Shukrani zangu za dhati kwa wanaJF baada ya Uchaguzi

Ndugu zangu wanaJF,habari za majukumu mbalimbali mliyonayo.

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wale wote kwa njia moja ama nyingine mmeshiriki kuniunga mkono kabla,wakati na baada ya uchaguzi.Ninathamini sana sapoti mliyonitendea sina cha kuwalipa ila Mwenyezi MUNGU atawalipa kwa niaba yangu.

Hapa ninawashukuru members wa JF tu wale walionisapoti nikiwa sijui na wale ambao nilikuwa ninafahamu.Napenda kuchukua fursa hii kuwatambua kwa majina.Samahani kwa wale ambao nitakuwa nimewasahau,orodha ni ndefu.

1.David Kafulila-ndiye aliyenihamasisha niingie CHADEMA Makao Makuu.
2.John Mnyika-Ndiye aliyenilea nilipofika makao makuu na kunisapoti mpaka dakika ya miwsho
3. Zitto Kabwe- ndiye aliyefundisha siasa za nje ya makao makuu,alinitetea kwa nguvu zote kwenye Kamati Kuu jina langu lisichakachuliwe baada ya kushinda kura za maoni
4.Dr Slaa-Amekuwa akinitia moyo na kunishauri
5.Freeman Mbowe- ndiye aliyeshauri nishiriki kwenye operesheni za chama nje ya makao makuu mfano Sangara n.k
6.John Mrema-Ushauri
7.Mzee Mwanakijiji-Alinitetea jina langu lisichakachuliwe baada ya kushinda kura za maoni,alipitia Ilani yangu na kuiboresha pamoja na kunifanyia kampeni.
8.Remmy-mchango wa hali na fedha
9.Dr Ndege ya Uchumi-Financial support
10.Erck Ongara-Financial support
11.Ben-Financial support
12.Saed Kubenea-Financial support
13.Dark City-Financial support
14.Maxence Melo-Muda wa maongezi
15.The invincible-Muda wa maongezi
16.FirstLady-Financial support
17.Firstlady1-Maombi mbele za MUNGU na kunipigia simu au kunisms kunipa moyo.
18.Bht-sms za kunitia moyo

Hawa ni wale walionisapoti nikifahamu wananisapoti lakini natambua kwamba kuna wengine mmenisapoti nikiwa sina habari,asanteni sana wote.

Nina washukuru sana wote na MUNGU awabariki sana.Tupo pamoja.Kwa wale ambao nitakuwa sijawataja majina yenu na mliniunga mkono kwa namna moja ama nyingine ninaomba radhi sana,sio lengo langu kuwasahau.

Aluta continua.
With Love Regia

Pole na hekaheka na hongera kwa kumaliza salama.
Aisee kumbe huko pia kuna kuchakachua <joke>.
 
kumbe saidi kubenea ni mkereketwa wa chadema!!! Silisomi tena gazeti la mwanahalisi maana litakuwa upande wa chadema tu badala ya kuandika hakika!!!!

Mkuu umeelewa mada inayojadiliwa au umeamua tu kuingia? Elewa swali lataka nini kabla ya kulijibu. Watu wanajadili mambo ya dadaetu we unaleta ushabiki wa kifisadi? Anyways kwanini usiseme
kumbe saidi kubenea anawapinga mafisadi?!!! Silisomi tena gazeti la mwanahalisi maana litakuwa upande wa wapenda tanzania na wasiokuwa wabinafsi tofauti na wakuu wangu wa chama cha mapinduzi wanaojitahidi kuitafuna nchi na kulindana?
 
Umepigana kiume (no pun intended) Mwanangu Regia na nakuomba ukumbuke kuwa kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi. Mapambano dhidi ya manyang'au na walafi wanaokula bila kunawa ndio kwanza kabisa yanaanza kwani kwa kuchakachua kura ndio sasa wamemwaga petroli kwenye moto tuliouwasha. Nakutakia kila la heri katika hatua yoyote utakayochukua kulisambaratisha hilo genge la wahuni na wezi. Mapambano yanaendelea hadi kieleweke, a luta continua !
 
kumbe saidi kubenea ni mkereketwa wa chadema!!! Silisomi tena gazeti la mwanahalisi maana litakuwa upande wa chadema tu badala ya kuandika hakika!!!!
Endelea kusoma UHURU na MZALENDO hujalazimishwa kusoma mwana halisi!hupunguzi chochote coz sidhani hata kama unanunua gazeti zaidi ya kuvizia watu wanunue!
Wajanja wataendelea kusoma mwanahalisi na mwananchi kama kawaida.
 
Kama utakuwa unagombea kupitia CCM, mimi naomba usinipe mwaliko.

