Mzee Mwanakijiji,Kwa kawaida - na karibu mara zote - shujaa wa kwenye filamu hauawi. Hata apitie matatizo kiasi gani tunajua kuwa mwisho wa siku shujaa wetu ataendelea kuwepo. Ndio maana ya ule msemo wa "sterling hauawi". Lakini kuna kitu kingine ambacho ni kweli pia, shujaa hatokei mwisho wa movie! Hata kama atachelewa kidogo kutokea lakini mara moja tutatambulishwa kuwa huyu ni shujaa wetu na toka mwanzo tutamuona anvyopambana na mgogoro. Fikiria shows kama 24 au filamu kama za Rambo, n.k
Sasa inakuwaje kwenye filamu uangalie hadi mwisho hadi kisa kimekwisha halafu shujaa anatokea? Fikiria kuwa umeangalia movie nzima na matukio yote muhimu yametokea na filamu imeshaandikwa "the end" halafu credits zina roll down halafu shujaa anatokea na kuanza kuelezea jinsi ambavyo angeweza kupambana na maadui au jinsi gani maadui walivyoshindwa! Kwanza itabidi ujiulize kama ni shujaa kweli na kama ni shujaa basi unajiuliza ni shujaa wa kitu gani!
Nilichojifunza ni kuwa shujaa hatokei mwisho wa filamu kupewa sifa!
MMM
Katika sinema karibu zote za Hostage taking, shujaa huwa yule aliyemaliza mgogoro japokuwa Acadamy winner wa perfomance anaweza kushinda mtu mbaya. Kuna sinema ya Danzel na pia Samuel Jackson zote zinaonyesha Hostage taking ktk hospital na wana sababu za maana kabisa kiasi kwamba wakaitwa mashujaa lakini behind the scene ushajaa wao haukumalizika vizuri isipokuwa yule aloweza kumaliza mgogoro wao...Hakuna sinema nzuri isiyiokuwa na maafa zaidi, we tend to love movie kwa ushenzi uliomo na sio hekima inayotumika...
Katika mgogo huu wa madaktari hukuniona wala hutaniona mimi nikiwapongeza Madaktari wala JK. Wengi hapa JF mlimpongeza JK kwa kumaliza mgogoro lakini ajabu ni kwamba pongezi hizo zikawa withdrawn kwa sababu tu hakuzungumza mlichokitaka...Binafsi yangu tatizo la huduma ya Afya nchini ni sugu na linahitaji sii tu mgawanyo wa fedha (keki ya Taifa) au allocation bali mfumo mzima kuvunjwa..Hili nyote mnalikimbia japokuwa mnajua fika ndio msingi wa matatizo yote.
Na inasikitisha sana kuona kwamba sisi Watanzania we never learned through mistakes ambazo zilitangulia kuondolewa kwa Lowassa, Msabah, Karamagi, Nyoni na leo tunataka Mponda na Nkya ili hali tunajua fika kwamba vita yetu ni UFISADI - na serikali haiwezi kuacha wala kupunguza matumizi yake ili kuboresha vyanzo vya huduma zetu iwe maji, umeme, afya, elimu na hata ukusanyaji wakodi na kadhalika. SERA za chama CCM ni chukua chako mapema sasa tukitaka kubadilisha sera hizo ziwe kwa kila mtu kwa nafasi yake... Then, nyote kwa ujumla wenu hamuitakii mema nchi yetu.