapokosea, badala ya kujifanya kipofu!
Ni kweli wengine hawapendi kuanikwa majina yao hadharani,nadhani ni jambo jema kama ulishauriana nao kuwa utatoa majina yao humu kuwashukuru na wakakubali.
 
Ndugu zangu wanaJF,habari za majukumu mbalimbali mliyonayo.

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wale wote kwa njia moja ama nyingine mmeshiriki kuniunga mkono kabla,wakati na baada ya uchaguzi.Ninathamini sana sapoti mliyonitendea sina cha kuwalipa ila Mwenyezi MUNGU atawalipa kwa niaba yangu.

Hapa ninawashukuru members wa JF tu wale walionisapoti nikiwa sijui na wale ambao nilikuwa ninafahamu.Napenda kuchukua fursa hii kuwatambua kwa majina.Samahani kwa wale ambao nitakuwa nimewasahau,orodha ni ndefu.

1.David Kafulila-ndiye aliyenihamasisha niingie CHADEMA Makao Makuu.
2.John Mnyika-Ndiye aliyenilea nilipofika makao makuu na kunisapoti mpaka dakika ya miwsho
3. Zitto Kabwe- ndiye aliyefundisha siasa za nje ya makao makuu,alinitetea kwa nguvu zote kwenye Kamati Kuu jina langu lisichakachuliwe baada ya kushinda kura za maoni
4.Dr Slaa-Amekuwa akinitia moyo na kunishauri
5.Freeman Mbowe- ndiye aliyeshauri nishiriki kwenye operesheni za chama nje ya makao makuu mfano Sangara n.k
6.John Mrema-Ushauri
7.Mzee Mwanakijiji-Alinitetea jina langu lisichakachuliwe baada ya kushinda kura za maoni,alipitia Ilani yangu na kuiboresha pamoja na kunifanyia kampeni.
8.Remmy-mchango wa hali na fedha
9.Dr Ndege ya Uchumi-Financial support
10.Erck Ongara-Financial support
11.Ben-Financial support
12.Saed Kubenea-Financial support
13.Dark City-Financial support
14.Maxence Melo-Muda wa maongezi
15.The invincible-Muda wa maongezi
16.FirstLady-Financial support
17.Firstlady1-Maombi mbele za MUNGU na kunipigia simu au kunisms kunipa moyo.
18.Bht-sms za kunitia moyo

Hawa ni wale walionisapoti nikifahamu wananisapoti lakini natambua kwamba kuna wengine mmenisapoti nikiwa sina habari,asanteni sana wote.

Nina washukuru sana wote na MUNGU awabariki sana.Tupo pamoja.Kwa wale ambao nitakuwa sijawataja majina yenu na mliniunga mkono kwa namna moja ama nyingine ninaomba radhi sana,sio lengo langu kuwasahau.

Aluta continua.
With Love Regia

Mbona uweki mambo hadharani. Umesema mengi lakini ujabainisha umeshiriki uchanguzi kama mgombea au mpiga kura.

kama mgombea kwa ngazi gani , Udiwani au Ubunge.

Nini matokeo?
maoni yako dhidi ya uchaguzi huko jimboni na chama chako.
 
Dah,sikuwahi kujua kama upo jf. you are one of the few women i appreciate kwa kidiriki kwenda mbele pasipo woga wowote na kupigania kutetea wananchi,big up sana!

I suggest chadema wasikuache nje ya uteuzi wa vitimaalumu you deserve to be in the house.
 
Mimi Pia nakupongeza kwa jitihada ulilizozifanya ili kupata fursa ya kuwatumikia wananchi.

Lakini napenda kuwa Muwazi, SIJAFURAHISHWA NA APPROACH YAKO YA KUANIKA MAJINA YA BAADHI YA WATU HADHARANI. Amini usiamini jambo ulilolifanya lina tafsiri nyingi sana na hasa kutokana na baadhi ya watu uliowataja wana-influence kubwa kwenye jamii. Najua nitapingwa kwa hili lakini ndo hivo dada Regia nakupa constructive feedback.
Mwisho kabisa ukisoma between lines utagungua kuna issues nyingi za kuwafungua watu macho zimezungumzwa. Msinichukie Kwa sababu lengo ni kujengana pale mtu anapokosea, badala ya kujifanya kipofu!

Mkuu heshima mbele!!Nimekupata vizuri kuhusu hofu yako.
Unayemhofia hapa nani ambaye unaona kumtaja kwake ni hatari? je ni Kubenea?kama ni ndugu yangu je hana haki ya kunichangia kwa kuwa niko CHADEMA? Je ni Maxence,kama ni ndugu yangu je hana haki ya kunichangia kwakuwa yeye ni mtu neutral na je hata kama hawa wote wawili sio ndugu zangu lakini wanaukaribu na mimi hawana haki ya kunisapoti?je ni Mwanakijiji mbona maefanya hayo hadharani?ni nani hapa unayemhofia basi?Jamani mimi ninaamni kabisa demokrasia ya nchi imekuwa kwa kiwango fulani sasa habari za watu kuwekewa mipaka halafu watu hao wakakubaliana na hoja hizo basi ni utumwa.Mi siku zote ni muwazi na mkweli.Ukweli will always prevail.
 