Keil;

Nimeanza kuogopeshwa na habari hii ya Dada Regia maana kuna sehemu anaonyesha kuwa nusura"uchakachuaji"umuondoe kugombea ingawaje alishinda kidemokrasia kwenye kura za maoni;kamshukuru sana Mbunge Zitto Kabwe kuwa ndiye aliyemsaidia"asichakachuriwe"!

Keil;

Nakuhakikishia kuwa mwaka 2015 ndani ya CHADEMA-kyela nitashinda kura ya maoni tena kwa urahisi kabisa lkn ukifanyika "uchakachauji" na kutengua ushindi wangu nilioshinda kidemokrasia basi sitakuwa na jinsi ingine zaidi ya kwenda chama kingine ambapo kwa urahisi kabisa nitashinda Ubunge!

"Uchakachuaji" ukifanyika basi yatajirudia tena kama yale yale ya kijana Kafulira kule Kigoma!
 
Binafsi niliguswa sana na kilichokuwa kinaendelea Kilombero, kuanzia taarifa za wewe kushinda na baadae kutangazwa kuwa umeshindwa. Pole sana na Hongera kwa mapambano uliyoonyesha-nimekubali kumbe wanawake mnaweza.

Lakini wengi tunapenda kujua nini kilitokea tangu unaongoza kwa kura 1212 hadi kushindwa kwa tofauti ya kura karibu 5000. Experience yako itatusaidia kurekebisha pale tulipokosea au pale tulipolegea wakachakachua matokeo.

Hata kama hutakuwa tayari kuweka wazi basi hata kwa email zetu kama: kamakabuzi@yahoo.com. Mimi nilikuwa Karagwe wakati wa uchaguzi, kilichotokea kwa Deusdedith Jovin Kahangwa inawezekana kikashabihiana na kilichotokea kwako.
 
Dada Regia,
Hongera sana. Kwangu mimi wewe ni mshindi....umetuma ujumbe mzito mno kwa jamii. Wana Kilombero wanalijua hilo.
Mungu ni mwaminifu.
Naamini utapata viti maalum.
 
Dada regia, Mimi napenda kuwashukuru wote wale waliokuwa wanatujuza kuhusu wewe na mchakato kilombero. Nilipata picha kwamba ulishinda lakini ccm wakachakachua. Kama ni kweli, je utakata rufaa?
 
kama ilivyokuwa kwa mnyika, nakuomba usipotee katika jimbo husika. Mwaka 2015 utakuwa ni lulu katika jimbo hilo kama alivyokuwa mnyka jimbo la ubungo. kutokana na kutambua utendaji wako nafahamu kuwa utakuwa ni msaada mkubwa kwa madiwani na wabunge wa chadema kimkakati ili kuhakikisha chadema inatimiza matarajio waliyonayo wananchi.
 
Dada Regia,
Hongera sana. Kwangu mimi wewe ni mshindi....umetuma ujumbe mzito mno kwa jamii. Wana Kilombero wanalijua hilo.
Mungu ni mwaminifu.
Naamini utapata viti maalum.

Ni kweli atapata viti maalum lakini atetee haki yake ya kuchaguliwa na wananchi kisha nafasi ya viti maalum atampatia mwingine baada ya kushinda mahakamani.
 
chadema, mpelekeni huyu dada bungeni kwa viti maalum bila ya kujali kuwa ana strong case to present kwenye uchaguzi wa jimbo la kilombero.
chadema mnaweza kuacha kupeleka kesi zozote kupinga matokeo mahakamani kwa kuwa hakuna uwanja sawa hata mahakamani kwani hata urais haupingwi kokote!
 
Regia,
Hongera sana kwa kuthubutu, mafisadi wamebana safari hii , lakini huu ni mwanzo, 2015 watachia. Mungu akubariki.
 
Mpwa umenisahau nilikuwa nakuombea sana ushinde...na ukashinda ila hukutangazwa mshindi...ntazidi kukuombea
 
Don't 4get one thing Regia...

Kampeni ndio zinaanza... Jipange, tujipange, tuhakikishe kuwa piga ua garagaza, next time kama sio yote, bas zaidi ya nusu ya majimbo ya Morogoro yanakwenda CHADEMA. Naamini katika wagombea ubunge na wanaharakati wa CHADEMA wa Morogoro, we ni mmoja wa walio juu. Tunahiitaji msaada wako wa hali na mali kuukomboa huu mkoa...
 
Pongezi dada Regia kwa hatua kubwa uliyopiga come 2015 we will be there for you again.
 
Kila la Kheri Regia Mtema ( Mb Kilombero)

Kwangu mimi wewe ni Mbunge Mteule ambaye hakutangazwa na Tume ya Manyang'au

Mapambano ndio kwanza yameanza
 
Hongera sana...ubarikiwe katika haya mapambano..! hatulali mpaka kieleweke!!
 
Back
Top Bottom