Dada Regia na Keil;

Kwa miaka mingi nimekuwa mpinzani wa vyama vya siasa na nikaamua kujikalia bila chama. Ila kitendo cha Said Nkumba kushinda tena na kuwa mbunge wa Sikonge, kumenitibuwa sana na sasa nataka kufanya mikakati ya kuanza kumtoa mwaka 2015.

Ningeliweza kusema nijiunge na CCM ila nafahamu kuwa huko ana mizizi yake mirefu sana na ni vigumu kumtoa. Hivyo itakuwa vema kama ntaingia na gia ya kumshambulia ndani na nje ili mradi tu atolewe. Hadi mwakani nitakuwa nimeshajipanga tayari kuingia kwenye Siasa au lahh. Ndiyo maana hadi leo hii sina Chama na kwangu mie chama si muhimu sana ila cha muhimu ni maendeleo ya Wanyamwezi wangu wa Sikonge. Nitakuwa tayari kushirikiana hata na Shetani, kama tu atakuwa tayari kuwatumikia na kuwasaidia Wanyamwezi wangu hawa.

Ngoja kwanza nijiweke sawa kimawazo maana mwaka huu umekuwa mwaka wa kushindwa kwangu. Nimempigia kampeni Mwakalinga tangu mwaka jana, tukashindwa. Tangu miaka miwili iliyopita, nilianza kampeni za Dr. Slaa for President, uppsss!!! Inasemekana tumeshinda au kushindwa kwa point chache sana ila matokeo ya mwisho, NEC wamechakachua.
Hii inanipa wasiwasi mzito sana kwa hatua nzima ya kuacha shughuli zangu na kuingia kwenye Siasa. Kuna jamaa yangu mmoja ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi na mwakani akirudi Tanzania, tutakaa na kujadili kwa kina hili swala. Tutakubaliana kati yangu na yeye nani aende na aende kwenye chama gani.

Tatizo la chama kwa Sikonge / Wanyamwezi ni kubwa sana. Kule watu wanafahamu CCM tu na hakuna zaidi. Kitendo cha kuingia kwa kutumia chama kingine inakuwa ni kujipa kazi ya ziada. Ila kuwepo tu vyama vya upinzani, kutaanza kuwapa watu wa huko Mwanga wa kufikiri kuwa Mtanzania anaweza kuwa kwenye chama chochote kile na hakuna vita itatokea. Hiyo tu inaweza kuanza kuwafungua watu macho na kuanza kufikiri au kuona mbali zaidi ya Sikonge.

Nitaendelea kuwa karibu na Kila Mtanzania bila kujali Chama ili mradi anaweka Maslahi ya Taifa mbele. Sintataka kuwa fanatic wa Siasa ambaye hata akisikia chama chake ni Mafisadi, Majambazi, wezi, wauwaji, watoa hongo, wazembe nk yeye bado anasimama na kusema bila wasiwasi Chadema Oyeeee!!!!!!

KEIL: Kabla sijanunua kadi ya Chadema, utakuwa wa kwanza kusikia na hapo ujuwe TUMEANZA KAZI. Kabla sijaenda Chadema, nafikiri nitataka kwanza kuwa na mazungumzo marefu na wewe maana msaada na ushauri wako, utakuwa ndiyo RISASI ya kwanza kwa Said NKUMBA.

Mkuu nimekupata vizuri sana.Tupo pamoja.Kuhusu hofu yako ya UCCM huko kwenu na wewe kufanya kazi ya ziada ili kuuzima wala usitie shaka,wananchi wakikukubali tu kazi inakuwa nyepesi ila wasipokukubali hali ndio inakuwa ngumu kidogo.Kilombero ilikuwa ni strong hold ya CCM na watu wengi walijua ninaenda kujifurahisha,hata CCM wenyewe walijua hivyo.Lakini pamoja na Ulemavu na Uanamke wangu nilitikisa kwenye kampeni kiasi kwamba ilibidi waongeze nguvu za ziada,chafu na nzuri ili washinde.Nimeandika historia ya aina yake katika jimbo hili,nitaeleza baadaye kwa mapana yake.Ukijua wananchi nini wanataka na wakakukubali basi ni rahisi sana kuiondoa CCM.Hakuna chama chenye hati miliki.Nimejifunza mengi kupitia uchaguzi huu.
 
Dada Regia,

Hongera kwa kampeni nzuri na pole kwa hujuma mbaya uliyofanyiwa. Kama nilivyosema nitakuwa tayari kutoa msaada wa kisheria pindi itakapohitajika. Lakini unatakiwa kufungua kesi mapema kwani muda ni siku 14 baada ya matokeo kutangazwa. Itakuwa vizuri nikipata simu yako ili tuweze kuwasiliana katika suala hilo.

Asante na mapambano yanaendelea kwa nguvu zote.
 
Mkuu asante sana.Tupo pamoja.Kwa mujibu wa sheria mpya kufungua kesi ni siku 30 baada ya matokeo.NakuPM ili nikupe nama zangu.
 
Back
Top Bottom